Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima aliyekuwepo Ikulu wakati mikataba hiyo ikisainiwa alisema maaskofu wanasubiri kuona maandishi ya kilichomo ndani.
βMaaskofu wanahitaji kuusoma, kusikia tu hakutoshi. Walikuwepo watatu kushuhudia tukio na walipoitwa hawakuambiwa kuna nini, lakini walichosikia wameona angalau kuna kusikilizwa kwa maoni ya wananchi na maaskofu walikuwa wanawasemea kwa sababu rasilimali za wananchi zilikuwa hatarini,β alisema.
Chanzo: Mwananchi