Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Aimiminia Sifa Na Pongezi Tanzania kwa Kuwa Kinara wa Amani Barani Afrika.

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Antonio Guterres Ameimiminia sifa na pongezi kubwa sana Tanzania chini ya uongozi shupavu, imara na madhubuti wa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa kuwa Kinara wa Amani Barani Afrika.

Ametoa sifa na pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo Ofisini na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kasimu Majaliwa alipokutana naye Nchni Marekani .ambako yupo huko kwa ajili ya kumuwakilisha Mama yetu Mpendwa katika mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa. lenye kauli mbiu ya kutokumuacha yeyote yule nyuma. Kushirikiana Pamoja kuendeleza Amani , maendeleo endelevu na heshima ya binadamu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Katibu Mkuu huyo Ameipongeza sana Tanzania kwa kupokea kwa miaka mingi wakimbizi kutoka Nchini Burundi na kuwahifadhi ,mpaka sasa ambapo nchi hiyo imetulia ,kuwa na amani na utulivu. Ameipongeza Tanzania kuendelea kutoa na kupeleka wanajeshi wake kulinda amani katika nchi mbalimbali ndani ya jumuia ya Afrika mashariki pamoja na SADC ,pamoja na kusaidia sana katika ukombozi wa nchi mbalimbali za Afrika kujipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni..

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kasimu Majaliwa amemueleza juu ya kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa mwishoni mwa mwaka huu pamoja na uchaguzi Mkuu hapo mwakani.

Waziri Mkuu hapo kesho atashiriki katika mkutano huo na kutoa salamu za serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Nahodha wetu makini na shujaa wetu Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,ambaye anaendelea kuchanja Mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania kutokana na uchapakazi wake uliotukuka na wenye kugusa mioyo ya watu

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 

Mmmh!
Kinara wa amani barani Afrika?
 
Acha unafiki
Nafikiri bado hajapewa taarifa kamili kuhusu hali ya Demokrasia, Amani na Usalama kuhusiana na nchi hii ya Tanzania. Akipata Ripoti ya namna hiyo naamini atabadili ghafla huo msimamo wake alionao hivi Sasa.
 
Amewahi kuishi au hata kuisikia Ununio?
 
🙄 🙄🙄🙄🙄🙄🙄
 
Na tutailinda kwa gharama yoyote ile, tukiongozwa na Rais, kipenz cha waTanzania wote Dr.Samia Suluhu Hassan 🌹
 
Reactions: Tui
Wivu tu ndio unawasumbua Ninyi Ma CHADEMA
Ukweli mchungu huwa una kawaida ya kuchoma Sana rohoni,

Aidha, Nafikiri huyo Karibu Mkuu wa UN bado hajapewa taarifa kamili kuhusu hali ya Demokrasia, Amani na Usalama kuhusiana na nchi hii ya Tanzania. Akipata Ripoti ya namna hiyo naamini atabadili ghafla huo msimamo wake alionao hivi Sasa.
 
JAMBO CCM TV!
Kuna Amani gani wakati tunaona Polisi na Magari,Farasi na Mbwa jijini Dar wakipita pita kwa hofu ya CDM?
 
Vipi hajabubujikwa na machozi ya furaha?
 

Msione vyaelea, vimeundwa. Amani imefanyiwa kazi. Kama tunaipenda nchi yetu na kuitakia mema, lazima tuendelee kuifanyia kazi.
Tujenge jamii yenye kuheshimiana, kusikilizana na kukubali kutokukubaliana. Na kikubwa kabsa, lazima tujue uongozi ni dhamana.
Tuna wajibika kuhakikisha tunatumia vema naafasi za kiuongozi na kiutendaji kwa kuwajibika. Kuiba, au kutumia vibaya mali na vyeo ambavyo tunakasimiwa ni makosa makubwa sana na yanatishia umoja na ustawi wa Taifa lolote lenye kunia mema.
 
Huyu mama anaua na müteşâbihtir raia leo hii wewe Zuzu unamuona kipenzi cha wananchi?
Kwa ulinzi aliojiwekea ni dhahiri kuwa anajua kuwa watu hawampendi!!
atalindwa kwa ulinzi mkali daima na ataendelea kutuongoza katika kulinda umoja,amani na utulivu wa waTanzania kwa gharama yoyote, upende, usipende gentleman 🐒

Maoni ya waTanzania wengi sana, wangependelea aongoze nchi walau hadi 2035. Na kama taifa tunaangalia uwezekano huo 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…