Katibu wa TEC: Maaskofu wanahitaji kuisoma mikataba iliyosainiwa, walipoitwa hawakuambiwa kulikuwa na nini

Katibu wa TEC: Maaskofu wanahitaji kuisoma mikataba iliyosainiwa, walipoitwa hawakuambiwa kulikuwa na nini

Hivi kumbe bado kuna usiri kwenye hii mikataba?"Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa."Marko 4:22,Neno la Yesu Kristo
 
samia Hilo suala la hili limkataba la bandari ilikuwa afe kipa afe beki ilikuwa harudi nyuma na ndio mana kafanya aliyoamua kuyafanya ili DP uanze kazi bandarini.

Kuna ajenda ya siri sana inafichwa juu ya suala hili waTanganyika tuombe sana

Imagine mwarabu wa DP kabla hata hajaanza kazi bandarini keshafika Njombe kuangalia ardhi ili awekeze huko sasa unajiuliza wamekuja kwa ajili ya bandari au na mambo mengine?
Acha uoga wewe jiamini muhimu mikataba izingatie maslahi ya taifa.
 
Sasa mkuu mimi naamini ile nadharia ya kuwa mali zote pamoja na rasilimali za Nchi zinatoka kwa Mungu na yeye pekee ndiye mwenye nguvu na mamlaka ya kulinda hizo mali.

Ikitokea Mungu kaona serikali ya samia haitendi haki kwenye uangalizi wa mali zake Mungu ataleta serikali nyingine kwaajili ya kuzilinda mali zake zote. Kwa sasa relax na ujifunze kutofautisha viongozi ili akija mwingine mwenye misimamo msimpinge.

Kazi ya kanisa ni kulingania kondoo wa bwana na sio kuwa mtetezi wa mali.
...Sasa Mungu anakuwaje na Mali bila Kuzilinda ???....
 
Imagine halafu kumbe wanajenga misikiti huko Njombe na Mbeya

Hili suala waTanganyika tusipofungua jicho la tatu kuna madhara makubwa sana yanaenda kutokea huko mbele ya safari
Sasa kuna ubaya gani kujenga misikiti njombe na na mbeya mbona juzi Rais samia kawapa wakatoliki pale babati milioni 100 wamalizie kanisa lao pale?
 
Imagine watu wameitikia wito kwa utii tu kwa mamlaka bila kujua kuna shughuli ya nini hasa …halafu wanafika pale waimba mashairi wanaanza kuimba ,” …hata waliopinga mkataba Leo wako hapa kwa sababu wanakubaliana nao “ …haikuwa lazima…watafanya siku nyingine wakiwaita wasiende au watume uwakilishi wa kawaida sana …mfano kanisa katoliki kuweza kutuma maaskofu watatu wakasindikizwa na katiibu mkuu wa TEC ni heshima sana …..shughuli nyingi tu kubwa huwa wanatuma Padre wa parokia ya eneo husika panapofanyika jambo kuwakilisha
Kwa maana halisi, hawa TEC wamedharauliwa na serikali kama wanayoyasema ni ya kweli. Lakini sina sababu ya kutilia mashaka aliyoeleza Kitima. Samia anajulikana ni kiongozi wa hadaa na udanganyifu mwingi. Hii ndiyo tabia yake.
 
Kwanini tusiletewe kwanza? Ivyo vya kukimbizwa bungeni yatakuwa kama yale waliopitisha hewa na sasa wanarudia.
 
Lile joho alilopewa Mheshimiwa Protase kule Tabora niliofia sana, nilijua kuna kitu kigumu kinafuata. Mwenye ile picha naiomba

I wish asilivae, likae tu huko Vatican.
Unajua misimamo ya TEC wewe! Tulia utaona mziki wao. Ila kusema kweli tunataka kuona huo mkataba sio maneno.
 
Nadhani ulimuona pale namna alivyokuwa hana amani moyoni.
EEEeeeenHeeeeee!
Ni kama mtu aliyetekwa?
Sasa unaona ujambazi huu mnaolifanyia taifa letu?

Huyo padre chini ya Magufuli angletwa hapo huku bastola ikigusa mbavu zake, na hali yake ingekuwa hivyo hivyo, kama hiyo uliyomwona nayo chini ya Samia.
Hakuna tofauti yoyote zaidi ya njia tu zinazotumika.
 
Lile joho alilopewa Mheshimiwa Protase kule Tabora niliofia sana, nilijua kuna kitu kigumu kinafuata. Mwenye ile picha naiomba

I wish asilivae, likae tu huko Vatican.
Sidhani kama atalivaa.

Huwezi joho hata hujui limetokea wapi.

Ulivaa madhabahuni
 
Body language ya Charles Kitima +Masimango ya Chawa Mpoto vinaonesha Mapadri hawakujua wanaitiwa kitu gani, uleule utii wa kijinga kupokea wito bila kuuliza wito niwa nini mwishowe wamepakawa matope hadharani. Ukimuangalia Mpoto na maneno yake utagundua ulikuwa ni Mtego wa Kimkakati kabisa.
 
Wanaotusababishia hasara kwa kutuingiza kwenye mikataba hiyo mibovu wako ndani ya uwezo wetu.

Natamani siku moja tupate wanajeshi wazalendo waongoze nchi na kuwashughulikia kisawasawa hawa hayawani, maana hata wakitoka kwa njia ya kura hakuna hakika kama watakaoingia watakuwa tofauti.
That will never happen.

SERVICE people are YES PEOPLE.

Too brave to kupasua tofali but FEARING of nasty Politicians.

Never will happen.
 
samia Hilo suala la hili limkataba la bandari ilikuwa afe kipa afe beki ilikuwa harudi nyuma na ndio mana kafanya aliyoamua kuyafanya ili DP uanze kazi bandarini.

Kuna ajenda ya siri sana inafichwa juu ya suala hili waTanganyika tuombe sana

Imagine mwarabu wa DP kabla hata hajaanza kazi bandarini keshafika Njombe kuangalia ardhi ili awekeze huko sasa unajiuliza wamekuja kwa ajili ya bandari au na mambo mengine?
Hii nchi jamani watu wanafikiri Kwa kutumia nini ????
Hivi karne ya 21 bado mtu una mashaka na mgeni kwenda kuangalia fursa Njombe ?
Hivi unafahamu Kenya Kuna Mkulima mmoja tu analima Parachichi kushinda wakulima wote wa Njombe ?
Kuna Mkenya anataka kujua huyo Mkulima anatokea wapi ?
Hivi unajua nchi kama Dubai, Saudi Arabia, Dubai, au Oman Kuna nyumba zinauzwa RAIA WA NCHI yoyote akinunua na akitaka uraia wa nchi hiyo anapewa within 24 hours ?
Hivi hii hangover ya hulka za ujamaa itaindoka lini katika mabongo yetu
Na watu wenye akili kama hizi bado wengi kwenye mfumo wetu

Akili kama hizi ni kama Pingu zisizoonekana ni kikwazo kikubwa sana
View attachment 2791608
 
Mbona ume panic jiwe limekupiga. Aseme tu mimi ni mwanaharakati wa Chadema sio kujificha sijui katibu wa maskofu. Mbona Gwajina kasema tu mimi CCM na mchungaji hakuna shida. Kama mwanamme kweli aseme yeye ni nani sio kujificha kwenye kivuli cha udini huo ni uwoga. Kwanza sasa hivi hana thamani yoyote kaalikwa kapigwa mawe na kina Mrisho sura akaishusha na mpiga picha kaambiwa peleka kule camera. Unacheza na CCM weweee
Wewe ni nani wakufanya mtu aseme utakayo. Poor argument.
 
Samia ameamua kukaza fuvu sizani kama atakuwa na mwisho kuzarau viongozi wa dini
 
Mbona ume panic jiwe limekupiga. Aseme tu mimi ni mwanaharakati wa Chadema sio kujificha sijui katibu wa maskofu. Mbona Gwajina kasema tu mimi CCM na mchungaji hakuna shida. Kama mwanamme kweli aseme yeye ni nani sio kujificha kwenye kivuli cha udini huo ni uwoga. Kwanza sasa hivi hana thamani yoyote kaalikwa kapigwa mawe na kina Mrisho sura akaishusha na mpiga picha kaambiwa peleka kule camera. Unacheza na CCM weweee
Duh!
Akili nyingine ni za kipekee sana. Kwa hiyo Samia kiongozi anayedanganya bila aibu ndiye thamani yake imekuwa juu kwa ulaghai anaofanya?
Naona unajiandikia tu maneno bila ya kuwa na tafakuri nyuma ya hayo unayoyaandika.
 
It's like a page from Mario Puzzo Novel (Actually this is Stranger than Fiction)....; Gives a Whole new Meaning to Banana Republic...
As a nation, we're up to an interesting episode. Can't wait to see what follows next!
 
Back
Top Bottom