TANZIA Katibu Tawala Arusha, Bw. Richard Kwitega afariki Dunia

TANZIA Katibu Tawala Arusha, Bw. Richard Kwitega afariki Dunia

Chanzo cha ajali mwendokasi dereva hana lawama kwa kumsikiliza boss wake.
 
Kiukweli sisi madereva wa serikali tuna kiburi barabarani. Mimi nina pikipiki yenye namba za DFPA kweli barabarani huwa nataman fuso zinipishe
 
Salaam Wakuu,

Habari Mbaya ni kwamba Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw.Richard Kwitega amefariki Dunia kutokana na ajali.


Richard Kwitega kafariki alasiri ya leo kwa ajali ya gari katika kituo cha afya cha Magugu. Alikuwa anaenda Dodoma Kikazi, alipofika maeneo ya Mdori Manyara gari lake iligongana na Basi la Makala uso kwa uso, basi lilikuwa linalotoka Babati.

Baada ya ajali akakimbizwa kituo cha afya cha Magugu ili baadaye apelekwe Babati kwa matibabu zaidi.

Ilipofika saa tisa na dakika 50 akafariki Dunia. Mipango inafanyika ya kuurudisha mwili Arusha.

Apumzike kwa amani.
Ajali za namna hii mara nyingi ni uzembe wa dereva katika kuyapita magari ya mbele (overtake). Nimewahi shuhudia aina hizi za gari ziki-overtake kwenye mpando, kona, au mkanda wa malori bila kuhofu kitakachojiri mbele na ghafla unakutana na semi au basi nalo limeiva, hapo ndipo unapokumbuka sheria za barabarani hazikuwekwa na wendawazimu japo inakuwa too late for you.
 
Kila siku huwa nasema madereva wa mahari ya serikali hawana akili. Wanadhani mtu aliyegundua kuwa gari ili ipishwe inahitaji kutoa taarifa ya suti(siren) na taa pia(vimulimuli) wao wakishafunga vimulimuli kwa dicksound wanajiona wana haki ya kupishwa wananyoosha mguu tu

Sasa ukute sehem pazuri naweza kuitoa kidogo yangu. Kama pabaya tunakutanisha vyuma tu halafu tunaomba Mungu
Hahahaha unakutanisha chuma kwa chuma 😁😁😁 mwendo mchubuyu
 
Nikiwa kama mhanga wa ajali zinazosababishwa na magari ya serikali.

mwaka 2012 pale junction ya kwenda ITV, niko navuka kwenye zebra, STK 232 nyeupe ikanigonga, ikiwa inatokea mwenge. Nyuma yake kulikua na gari 3 zimekaa foleni kusubiri nivuke, yeye akatanua akaja kunivaa paaaap!

Bahati yangu Mungu aliniokoa maana jamaa alikuja kufunga break karibu kabisa na kichwa changu.

Nikainuka kurudi upande nlipokua. Dereva yule alisepa fasta hakusimama wala kuonesha kujali.

Wito: Maereva wazembe wawajibishwe kwasababu hakuna aliye juu ya sheria.
Pole mkuu.
Sijawahi na sitawahi kuja mantiki ya magari ya serikakali kutofuata sheria za barabarani.
Trafiki wanawaangalia tu. Kila mtu atavuna alichopanda.
 
Back
Top Bottom