Tarehe 15 Oktoba, 2020, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, atakutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mazungumzo hayo yatafanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu Lumumba jijini Dar es salaam kuanzia mida ya saa nne asubuhi.
Vyombo mbalimbali vya habari vinaalikwa kufuatilia na kuhabarisha Umma katika mazungumzo hayo.
Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
14 Oktoba, 2020