Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Ilishavuja hii.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anayetafutwa ni Mr katelephoneBado movie inaendelea hawa wote sio target kuna mtu anatafutwa haswa.
Target bado haijafikiwa hizi zote zinapigwa " deflection " tu ni kama mawimbi ya bahari kabla ya bahari kuchafuka rasmi.
Nilishasema siku miingi kuwa chama kinaporomoka na hakika waendelee kujifariji lakini Mene Mene Tekeli na Peresi imeshaandikwa.
Taarifa zilizotufikia usiku huu ni kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amejiuzulu nafasi yake hiyo.
Vyanzo vyetu vilivyo karibu na CCM vimethibitisha kuwa tayari Chongolo amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.
Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama (NEC), ambavyo vinafanya vikao vyake vya kawaida jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2023, huenda vikampitisha Katibu Mkuu mpya wa CCM ambaye atachukua nafasi ya Chongolo.
Sababu za kujizulu kwa Chongolo tutawaletea baadae.
=====
UPDATES: 28 NOV 2023
======
JamiiForums imejihakikishia kuwa ni barua aliyoandika mwenyewe ila taarifa za kuwa amepata ajali si za kweli bali gari lake lilihusika na ajali mapema Machi/Aprili.
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 01 Mei 2021 iliza nafasi ya Ukatibu Mkuu iliyoachwa tangu Machi 26, mwaka 2021, kwa kumteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.
Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya aliyekuwa akiishikilia, Dk Bashiru Ally, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Itakumbukwa kuwa wakati Dk Bashiru anateuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, nafasi aliyoihudumu kwa kipindi cha miaka miwili na miezi minane.
Nyota ya Chongolo kupanda kisiasa ilianza kuonekana zaidi tangu Juni 27, 2016 wakati Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli, alipomteua Chongolo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido.
Julai 28, 2018, Chongolo alihamishwa kutoka Wilaya ya Longido kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Dar Es Salaam
Akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni alifanya mambo Mbalimbali.
1). Novemba 6, 2018 Chongolo aliiagiza Polisi Kata ya Kijitonyama kuwakamata wanaume wanaonunua machangudoa.
2). Septemba 22, 2019, aliunda kamati ya watu sita kuchunguza tukio la ajali ya moto uliotekeleza Hoteli ya Coco Beach.
3). Novemba 9, 2019, alitekeleza agizo la Rais John Magufuli, la kumrudishia nyumba bibi mwenye umri miaka 80, Amina Muhenga, aliyoidai zaidi ya miaka 30.
4). Januari 17, 2020, Chongolo alipiga marufuku wanafunzi walioanza kidato cha kwanza mwaka huo kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kutokuwa na sare za shule.
5). Februari 25, 2020, alisema wilaya yake ilitenga Sh3.4 bilioni kwa ajili ya kuwakopesha wanawake, vijana na wenye ulemavu katika bajeti ya mwaka 2020/21.
6). Januari 10, 2021, alifanya operesheni maalum iliyofichua nyumba zinazohifadhi watu wenye ulemavu wanaotumika kuomba jijini Dar es Salaam.
7). Aprili 1, 2021, alitoa siku 21 kwa wataalamu wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka (Dawasa) kwenda kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Kata ya Mbezi Juu. Nk
29, 2013 BY ZANZIBARIYETU
Hamkani Si Shwari Tena
Ahmed Rajab
NOVEMBA
Ahmed Rajab
NOVEMBA 1960 Chinua Achebe, mshairi na mwandishi wa riwaya wa Nigeria aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita akiwa na umri wa miaka 82, alifunga safari yake ya kwanza kuja Afrika ya Mashariki na ya Kati. …
Alifika Kenya, Uganda, Tanganyika na Zanzibar. Baadaye alizizuru Rhodesia mbili — ya Kaskazini (sasa Zambia) na ya Kusini (Zimbabwe).
Aliyoyaona yalimshangaza na kumshtua. Alikumbana na ukabila na ubaguzi.
Mshangao wa mwanzo aliupata wakati ndege aliyopanda ilipokuwa inakaribia kutua uwanja wa ndege wa Nairobi. Abiria walipewa fomu za uhamiaji kujaza. Akaona kuna vijisanduku vinne vya kuchagua kwenye fomu hiyo: kimoja kiliandikwa ‘Mzungu’, vingine ‘Mwasia’, ‘Mwarabu’ na cha mwisho kiliandikwa ‘Mwingine’.
Mwafrika alikua ‘mwingine’. Wakoloni walimnyima utu wake. Walifika hadi hata hatua ya kumpokonya ubinadamu wake.
Achebe alizizuru sehemu za huku kwetu mwezi mmoja baada ya Nigeria kupata uhuru wakati ambapo nchi zetu zilikuwa bado zikitawaliwa na Mwingereza ingawa zilikuwa karibu kupata uhuru.
Alipofika Tanganyika na Zanzibar, Achebe alifadhaishwa na namna Mwafrika alivyokuwa akidharauliwa na wasio Waafrika.
Jijini Dar es Salaam alisoma magazetini jinsi klabu moja ya wazungu ilivyokuwa ikijadiliana kubadili kanuni za klabu hiyo ili Julius Nyerere aweze kukaribishwa na mwanachama wa klabu kwenda kunywa pombe klabuni humo, ingawa hatujui iwapo Nyerere mwenyewe alitaka kunywa katika klabu hiyo.
Wakati huo Nyerere alikuwa amekwishachaguliwa waziri mkuu wa serikali ya mwanzo ya madaraka ya ndani.
Kuna maudhi mengine aliyoyaona. Kwa mfano, yale yaliomfika Mtanganyika mmoja tajiri mwenye asili ya Kihindi na ambaye Achebe alisema alikua ‘mtu mwema’.
Jamaa huyo alimlalamikia kwamba japokuwa alizaliwa Tanganyika na hakuwa na kwingine pa kukimbilia na ijapokuwa alitoa fedha nyingi za sadaka kuwafadhili wananchi wenzake Wakiafrika, bado hao wenzake hawakumkubali wala hawakuwa wakimuamini. Sababu ilikuwa damu yake ya Kihindi. Ilikuwa kama ya kunguni, ikinuka.
Inasikitisha kwamba ubaguzi aina hiyo bado upo nchini Tanzania ingawa tunajidai kuufumbia macho kana kwamba haupo.
Akiwa Dar es Salaam, Achebe alihudhuria mkutano wa kisiasa uliopangwa kuukosoa uongozi wa Nyerere. Mkutano wenyewe uliongozwa na Bibi Titi Mohamed, ambaye Achebe alimuelezea kuwa ni ‘kiongozi wa ajabu wa tawi la wanawake la TANU’.
Lawama hizo hazikutolewa kwa ukali bali zilitolewa kwa upole mno ukidhania kama vile badala ya kumkosoa Nyerere zilikua na lengo la kumdekeza.
Achebe alishangazwa na hali ya mkutano huo kwani mwanzo mwanzo aliuona kuwa kama uliopwaya akiulinganisha na mikutano ya hadhara ya kisiasa ya kwao Nigeria ambayo ni ya fujo, ghasia na kelele.
Mambo yaligeuka aliponyanyuka Nyerere kuhutubu. Aliposimama Nyerere kujitetea, Achebe alipigwa na bumbuwazi. Licha ya kwamba alimtegemea mkalimani wake kwani hakukijua Kiswahili, hata hivyo alivutiwa na balagha ya kisiasa ya Nyerere, ufasaha wake wa kusema. Na kusema Nyerere akisema, wakati mwingine akinguruma.
Miongoni mwa Watanganyika mashuhuri aliokutana nao Achebe ni Mtwa Mkwawa yaani Chifu Adam Sapi – mjukuu wa Sultan Mkwawa wa Wahehe, na aliyekuwa Spika wa bunge la kwanza la Tanganyika huru.
Achebe alipokewa vizuri alipoalikwa kwenda kunywa chai kwa Chifu Adam Sapi, mtu aliyekuwa mpole na mwenye haya. Siku ya pili alipokuwa Achebe anafunga begi lake kwa safari ya kurudi Dar es Salaam alisikia mtu akipiga hodi kwenye mlango wa chumba chake cha hoteli.
Alipofungua mlango alimkuta Chifu Adam Sapi Mkwawa amesimama akiwa na mshale mdogo wa Kihehe aliomtunukia zawadi.
Mtanganyika mwingine mashuhuri aliyekutana naye Achebe wakati wa ziara yake ya Tanganyika alikuwa mshairi Sheikh Shaaban bin Robert aliyemtembelea nyumbani kwake.
Pamoja na kuwa mshairi, Shaaban Robert alikuwa pia mwandishi wa riwaya, mwandishi wa insha na alitafsiri kwa Kiswahili mkusanyiko wa mashairi ya Omar Khayyam, mshairi wa kale wa Kiajemi ‘Rubaiyat ya Omar Khayyam’. Mkutano wa Shaaban Robert na Achebe ulikuwa wa aina yake kwani Shaaban Robert alizungumza kwa Kiswahili na Achebe kwa Kiingereza.
Ingawa walizungumza sana kuhusu fasihi, Shaaban Robert hakuwahi kuyasoma maandishi ya Achebe na Achebe naye hakuwahi kuyasoma ya Shaaban Robert aliyekuwa akiandika kwa Kiswahili.
Hata hivyo walipoagana, Shaaban Robert alimtunukia Achebe zawadi ya vitabu viwili vya mashairi yake.
Walipokutana kitabu cha kwanza cha Achebe na kilichompa umaarufu mkubwa ‘Things Fall Apart’ kilikuwa bado hakijatafsiriwa kwa Kiswahili. Kitabu hicho cha riwaya kilichochapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1958 kimetafsiriwa mara mbili kwa Kiswahili.
Kilitafsiriwa kwanza na Mohamed Mlamali Adam mwaka 1972 na kikapewa jina la ‘Hamkani si Shwari Tena’. Mara ya pili kilitafsiriwa mwaka 1973 na Clement Ndulute na kuitwa ‘Shujaa Okonkwo’.
Mbali na Kiswahili, kitabu hicho kimetafsiriwa pia katika lugha 49 nyingine na kimeibuka kuwa ni kitabu muhimu sana katika ile iitwayo fasihi ya Kiafrika.
Wiki iliyopita wengi walioandika kuhusu maisha ya Achebe walimuelezea kuwa yeye ndiye ‘baba wa fasihi ya Kiafrika’ na wengine walisema kuwa yeye ni ‘babu’ wa fasihi hiyo. Sikubaliani nao.
Sikubaliani nao kwa sababu kabla ya Chinua Achebe kuanza kuchapisha riwaya zake alizoziandika kwa lugha ya Kiingereza, tayari kulikuwako riwaya za waandishi kama akina Amos Tutuola na Cyprian Ekwensi.
Na wala kutomtambua Achebe kuwa baba au babu wa fasihi ya Kiafrika iliyoandikwa kwa Kiingereza hakumvunjii heshima yake. Bado ataendelea kuwa mmoja wa waandishi gwiji wa fasihi ya Kiafrika, msanifu riwaya aliyebuni mtindo wa aina yake wa uandishi wa riwaya uliojikita katika mazingira ya kijamii ya Kiafrika.
Ingawa niliwahi kukutana naye mara kama tatu hivi – zote jijini London, hata hivyo sikuwa nikimjua Chinua Achebe kama nimjuavyo, kwa mfano, Ngũgĩ wa Thiong’o au Nuruddin Farah au Taban Lo Liyong au Abdulrazak Gurnah miongoni mwa waandishi wa Kiafrika wanaoandika kwa Kiingereza (ingawa Ngũgĩ haandiki tena riwaya kwa Kiingereza) au mshairi wa Kiswahili Abdilatif Abdalla au mwandishi wa riwaya za Kiswahili, Adam Shafi – mmoja wa watu walionifungua macho kisiasa.
Pia sijapata kuwa mshabiki wa misimamo yake ya kisiasa hasa msimamo wake wa awali wa kuunga mkono kuzaliwa kwa Jamhuri ya Biafra, jimbo la Kusini-Mashariki mwa Nigeria lililojitenga Mei 30, 1967. Kutangazwa kwa jamhuri hiyo kulisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Nigeria vilivyoendelea kuanzia Julai 1967 hadi Januari 1970.
Kwa hakika, nakumbuka niliuponda sana msimamo wake wa kisiasa nilipokuwa nakichambua kitabu chake cha ‘The Trouble With Nigeria’ katika jarida la ‘Africa Events’ mwaka 1984.
Nilimshambulia kwa kutolizingatia suala la tabaka za kijamii katika uchambuzi wake wa siasa za Nigeria.
Juu ya yote hayo, mara zote nilizokutana naye nilizidi kumheshimu kwa unyenyekevu na upole wake. Ni mtu aliyekuwa hana kiburi wala hakuwa akijiona kama alivyo mwandishi mwenzake wa Nigeria, Wole Soyinka. Tena Achebe alikuwa na tabasamu ya sumaku.
Kifo cha Chinua Achebe kimelitia bara la Afrika katika huzuni. Nina hakika kwamba katika pembe au kona moja ya Afrika au miongoni mwa wapenzi wake kifo hicho kimezusha hali ya hamkani na mambo si shwari tena
Truehata asingepata kashfa angetoka tu ni vigumu kwa WATOTO kuelewa
Mkuu hivi kuna siku uliwaza mtu kama sabaya angeweza kulala hata kituo cha polisi kweli? Jela tuliizoea kwa watu kama mbowe na lema ila sio sabaya, amini usiamini sabaya alishanyolewa upara bila kupendaSiku gani,?mlimsema sabaya ,leo hii kawapiga nje ndani,yuko uraiani,mtakufa kihoro
Hili jambo umeandika ni kubwa sana. Kinana anafuatia.Sababu za kujiuzulu Chongolo ni kukimbia kukaa meza moja na muuaji Makonda.
Sent using Jamii Forums mobile app
Labda juu ya maweUmekuja umesoma na umetia lako.
CCM juu, juu, juu zaidi.
Ajali siyo ya juzi na hakuwepo…soma habariTrue
Siajabu hata Ile ajali ya juzi ilipangwa kama Mbowe alivyopangiwa dodoma ya konyagi🐒🐒
Wewe usiige ya Mjaliwa.Kuna barua feki inatembezwa au kusambazwa mitandoni eti chongolo Kajiuzulu.
Chongolo hajajiuzulu yupo ofisini anachapa kazi. Hii barua ni fake..angalia hata paragraph ya Mwisho. Mmegushi hata saini yakeView attachment 2827408
Sasa wameamua wenyewe kuweka wazi.Habari ndio hiyo!.
Wanabodi
Hii ni C&P from X
My Opinion
This is just too good to be true!.
Kwasababu, tangu baada ya kuteuliwa Mwenezi mpya, KM Chongolo was too cool, too calm na kumwacha Mwenezi atambe na ku trends.
Anayeidhinisha bajeti ya matumizi ya chama ni KM, hata yeye KM mwenyewe huwa hazunguki na a pool of media kubwa kama ya Mwenezi anayozunguka nayo na kum trendisha!.
Kwa vile kule nyuma Konda Boy akiwa RC wa DSM ni boss wa Chongolo akiwa DC Kinondoni, alimkaripia kwenye kadamnasi ya watu mkutanoni na kumuamuru! nyamaza wewe, kaa chini!.
Sasa Chongolo ni Boss wa Konda Boy, Mwenezi lazima aombe ruhusa kwa KM akubaliwe ndipo afanye ziara!. Inawezekana KM na yeye anaona dogo anafanya amsha amsha huku na kule bila yeye kuidhinisha hivyo amekuwa by passed na dogo, baada ya kugundua hilo, akaona ili kulinda hadhi na heshima yake, bora awaachie chama chao!.
If this is true, Nchimbi kaa mkao wa ...
Paskali
NB: Nimeipandisha hii story, thread ikafutwa fasta, ila hapa imepandishwa.
P
Hakuna msafi kwenye kapu la Ccm. Yaani wote wame oza.CCM nchi ishawashinda, kilichobakia ni ubishi tu kama ubishi mwingine!
Hiyo haina mashaka kabisa !!Kama ni kweli basi Makonda kiboko yao na anayefuata ni mwenyekiti, hawa Sukuma Gang msiwachukulie poa wamejipanga na wana nguvu kubwa sana.
Karibu sana Mkuu tupe really newsUandishi huo sio wa mtu anayejiuzulu... fake news
Mahakama ipi? Hatuna mahakama Tanzania, hata mkimtetea huyo mtu wenu hamuwezi kumsafisha kwa ushenzi aliowafanyia watu. Kuna siku atalipia matendo yake maovu.Peleka kesi mahakamani wewe,acha kuchafua watu,uzuri makonda yuko fit hajari maneno za wstu