Katibu Wizara ya Nishati Felchesmi Mramba: Umeme unaokuja kutoka Ethiopia utakuwa na hasara lakini hiyo hasara haituhusu

Tunataka umeme kutoka bwawa la Nyerere mliotuaminisha utakuwa ni mwingi wa kutosheleza hadi kuuza nje ya nchi. Acheni mambo ya kutudanganya kama watoto wadogo. Hivi hamuoni hata aibu,nchi imekopa matrillion ya fedha Kwa ajili ya mradi huo,halafu leo mnatueleza ujinga gani!!
 
Matapeliiii
 
Kwahiyo Ethiopia wanatuuzia umeme kwa hasara?

Hivi kweli kuna nchi ambayo ipo tayari kufanya biashara kichaa?
 
Kama anakiri sisi tunazalisha umeme kwa gharama ya juu kuliko majirani zetu, ina maana majirani tunaowauzia wapo tayari kununua umeme wetu kwa gharama ya juu kuliko gharama ya umeme wao?

Au sisi tutalazimika kuwauzia umeme majirani kwa bei chee inayoendana na bei yao bila kujali tutapata hasara?
 
Ccm ni πŸ‘‰πŸ’©πŸ’©πŸ’©πŸ’©
 
Watanzania huwa sio watu wa kuhoji hoji na wanaridhika haraka sana baada ya kupigwa sound.

Jana nilikuwa naangalia you tube ya akinadada wa Kikenya wakiwa Mwanza walikuwa wamepanda Basi la Nyehunge lile Basi likawa na hitilafu nje kidogo ya mji wa Mwanza.

Badala ya wahusika wa Basi kusema ukweli kwamba gari limeharibika wakawa wanajizungusha kwenye migahawa na sintofahamu ikaendelea mpaka wale wadada wa Kenya kwenda kulalamika na kutishia kuita Polisi ndipo Basi lingine kuletwa.

Halafu wale Wadada wakawa wanawashangaa Watanzania kwa kuvumilia USANII wakawa wanasema kama imgelikuwa ni Kenya wakenya wasingevumilia hata nusu saa.
 
Nchi hii kazi ipo kwakweli
 
Kwa wale wenye kumbukumbu kama Mimi, Tegeta Escrow na ndugu mitambo na Symbion walianzaga hivi hivi kwamba Umeme hautoshi plus bla bla kadhaa

Kumbe wajanja walikuwa wanatafuta hela za Kampeni

Hii Nchi haina Viongozi wenye uchungu calibre ya Nyerere

Wote ni mafisadi tu, ndiyo maana haipigi hatua

Na bahati mbaya, Wananchi pia tumelala Usingizi wa Pono πŸ™Œ
 
Kipindi Cha magufuli huyu alinyooshwa Kwa utendajikazi wake mdogo lakini Kwa kuwa Sasa hivi tuna rais legelege na asiye na maono ndiyo kayarudisha madarakani watendaji wa hovyo kama Hawa.
 
Mkuu nchi yetu imekuwa ya hovyo sana. Wanasiasa wamejipa nafasi kubwa kuliko Wataalam. Badala ya Wataalam kuwashauri Wanasiasa, imekuwa ni kinyume chake.

Mtaalam atakaesimamia Taaluma yake, basi ni adui kwa Wanasiasa. Huondolewa mara moja kwenye taasisi. Jambo hili limewpelekea wengi wao kuwa CHAWA.

Nilikuwa simkubali Magufuli kwenye maamuzi yake mengi (fuatilieni comments zangu) lkn kwenye hili nimemkumbuka Mwamba. Huu ni upuuzi na dharau ya hali ya juu kwetu raia.
 
Kwahiyo tunaweza kuwa madalali
 
Walau huyu Katibu Mkuu Mramba namwelewa.

Nilitaka kuanzisha mada nzito hasa kuwa Raisi awavurumishe wataalamu wa Tanesco waende Ethiopia wakajifunze kuwa wao kwa nini kilomita zote hizo toka Ethiopia umeme haupotei njiani na kuwapa loss ila wetu kilomita nyingi unapotea na kuipa Tanesco mabilioni ya hasara

Argument ya katibu mkuu ina make sense naikubali Ruksa kanunueni kwa muono wangu huo umeme wa Ethiopia

Katibu mkuu Mramba nimekuelewa
 
Hakuna swali la msingi hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…