TANZIA Katibu Mkuu wa CUF, Khalifa Suleiman amefariki dunia

TANZIA Katibu Mkuu wa CUF, Khalifa Suleiman amefariki dunia

Chibudee

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2016
Posts
1,775
Reaction score
2,404
Katibu mkuu wa CUF, Khalifa Suleiman amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar, mkurugenzi wa mafunzo wa chama hicho Thney Juma amethibitisha.

FB_IMG_1585602988346.jpeg

KHALIFA Suleiman Khalifa alikuwa Mbunge wa Gando, kisiwani Pemba ambako aliongoza jimbo hilo kuanzia mwaka 1995 hadi 2015 kupitia Chama cha Wananchi (CUF).

Machi 17 mwaka 2019, Baraza Kuu la Uongozi wa CUF lilimteua Khalifa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho akisaidiwa na naibu wake, Fakhi Suleiman Khatibu (Zanzibar) huku Magdalena Sakaya akiteuliwa naibu kwa upande wa Bara.
 
Pole familia kwa kuondokewa na mpendwa wenu na pole upinzani tanzania kwa kuondokewa na kiongozi mzito!
 
‪TANZIA: KATIBU MKUU WA CUF, KHALIFA SULEIMAN AFARIKI DUNIA‬

‪> Amefariki dunia akipatiwa matibabu katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar‬

‪> Aliwahi kuwa Mbunge wa Gando (1995-2015) na alizaliwa Agosti 9, 1956‬

IMG_20200331_000807_081.jpg
 
Back
Top Bottom