Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu

Mimi ni Wamrengo wa kushoto kiasili. Huyu chongolo ni mtu mwema Sana ni mtu haswa na naamini hapendi makandokando
Hakika mkuu, Chongolo ni mtu poa sana. Sema tu amekosa ile kariba ya ubabe babe na ukorofi ndiyo maana watu wanaona kama amepwaya. By the way typing error 2024 na 2025
 
Chongolo hakufaa kuwa Katibu Mkuu; kazi inayotaka mtu analytical; yeye angepewea nafasi kama vile Oganaizesheni, Nadhani Katibu mkuu mzuri kwa CCM alikuwa ni Dr Bashiru Ally, na kipindi fulani cha nyuma kulikuwa na Wilson Mkama, Philip Mangula, pamoja na Horace Kolimba. Makatibu wakuu wazuri wa CCM walikuwa hawadumu sana kwenye nafasi hizo ispokuwa Philip Mangula.

Katibu mtendaji mkuu wa Kwanza Pius Msekwea yeye alikuwa ni intellectual sana, alama zote za CCM zilizopo leo: katiba, nembo, bendera na hata wimbo wa CCM ni matunda ya uongozi wake.
 
Duh! Yaani katika makada wooteee, imegeuka kuwa Albert Chalamila. Ngoja tuzidi kunywa mtori huenda nyama tutazikuta chini!
 
Habari ndio hiyo!.

Wanabodi
Hii ni C&P from X
My Opinion
This is just too good to be true!.
Kwasababu, tangu baada ya kuteuliwa Mwenezi mpya, KM Chongolo was too cool, too calm na kumwacha Mwenezi atambe na ku trends.

Anayeidhinisha bajeti ya matumizi ya chama ni KM, hata yeye KM mwenyewe huwa hazunguki na a pool of media kubwa kama ya Mwenezi anayozunguka nayo na kum trendisha!.

Kwa vile kule nyuma Konda Boy akiwa RC wa DSM ni boss wa Chongolo akiwa DC Kinondoni, alimkaripia kwenye kadamnasi ya watu mkutanoni na kumuamuru! nyamaza wewe, kaa chini!.

Sasa Chongolo ni Boss wa Konda Boy, Mwenezi lazima aombe ruhusa kwa KM akubaliwe ndipo afanye ziara!. Inawezekana KM na yeye anaona dogo anafanya amsha amsha huku na kule bila yeye kuidhinisha hivyo amekuwa by passed na dogo, baada ya kugundua hilo, akaona ili kulinda hadhi na heshima yake, bora awaachie chama chao!.

If this is true, Nchimbi kaa mkao wa ...

Paskali
NB: Nimeipandisha hii story, thread ikafutwa fasta, ila hapa imepandishwa.
P
Baada tu ya DAB kuteuliwa ile video ikarushwa mitandaoni, binafsi nilipoiona nilihisi hili lingetokea. Na siyo kwa huyu Chogolo tu, ni wengi ndani ya CCM hawakupendezwa na uamuzi wa Mwenyekiti wao kumteua DAB kuwa Mwenezi wa chama, na wengi waliongea chini chini kupinga uteuzi huo.

Lakini nadhani na Mwenyekiti ana lipa fadhila kwa DAB kiaina. Kuna video ili pita pia ikionyesha DAB alivyo mpigia chepuo kuwa Mgombea mwenza wa hayati Magufuli, toka kwenye U-spika wa bunge la katiba hadi kuwa mgombea mwenza na hatimaye leo Mwenyekiti wa CCM taifa.

Baada ya huyu hatujui nani atafuata, ila ccm wengi hawakumfurahia DAB kurudishwa hata kidogo.
 
Nimeamini jf ni chanzo Cha habari nyingi Sana,tetesi ya makonda kulamba uenezi nilisikia hapa hapa ,nikachukulia POA Kama vile umbea umbeya,mwisho ikawa,pia Raisi magufuli kupitishwa kuwa mgombea uraisi nikianza kusikia mapema kupitia hapa hapa,,makamba kuondokewa nishati nikianza mapema kusikia Kama tetesi vile ,hatimaye ikawa,na hili la chongolo laweza kuwa
 
CCM yenye amsha amsha ni ile ya Kina bashiru Ally na polepole kuliko hii,ya chongolo imepoa mno Hadi inaboa
 
Nimeamini jf ni chanzo Cha habari nyingi Sana,tetesi ya makonda kulamba uenezi nilisikia hapa hapa ,nikachukulia POA Kama vile umbea umbeya,mwisho ikawa,pia Raisi magufuli kupitishwa kuwa mgombea uraisi nikianza kusikia mapema kupitia hapa hapa,,makamba kuondokewa nishati nikianza mapema kusikia Kama tetesi vile ,hatimaye ikawa,na hili la chongolo laweza kuwa
Ya PM tu ndio haijawahi timia!
 
Back
Top Bottom