Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu

Hili jambo lina mambo mengi nyuma yake.
Kwanza, kulikuwa na habari za ''kumchafua' ambazo ni kazi ya 'ndani ya CCM kupitia Vijana wao'

Pili, si kawaida barua ya kujiuzulu kuwekwa wazi. Ikiwa ameitoa Chongolo basi alikusudia kueleza Umma jambo.
Ikiwa imevujishwa na Ofisi, ni katika jitihada za kujisaifsha kwamba kilichotokea ni takwa la Chongo mwenyewe

Je, hili la Chongolo halikutarajiwa? Ukimsikiliza DAB siku alipokwenda Ofisi ndogo ya Chama alisema '' ... yeye anakosea na akikosea anaomba Msamha na kisha alimtaja Chongolo kwa kumsifia'' Hili lililonyesha kwamba kulikuwa na Ufa.
Kuondoka kwa Chongo hakuwezi kutengwa na Ujio wa DAB hata kama kuna sababu nyingine

Moja ya 'zana' anazotumia DAB ni vyombo vya habari kujitangaza. Hili alianza nalo tangu akiwa RC na Ofisi katika private media. Yote ilikuwa kuweka vyombo vya habari vya Umma na Private katika 'himaya yake.
Kazi ya kumchafua Daniel mitandaoni imefanywa na vijana , sijui ni wapi lakini ni ngumu kusema si ''vijana wake''

Tatizo ndani ya CCM kuna fukuto kubwa sana si kwa mbio za 2025 bali makundi kinzania. Ujio wa DAB ni tatizo kubwa zaidi kwasababu anahusishwa na uchafu lakini pia anakingiwa kifua. Swali kuna nani anakingiwa kifua namna hiyo?

DAB alikingiwa kifua na Mwendazake na hata baada. Wengi wa wanaCCM walikuwa wahanga pia wa utawala.
Hofu inayojaa ni kurejea zama zile ambazo DAB alikuwa kama naibu mkuu. Tangu ameingia hofu ipo wazi.

Anayeweza kurudisha nidhamu hawezi kutoka ndani ya timu ya leo, lazima atoke nje kama alivyokotwa Bushiri.

Kwa uoande mwingine, hili linaweza kuwa nusura ya Taifa , dalili za Punda kufa ni kupiga mateke!

Pascal Mayalla JokaKuu
 
Simba kuna kocha mpya na wasaidizi wake, unaelewa hilo?
 
Performance ya Chongolo kwenye chama ikekuwa chini sana. Chama kimekosa mvuto, mikutano hadi kusombelea watu. Acha apumzike.
 
Ngoja Tusubiri tuone !!
 
Kama Chongolo angekuwa hataki kufanya kazi na DAB basi angejiuzulu toka kipindi yeye ni mkuu wa wilaya na Makonda ni RC ! Lakini hadi sasa sidhani kama sababu ni Bashite…Chongolo atakuwa awezi siasa maana kwenye siasa lazima uwe tayari kufanya kazi na yeyote yule ata aliyekutukana ..sasa kama amejiuzulu kisa DAB basi ni mmoja ya watu wajinga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…