Nimeukumbuka wimbo wa "Ambassadors Choir" ya Rwanda, waliouimba baada ya wenzao kufa kwa ajali ya basi huko mkoani Mbeya wakiwa ziarani nchini Tanzania. Waliimba hivi, "KWA NINI UMERUHUSU?". Walikuwa wakimlilia MUNGU aliyeruhusu ajali itokee na wenzao wakafa. Hii ni kwa sababu hata Shetani hawezi kumdhuru mwanadamu kama MUNGU hajaruhusu, Kumbuka hadithi ya Ayubu, pale MUNGU alipokutana na Shetani akamhoji, Unatoka wapi wewe? Naye akajibu "Ninatoka huku na huko na humo" .............,....Mbona mama aliyesema tusitupe sukari ziwani nae hali ni tete!
Mimi ninamlilia MUNGU aliyetuletea utawala huu wenye kiburi cha ajabu na ambacho tulio waamini watuwakilishe wanaendelea kusifu hata pale wanapowashuhudi wenzao wakianguka na kufa kila uchwao. Kilangila.