Uchaguzi 2020 Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ndani ya Dakika 45 leo Septemba 14

Uchaguzi 2020 Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ndani ya Dakika 45 leo Septemba 14

Watanzania hawaitaki CCM hata majeshi sema viapo vinawabana
Zile kura wanazopata CCM zinapigwa na wanajeshi?

Acha kujidanganya, yaani mgombea wenu anasimama jukwaani anatoa somo la sheria kama lecturer wa Mzumbe halafu utegemee atapata kura? Oct 28 tutawaonesha tunachokitaka wananchi
 
Zile kura wanazopata CCM zinapigwa na wanajeshi?
Acha kujidanganya, yaani mgombea wenu anasimama jukwaani anatoa somo la sheria kama lecturer wa Mzumbe halafu utegemee atapata kura? Oct 28 tutawaonesha tunachokitaka wananchi
Kwahiyo huyo magufuli wenu anaekimbia hadi kipindi cha dk 45 cha ITV kuogopa maswali na kujieleza ndo atashinda????

Kakojoe ukalale kilaza wa Lumumba wewe!!
 
Katibu Mkuu wa CCM(T) Msomi Dr Bashiru Ally anatarajiwa kuwepo katika kipindi cha TV cha Dakika 45 (ITV).
Unakaribishwa kusikia...
Asisahau kutuambia kama uchumi wa viwanda umefikiwa au bado. Rais kaingiza mamluki kumsaidia mtihani
 
Dah ! Mgombea wa CCM Mpya John Pombe Joseph Magufuli sijawahi kumuona akifanyiwa mahojiano ya aina yoyote na chombo cha habari wala kushiriki katika mdahalo kushindanisha mipango na maono yake.
BASHIRU ALLY KAKURWA AKIWA GEITA 14/09/2020

Mambo yakiharibika wanaCCMpya wanaelekeza lawama siyo kwa Mgombea wao bali kwa wataalamu na wasaidizi kama Bashiru Ally kushauri kununua wanasiasa wa upinzani, Dr. Philip Mpango sera za fedha & Uchumi, Humphrey Polepole dhana potovu kuwa upinzani utakuwa umekufa 2020, Prof. Palamagamba Kabudi kuhusu korosho n.k kwa kumshauri mgombea wao vibaya.

Ingekuwa kipindi hiki hakijarekodiwa basi tungempelekea mtangazaji Fardhia Middle kuhoji vipi ACT-Wazalendo, CHADEMA, CUF, CHAUMMA wote waliwapeleka wagombea wa urais ktk kipindi pendwa cha Dakika 45 ITV Tanzania kuelezea na kutetea toka ndani ya mioyo yao sera, mipango na maono yao lakini CCM Mpya wanamficha mgombea wao asije studio kuhojiwa ?

Dakika 45 tu zinamshinda miaka mitano mingine ndio ataweza ?
 
Katibu Mkuu wa CCM(T) Msomi Dr Bashiru Ally anatarajiwa kuwepo katika kipindi cha TV cha Dakika 45 (ITV).
Unakaribishwa kusikia

1- Mambo makubwa yaliyofanywa na CCM Kimataifa, kikanda, kitaifa hadi ngazi ya Kata na vijiini kwa kipindi kifupi cha miaka mitano ya Rais Magufuli...
Kuna mitakataka mingi kutoka jalalani siku za karibuni imemwagwa na BASHIR humu jamvini watz wenye akili tuteki kava pliz
 
13 September 2020
Mbarali, Mbeya

Mapogolo waililia CCM , Maendeleo ya Watu

Hawataki kusikia chochote kama kama ndege au ma-flyover bali wanataka CCM kumtua mama ndoo, wapate muda zaidi kufanya shughuli zingine kujipatia kipato kuliko kupoteza muda kusaka maji.




Wanawake wa kata ya Mapogolo Halmashauri ya Wilaya Ya Mbarali wameongea na mbunge mteule wa viti Maalum Mkoa Wa Mbeya Mary Obadia Mbwilo na kuwasilisha baadhi ya kero amabazo zimekua zikiwatesa kwa muda mrefu.

Wakizungumza na mbunge huyo mteule wa viti maalum wanawake wameomba endapo akifamnikiwa kwenda bungeni awasaidie kuwatatulia changamoto ya maji ambayo imewatesa miaka mingi katika kata hiyo.

Aidha wanawake hao wamemuomba Bi Mary kuwasaidia wanawake hao kuwawezesha kupata mikopo ya Halmashauri kutokana na vikundi vya kata hiyo kuto pata mikopo kabisa. Akijibu hoja za wanawake hao Bi Mary amewaambia wanawake hao kosa kubwa walilolifanya wananchi wa kata ya mapogolo ni kuchagua upinzani amabao umeongoza kwa miaka kumi sasa na kula fedha ambazo zilichangwa na wananchi wa kata hiyo kwaajili ya maendeleo kipindi chama cha mapinduzi kinaondolewa madarakani.

Pia Bi Mary amewaomba wanawake wa kata hiyo kuhakikisha wana chagua Diwani, Mbunge na Rais wanaotokana na chama cha Mapinduzi ili wakafuatilie fedha ambazo wananchi walikichanga kwajili ya maji zimeenda wapi na maji hakuna kwa miaka kumi sasa upinzani wakiwa madarakani katika kata hiyo.
 
Hivi kuna watu bado wanamsikiliza huyu? Alisema namnukuu " kuanzia sasa hatutawatumia Wasanii tena kwenye shughuli za chama tutabaki na TOT tu kwenye shughuli zetu" Bashiru 2017
 
mnarubuni wajinga tuu kuaminisha kwamba malaika kutoka chatoo ANAKUBALIKA
 
Aliwahi kusema hatumia wasanaii. Leo anaongea pumba gani hizi?
Screenshot_20200915-144435.png
 
Hakuna jipya! Ni uwongo juu ya uwongo mwingine! Tangu mzee huyo aliposemaga Katiba mpya sio kipaumbele cha watanzania wakati ndio chanzo cha mkwamo mkubwa tulio nao kiuchumi, kisiasa na kijamii, ukweli huwa sina tym ya kumsikiliza mzee huyo aliyeamua kuitundika Elimu yake juu ya bendera ya kijani nayo sasa inapepea kufuata upepo!
 
Back
Top Bottom