Uchaguzi 2020 Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ndani ya Dakika 45 leo Septemba 14

Uchaguzi 2020 Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ndani ya Dakika 45 leo Septemba 14

Tunamtaka Magufuli kwenye 45Min. Bashiri siyo mgombea hana mvuto wala hatajibu maswali tunayotaka kujua ikiwemo makosa na mauchafu aliyofanya boss wake
Umeanza kumjua lini?
 
Hahaha Magufuli hawezi kuongea kwenye vipindi vya maswali na majibu.

Kazoea kuongea yeye tu, kufokea watu, na kutukana, pale ataongea nini?!
 
14 September 2020
Mahojiano haya yalirekodiwa mjini Dodoma katika Ofisi Kuu ya CCM Makao Makuu
[emoji837]#Dakika45 na Bashiru Ally, Katibu Mkuu CCM.

.................................................................................
Dah ! Mgombea wa CCM Mpya John Pombe Joseph Magufuli sijawahi kumuona akifanyiwa mahojiano ya aina yoyote na chombo cha habari wala kushiriki katika mdahalo kushindanisha mipango na maono yake.

Mambo yakiharibika wanaCCMpya wanaelekeza lawama siyo kwa Mgombea wao bali kwa wataalamu na wasaidizi kama Bashiru Ally kushauri kununua wanasiasa wa upinzani, Dr. Philip Mpango sera za fedha & Uchumi, Humphrey Polepole dhana potovu kuwa upinzani utakuwa umekufa 2020, Prof. Palamagamba Kabudi kuhusu korosho n.k kwa kumshauri mgombea wao vibaya.

Ingekuwa kipindi hiki hakijarekodiwa basi tungempelekea mtangazaji Fardhia Middle kuhoji vipi ACT-Wazalendo, CHADEMA, CUF, CHAUMMA wote waliwapeleka wagombea wa urais ktk kipindi pendwa cha Dakika 45 ITV Tanzania kuelezea na kutetea toka ndani ya mioyo yao sera, mipango na maono yao lakini CCM Mpya wanamficha mgombea wao asije studio kuhojiwa ?
Mchato hawezi kukubali kwenda studio au kwenye mahojiano ya live. Ukimuangalia tu, unaona kwamba ni mtu wa kupanic haraka.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom