Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu

Umefikiri vyema...

Hii hoja yako, likely, imeunusa ukweli wa maamuzi ya huyu KM wenu...

Nafikiri pia, baadhi ya viongozi wakuu wa CCM hawakubaliani Paul Makonda a.k.a DAB kupewa nafasi hiyo ndani ya chama kutokana na tatizo la uadilifu wa kimaadili alilonalo huyu uliyemwita "dogo" yaani Paul Makonda..

Mimi sitashangaa hata Makamu Mwenyekiti wenu Abdulhaman Kinana akitupa jezi pia..!!
Kinana na Makonda , nani mwenye uafadhali mpaka useme hutoshangaa??.


Hivi kweli MAGUFULI amkatae mtu, JPM , Mwanausalama na Jasusi mahili , akukataee ni kwamba anakuonea wivu??.


Kama ulikataliwa na JPM, wee Jua HAUFAI TUU.

Ukweli ni kwamba Kuna watu wanapenda kua viongozi Kwa sababu tu Mabichwayao yatajaa masifa na kujiona fahari, ila huo Uongozi Huwa hawajui waufanyie nn katika kumkomboa mtanzania.
 
unaweza kuwajibika kwa hiari ukapumzike zako na familia yako, unaweza kuwajibika kwa sababu za kiafya,
unaweza kuwajibika kwa kujitathmini kwamba huna jipya tena miongoni mwa uliyoyafanya, ukatoa fursa kwa wengine,
unaweza kuwajibika kwa tuhuma tu whether ni kweli au uongo, ili kuhifadhi hadhi ya taasisi unayoitumikia na hadhi yako mwenyewe na kwamba hiyo inaweza kukupa credit ya ungwana ukapewa fursa sehemu nyingine...

unaweza ukashinikizwa kuwajibika kwa ababu za kisiasa, maadili mathalani rushwa, uwezo mdogo n.k
Yeye anatakiwa awajibike kwasababu gani katı ya hizo ulizozitaja hapo juu?
 
Kinana na Makonda , nani mwenye uafadhali mpaka useme hutoshangaa??.
Labda hakuna mwenye afadhali..

Lakini wa Abdulhaman Kinana kama nilivyosema kwa mjumbe mmoja hapo juu ni debatable, yaani mtu anaweza kubisha mpaka aoneshwe ushahidi maana husikia tu, hajawahi kuona...!

Lakini wa huyu ndugu Makonda a.k.a Bashite, huhitaji kuambiwa wala kuanza kuutafuta ushahidi wa uchafu wake..

Ndiyo maana tunajiuliza swali hili;

Kwamba, Je ina maana majambazi na wauaji (CCM) waliamua kumpa uongozi jambazi na muuaji mwenzao..?
 
Yeyote tu atayoona inafaa inakubalika ikiwa ni pamoya na kwenye baraua sambazwa
Mimi sioni sababu yoyote inayofaa kati ya hizo ulizozitaja.

Kama kuna ambayo wewe unaona inafaa, na kwasababu wewe ndiye uliyezitaja sababu hizo, naomba uniambie ni kwasababu gani unaona kuwa inafaa?

Kwanini nakuuliza wewe swali kutokana na ulichokiandika na wewe tena unasema “yoyote tu atayoona inafaa”?

Umeandika kiswahili kisicho sanifu, lakini wewe jibu swali langu tu tuachane na hoja ya kama unafahamu kiswahili sanifu au laah.
 
Mimi sioni yoyote inayofaa.

Kama kuna ambayo wewe unaona inafaa, na kwasababu wewe ndiye uliyezitaja, naomba uniambie ni kwasababu gani unaona kuwa inafaa.

Kwanini nakuuliza wewe swali kutokana na ulichokiandika na wewe tena unasema “yoyote tu atayoona inafaa”

Umeandika kiswahili kisicho sanifu, lakini wewe jibu swali langu tu tuachane na hoja ya kama unafahamu kiswahili sanifu au laah.
kwahiyo niseme sababu unayotaka au inayokupendeza wew kua hii ndio inafaa, right?

Kuwajibika ni kuwajibika tu, kuna kusaidia wew binafsi lakini kunasaidia kuretain credibility ya taasisi...

Kuwajibishwa ni kitu mbaya sana...
 
kwahiyo niseme sababu unayotaka au inayokupendeza wew kua hii ndio inafaa, right?

Kuwajibika ni kuwajibika tu, kuna kusaidia wew binafsi lakini kunasaidia kuretain credibility ya taasisi...

Kuwajibishwa ni kitu mbaya sana...
Sababu itakayonipendeza ambayo wewe umeitaja itawezekanaje na wakati sina sababu ya kuona sababu yoyote?

Wewe ndiye uitaje hiyo sababu ya sababu yako!

Rudi nyuma Soma mabandiko yako ujuwe sababu ya maswali yangu kuhusiana na sababu zako ambazo hazina sababu.

Kuwajibishwa bila sababu?
 

Taarifa zilizotufikia usiku huu ni kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amejiuzulu nafasi yake hiyo.

Vyanzo vyetu vilivyo karibu na CCM vimethibitisha kuwa tayari Chongolo amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.

Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama (NEC), ambavyo vinafanya vikao vyake vya kawaida jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2023, huenda vikampitisha Katibu Mkuu mpya wa CCM ambaye atachukua nafasi ya Chongolo.

Sababu za kujizulu kwa Chongolo tutawaletea baadae.


=====

UPDATES: 28 NOV 2023

======

JamiiForums imejihakikishia kuwa ni barua aliyoandika mwenyewe ila taarifa za kuwa amepata ajali si za kweli bali gari lake lilihusika na ajali mapema Machi/Aprili.
View attachment 2827882
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 01 Mei 2021 iliza nafasi ya Ukatibu Mkuu iliyoachwa tangu Machi 26, mwaka 2021, kwa kumteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya aliyekuwa akiishikilia, Dk Bashiru Ally, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Itakumbukwa kuwa wakati Dk Bashiru anateuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, nafasi aliyoihudumu kwa kipindi cha miaka miwili na miezi minane.

Nyota ya Chongolo kupanda kisiasa ilianza kuonekana zaidi tangu Juni 27, 2016 wakati Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli, alipomteua Chongolo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido.

Julai 28, 2018, Chongolo alihamishwa kutoka Wilaya ya Longido kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Dar Es Salaam
View attachment 2827887
Akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni alifanya mambo Mbalimbali.

1). Novemba 6, 2018 Chongolo aliiagiza Polisi Kata ya Kijitonyama kuwakamata wanaume wanaonunua machangudoa.

2). Septemba 22, 2019, aliunda kamati ya watu sita kuchunguza tukio la ajali ya moto uliotekeleza Hoteli ya Coco Beach.

3). Novemba 9, 2019, alitekeleza agizo la Rais John Magufuli, la kumrudishia nyumba bibi mwenye umri miaka 80, Amina Muhenga, aliyoidai zaidi ya miaka 30.

4). Januari 17, 2020, Chongolo alipiga marufuku wanafunzi walioanza kidato cha kwanza mwaka huo kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kutokuwa na sare za shule.

5). Februari 25, 2020, alisema wilaya yake ilitenga Sh3.4 bilioni kwa ajili ya kuwakopesha wanawake, vijana na wenye ulemavu katika bajeti ya mwaka 2020/21.

6). Januari 10, 2021, alifanya operesheni maalum iliyofichua nyumba zinazohifadhi watu wenye ulemavu wanaotumika kuomba jijini Dar es Salaam.

7). Aprili 1, 2021, alitoa siku 21 kwa wataalamu wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka (Dawasa) kwenda kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Kata ya Mbezi Juu. Nk

Chongolo ni Katibu Mkuu wa kumi wa CCM tangu chama hicho kilipozaliwa Februari 5, 1977.

Kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya, Chongolo amewahi kuwa Ofisa wa chama kwenye Idara ya Uenezi makao makuu wakati huo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi akiwa Nape Nnauye.

Pia, amewahi kuwa Mhariri wa Redio Uhuru ambayo inamilikiwa na CCM.

Kwa nyakati tofauti, Chongolo pia amewahi kuwa Katibu wa Bodi ya Shirika la Magazeti ya Chama (Uhuru na Mzalendo).
View attachment 2827893

MHESHIMIWA DR. SAMIA SULUHU HASSAN MWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

YAH; KUJIUZULU.

Kichwa cha barua chahusika.

NOVEMBA 27, 2023

Mh. Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwanza nitumie fursa hii kukushukuru wewe binafsi na Chama Cha Mapinduzi kwa kuniamini, kunilea na kunivumilia wakati wote wa uongozi wangu.

Mh. Mwenyekiti, utakumbuka kuwa Aprili 30, 2021 niliteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Uteuzi wangu ulitokana na mapendekezo yako, upendo wako na uongozi wako wenye mapenzi mema kwangu, kwa chama na taifa.

Mh. Mwenyekiti, siku chache zilizopita nimechafuliwa kupitia mitandao ya kijamii. Hali hiyo imenikumbusha wajibu wa kiongozi kuwajibika kwa maslahi ya Chama wakati wote unapotuhumiwa au kuhisiwa kufanya jambo lolote kinyume na kanuni, taratibu, miiko na tamaduni za Chama chetu.

Mh Mwenyekiti naomba uridhie ornbi langu kwako la kujiuzulu. Natambua kuwa uimara wa CCM unatokana na uongozi wako imara unaolenga kukuza na kustawisha hali ya maisha ya wananchi kijamii na kiuchumi.

Mh. Mwenyekiti sipo tayari kuona Chama Cha Mapinduzi kinachafuka kwa kuhusisha nafasi yangu ya Katibu Mkuu na uvumi wa matendo,tabia au mienendo ninayochafuliwa nayo.

Mh. Mwenyekiti kwa unyenyekevu mkubwa naomba uridhie ombi langu.

Mwisho, japokuwa si kwa umuhlmu, nakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuepushe na akulinde dhidi ya hila, husda na watu wote wenye nla ovu dhldi yako, Chama, Serikali na Taifa kwa ujumla. Nakuahidi kuendelea kuwa mwana CCM mtilfu wakati wote.


Wako mtiifu, Chongolo Katibu Mkuu
Safi sana ameandika barua yenye Maudhui mazuri sana, hekima na ustaarabu, Mungu amzidishie hekima na busara
 
Back
Top Bottom