Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani aandika barua ya Kujiuzulu. Lugola na Andengenye wakalia kuti kavu, Rais Magufuli asema hawafai

Lugola pamoja na kumsifia Rais leo kafukuzwa hadharani.Ningekuwa Lugola ningeaga nakwenda kuko joa na nasepa mbele kwa mbele.
Nimeiangalia sura yako apo juu nikawaza unasema kuwa unaenda kukojoa nikakiwaza kikojoleo chako, eeeh am kweli wakubwa wanafaidi, yetu macho, asante bi dada, pia pole yake Lugola aje uraiani tuchape kilauli
 
Mzee wa Masuti yenye Mabendera bendera, acha aisome namba.
Mzee wa 10% ana historia nzuri ya rushwa ,
CCM ni ile ile.
Saizi polisi lazima wamlipizie kisasi watakmpiga cheti cha makosa matatu 90 kama tunavyopigwa sisi
 
Huu uzi haueleweki, nafikiri Mods wameungaunga sana nyuzi za watu bila kufanya uhariri wa kutosha. Hata title haiendani na contents humu.

Anyways, suppose Lugola sio waziri tena, vipi? Yale mashati yake yenye bendera ataendelea kuyavaa? Political pundits kazi kwenu.

Halafu kufanya matumizi ya fedha za umma bila bunge kupitisha ni tatizo? Mbona tunaambiwa hata manunuzi ya ndege kwa cash na mengineyo kama yale manunuzi ya wabunge wa upinzani hayakupitishwa na bunge.
Watanzania tuache unafiki. Hakuna lolote hapa la kusifiwa.
 
Miaka miwili ijayo utashangaa wamepewa shavu pande nyingine...
 
Nina wasiwasi kama Lugola atarudi bungeni tena, nafasi kwa yule mropokaji imepatikana wakati muafaka kabisa, kwenye siasa kila kitu kina base na timing, mwaka wa uchaguzi huu, kwa heri Lugola.
 
Mkurugenzi wa NIDA kabaki Lugola out. Juzi Lugola akiwa Lindi alimuita mkurugenzi kana kwamba ni mwizi😀😀😀😀
 
Miaka miwili ijayo utashangaa wamepewa shavu pande nyingine...
Nina wasiwasi kwa kauli ya bashiru ally kuwa hata ukishinda kura za maoni wataweza kukumwaga hawa CCM watamtosa hata ktk ubunge kwani hii ni dosari tayari
 
KANGI LUGOLA- NINAKWENDA KUWATUMIKIA WANANCHI WA MWIBARA: Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemshukuru Rais John Magufuli kwa kumwamini na kumteua kushika wadhifa huo na kuongeza kuwa amepokea kwa mikono miwili uamuzi wa Rais wa kukaa kando katika nafasi hiyo na sasa atapeleka nguvu zake katika kuwatumikia wananchi wake wa Jimbo la Mwibara.

Lugola amesema hayo baada ya Rais Magufuli kuzungumzia kusikitishwa kwake na utendaji wa Wizara hiyo ya Mambo ya Ndani iliyoingia mkataba tata unaokadiriwa kuwa wa shilingi zaidi ya Trilioni Moja chini ya uongozi wake kama waziri.

Rais Magufuli aliweka wazi sakata hilo wakati wa uzinduzi wa nyumba za Magereza zilizopo Ukonga Jijini Dar es Salaam.

#UzinduzinyumbazaMagereza #AzamTVUpdates #AzamTVApp #AzamTV #AzamTWO
 
figganigga,
Mawaziri waliobaki hili ni funzo kuwa Uwaziri ni cheo cha kawaida ni muda wowote tu unaondoka. Nani alijua kama Kangi leo yanamtokea hayo? Ataficha wapi sura yake kwa watumishi aliokuwa akiwanyanyasa na kuwadhalilisha kisa tu yeye ni waziri?. Mawaziri mliobaki acheni kuwa na roho za kuwanyasasa walio chini yenu maana hujui siku wala saa Mhe. Rais atafikiria nini juu yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…