Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani aandika barua ya Kujiuzulu. Lugola na Andengenye wakalia kuti kavu, Rais Magufuli asema hawafai

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani aandika barua ya Kujiuzulu. Lugola na Andengenye wakalia kuti kavu, Rais Magufuli asema hawafai

Ila mzee baba yeye ananunua ndege bila kupitishwa na bunge
Rais Magufuli amethibitisha kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amejiuzulu nafasi yake.

“Kangi Lugola nakupenda sana na hapa umenisifia kwelikweli nakushukuru lakini kwenye hili hapana, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani nampenda sana lakini kwenye hili la kwenda Nje ya Nchi unasaini fedha ambazo hazijapitishwa hata na Bunge hapana”

"Ninajua Waziri wa Mambo ya Ndani hayupo hapa ameshaandika barua ya kujiuzulu na mimi nimeshamkubalia"

Pia Dkt.John Pombe Magufuli amemuondoa kwenye nafasi yake Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzania, Thobias Andengenye kutokana kwenda ulaya kusaini mdaradi ambao haujapitishwa na bunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mungu ni mwema ambavyo simpendi Kangi Lugola hii ni habari njema sana
 
RAIS WA JMT JOHN POMBE MAGUFULI AMETENGUA UTEUZI WA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MH KANGI ALPHAXARD LUGOLA, KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO MH KINGU PAMOJA NA MAAFISA KADHAAA WA WIZARA HIYO KWA KILE KINACHOSEMEKANA NI KUINGIA MKATABA WA KUKOPA KIASI CHA SHI TRILION 1.3 NJE YA NCHI ILI KUJENGA MAJENGO YA MAGEREZA KINYUME NA TARATIBU AMBAPO NI WIZARA YA FEDHA PEKEE NDIYO YENYE MAMLAKA YA KUKOPA PESA NJE YA NCHI KWA KUPITIA VIKAO MAALUMU VYA BUNGE.
Aisee umeandika vitu ambavyo sio vya kweli kwenye hayo maandishi. Hakuna mahali Mhe. Rais amesema pesa ambayo imekopwa itaenda kujenga majengo ya Magereza.

Kwanza kabisa uelewe, ishu ya fedha zilizokopwa ilikuwa ni kwa ajili ya Idara za Zima Moto na Uokoaji na sio Jeshi la Magereza.

Hivyo jitahidi kuwa makini unavyosambaza habari.
 
Hatimaye kupiga Vita makanisa ya walokole kumepata jibu .Nilimuonya Lugora humu bado Mjema
 
Ogopa watu waongeaji sana mkuu,huyo jamaa ni mpiga blah blah tu. Wizara ya nje na mambo ya ndani zinahitaji akili nyingi,na diplomacy nyingi mkuu ila kubalance mambo kwa stake holders wote.
 
Hii inaweza kuwa indicator mbaya kwake kwenye uteuzi wa chama chake kwenye uchaguzi ujao hii kashfa inaweza kuwa sababu ya kuonekana hafai kupitishwa na chama kuwa mgombeaji wake kwenye jimbo lake

Ni vyema akajiandaa kisaikolojia na kuangalia kazi nyingine ya kufanya kwa malipo atakayopata
Kazi Gani atafanya, atakula Hela zake alizovuna mpk zitaisha

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lugola hakuwa muadilifu hata kabla ya kuwa waziri wa mambo ya ndani alikua na tuhuma nyingi ikiwemo ile ya rushwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui kwanini Mh hatilii maanani background ya mtu kabla ya kumteua. Katika wenyeviti wapya wa bodi mbali mbali walioteuliwa juzi kuna mmoja alikuwa na tuhuma kama 280 hivi ila kateuliwa. Sasa sijui washauri wa mkuu wanampamba mtu au vipi
 
Kuna mwingine alikua na mashitaka 160 ya matumizi mabaya ya Fedha/utakatishaji cha ajabu juzi ameteuliwa kua Chairman of the Board(Veta) na Dpp amesema hana nia ya kuendelea na kesi yake.
Lugola hakuwa muadilifu hata kabla ya kuwa waziri wa mambo ya ndani alikua na tuhuma nyingi ikiwemo ile ya rushwa

Sent using Jamii Forums mobile app

dodge
 
Ni vyema tukajiuliza pia kwa nini walifanya hayo waliyofanya, Binafsi nafikiri ilikuwa na kufana upigaji hivyo ni vyema wakaburuzwa mahakama kwa makosa ya uhujumu uchumi, kutumia madaraka vijana, uharibu wa mali za umma, kosa la mauaji ( kuwaibia wanyonge ni kuwatia njaa na hatimaye kuwaua).
 
Back
Top Bottom