Uchaguzi 2020 Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ndani ya Dakika 45 leo Septemba 14

Uchaguzi 2020 Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ndani ya Dakika 45 leo Septemba 14

Katibu Mkuu wa CCM(T) Msomi Dr Bashiru Ally anatarajiwa kuwepo katika kipindi cha TV cha Dakika 45 (ITV).
Unakaribishwa kusikia
1-Mambo makubwa yaliyofanywa na CCM Kimataifa ,Kikanda,Kitaifa hadi ngazi ya Kata na vijiii kwa kipindi kifupi cha miaka mitano ya Rais Magufuli
2-Sera na Ilani mpya ya CCM
3-Ufafanuzi wa maswala mbalimbali kuhusu CCM na wanachama wake
4-Muelekeo wa Kampeni
5-Tathmini ya mapokeo ya jamii kwa wagombea wa CCM.

Dr Bashiru hataropoka bali ataeleza kwa ustadi wa kisomi ndani ya Dk 45.

Hagombei urais mbona anakwenda kumfanyia mtihani muhusika? Mwambie aje la list ya vile viwanda 100@mkoa.
 
Tumeona tayari kipindi cha Lissu ITV, hamna cha maana, Magu kwenda hapo hapo ni kumpa kiki tu Lisu, size ya Lissu ni Polepole.

Ni kweli kabisa, ila hicho kipindi kwa sasa ni kwa ajili ya wagombea wa urais. Mtoeni Magufuli ili Polepole akagombea aende kwenye hicho kipindi. Mwanafunzi mwenye akili hufanya mtihani mwenyewe, na wala hatumi mtu kumfanyia.
 
Wasanii wanaotembea na Magufuli kwenye kampeni za urais ni sawa na ubwabwa wa Mzee Rungwe. Vyote ni rushwa na kutojiamini uwezo wako wa kuvuta watu kuja kukusikiliza.
Tafuteni hela msitake kuambukiza watu umasikini
 
Katibu Mkuu wa CCM(T) Msomi Dr Bashiru Ally anatarajiwa kuwepo katika kipindi cha TV cha Dakika 45 (ITV).
Unakaribishwa kusikia
1-Mambo makubwa yaliyofanywa na CCM Kimataifa, kikanda, kitaifa hadi ngazi ya Kata na vijiini kwa kipindi kifupi cha miaka mitano ya Rais Magufuli.
2-Sera na Ilani mpya ya CCM
3-Ufafanuzi wa maswala mbalimbali kuhusu CCM na wanachama wake
4-Muelekeo wa Kampeni
5-Tathmini ya mapokeo ya jamii kwa wagombea wa CCM.

Dr Bashiru hataropoka bali ataeleza kwa ustadi wa kisomi ndani ya Dk 45.
Kwanini asije mgombea mkuu mwenyewe...
 
Comrade umeshawahi kijiuliza kazi ya kengele kanisani na adhana misikitini ni nini? Wasanii wanakuja kutoa burudani maana kazi na dawa pia ni mbinu ya kuwavuta watu waje wasikilize sera makini za chama cha mapinduzi.
Ndio hivi.View attachment 1569250
IMG_20200914_062723.jpg
View attachment 1569251
 
Ah ah walidai upinzani ungekuwa umekufa by 2020 kwa mazuti aliyoyafanya, sasa leo wanaenda kujitetea ktk tv.
Kweli magu lzm awaadabishe washauri wake kwa kumuongopea kwa kipindi chote cha miaka mi5
Kila chama na mikakati yake, wao CDM wamempeleka Lissu kwenye hicho kipindi, Magu yeye ameamua kutembea kijiji kwa kijiji, kila mtu ashinde mechi zake tusilazimishane njia za kupiga kampeni.
 
Dah ! Mgombea wa CCM Mpya John Pombe Joseph Magufuli sijawahi kumuona akifanyiwa mahojiano ya aina yoyote na chombo cha habari wala kushiriki katika mdahalo kushindanisha mipango na maono yake.

Mambo yakiharibika wanaCCMpya wanaelekeza lawama siyo kwa Mgombea wao bali kwa wataalamu na wasaidizi kama Bashiru Ally kushauri kununua wanasiasa wa upinzani, Dr. Philip Mpango sera za fedha & Uchumi, Humphrey Polepole dhana potovu kuwa upinzani utakuwa umekufa 2020, Prof. Palamagamba Kabudi kuhusu korosho n.k kwa kumshauri mgombea wao vibaya.

Ingekuwa kipindi hiki hakijarekodiwa basi tungempelekea mtangazaji Fardhia Middle kuhoji vipi ACT-Wazalendo, CHADEMA, CUF, CHAUMMA wote waliwapeleka wagombea wa urais ktk kipindi pendwa cha Dakika 45 ITV Tanzania kuelezea na kutetea toka ndani ya mioyo yao sera, mipango na maono yao lakini CCM Mpya wanamficha mgombea wao asije studio kuhojiwa ?
Tofautisha Rais wa JMT/ bingwa wa kupambana na corona duniani NA wachumia tumbo wengine
 
Kwanini azije JPM mwenyewe..?mana yeye ndiye mgombea na wagombea wenzake wote wamekuja katika hicho kipindi yeye ana excuse gani kama mgombea.?

Pili kabla hajaeleza mengi tunamtaka ajibu kwanza swali kwanini ameamua kutumia wasanii katika kampeni ilihali yeye ndiye aliye kataa utumiaji wa wasanii katika kampeni..?

#MaendeleoHayanaChama
 
Katibu Mkuu wa CCM(T) Msomi Dr Bashiru Ally anatarajiwa kuwepo katika kipindi cha TV cha Dakika 45 (ITV).
Unakaribishwa kusikia

1-Mambo makubwa yaliyofanywa na CCM Kimataifa, kikanda, kitaifa hadi ngazi ya Kata na vijiini kwa kipindi kifupi cha miaka mitano ya Rais Magufuli.

2-Sera na Ilani mpya ya CCM

3-Ufafanuzi wa maswala mbalimbali kuhusu CCM na wanachama wake

4-Muelekeo wa Kampeni

5-Tathmini ya mapokeo ya jamii kwa wagombea wa CCM.

Dr Bashiru hataropoka bali ataeleza kwa ustadi wa kisomi ndani ya Dk 45.
Dadeki Magu kautia mpira kwapani 😂😂😂😂😂
Kweli CCM wanapata shida sana mwaka huu!!! Wameona isiwe tabu asije akaenda akaharibu zaidi, wamempeleka Bashiru 😂😂😂😂
 
Na kutoa unifom za ccm kwa vitoto vya shule mkivilazimisha kujaa kt mikutano ya ccm kama ule wa kirumba mwanza ina maana gani au kwa ccm au ndo pale unapojitekenya ili ucheke?

Back
Top Bottom