Chuo Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Kigamboni Dar es salaam)
Wanafunzi na Mitandao ya Kijamii
Kongamano Maalum la Wanafunzi na Mitandao ya Kijamii- limefanyika Chuo Cha mwalimu Nyerere Dar es Salaam ambapo Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa, Cde Victoria Mwanziva alikua mgeni rasmi na kuzungumza na Wanafunzi kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa manufaa yao na manufaa ya Taifa letu kwa ujumla
Katika hotuba yake kwa vijana wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere- kwenye Kongamano maalumu la " Wanafunzi na Mitandao ya Kijamii" cde Victoria Mwanziva amezungumzia masuala kadhaa muhimu na yenye manufaa Kwa Wanafunzi hao
Masuala muhimu aliyozungmza kwenye kongamano hilo ni pamoja na mafunzo juu ya Fursa ya Masomo, fursa za mafunzo za ndani na nje ya nchi kupitia matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii
Lakini pia comrade Mwanziva amesisitiza Matumizi ya mitandao katika kuyasema mema ya Taifa letu kiujumla, bila kusahau kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Tanzania na Watanzania wote.
"Ni jukumu letu kama Vijana na Wasomi kuitumia mitandao ya kijamii kuinua Taifa letu Kwa kutoa ushirikiaono wa kutosha kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na kazi zake zote vilevile kufuatilia kazi zote zinazofanywa na Chama pamoja na Serikali". Alisema Victoria Mwanziva.
Aidha Victoria Mwanziva amesisitiza umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii kwa wanafunzi kama njia sahihi ya kujifunza na kupata taarifa muhimu kwa ajili ya maendeleo yao kitaaluma.
"Serikali yetu inayoongozwa na Mhe Rais " Samia Suluhu Hassan inafanya uwekezaji mkubwa kwenye TEHAMA hivyo matumizi ya internet yatakua juu sasa ni jukumu lenu kuitumia fursa hii kwenda kidigitali kujijenga na kukua kwenye uwanja wa TEHAMA"
Mwisho cde. Victoria Mwanziva amewapongeza wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuandaa kongamono hili Muhimu lenye malengo maalumu ya kuwaelimisha wanafunzi juu ya matumizi mitandao ya kijamii.
@uvccm_tz @victoria.mwanziva @kenanikihongosi