Katika biashara mbaya zaidi duniani ni ya madawa ya kulevya. Haitaki utani kabisa

Katika biashara mbaya zaidi duniani ni ya madawa ya kulevya. Haitaki utani kabisa

Wao wana viwanda vingi bidhaa zingine Wachina wanakuambia subiri unakaa hotel kumbe mzigo unatoka Vietnam..
Viatu vizuri vingi ni Vietnam na Caterpillar boot mimi nilikua natoka China naenda kupakia vitu vingine Vietnam na napakia Mawigi na saa Cambodia hapo...
Nauli huko sio kama unatoka Afrika ni ndogo sana.
Aisee lugha inatufelisha sana
 
Dawa za kulevya kwa Tanzania sasa hivi sio biashara. Kwanza ma informer ni wengi kuliko unavyofikiria. Aretas Lyimo amehakikisha katika kila wafanyabiashara watatu au wanne wa dawa za kulevya mmoja awe mnunuzi au muuzaji ni snich na utadakwa tu

Tena wengine wana jifanya wanunuzi wakubwa na anaweza kununua mzigo kiasi ili ujae kisha uishe(udakwe)

Miongoni mwa kesi ngumu kabisa Tanzania kwa sasa ni hizo za kusafirisha dawa za kulevya kuanzia mirungi, bangi, heroin, coceine na nyingine nyingi. Mtu anapokamatwa kwanza atachezea kichapo na mateso mengine yasiyosemeka

Kesi zake hazina dhamana na inaweza kuchukua miaka hadi saba kesi ndio ianze kusikilizwa na mara nyingi Jamhuri inashinda kwasababu kama vile kuna mkakati kwa vyombo vya dola kupambana na biashara hii. DCEA(Kitengo cha kupambana na dawa za kulevya), Mahakama Kuu na hata Mahakama ya Rufaa utadhani zinalengo moja kuhakikisha zinawafunga maisha wahusika

Tena afadhali kidoogo mirungi au bangi mtu anaweza angalau akatokea kwenye rufaa kuliko cocaine au heroine. Hawakuachi. Wengi wamefungwa kifungo cha maisha gerezani na kabda ya hapo hupitia mateso makali wakiwa mikononi mwa maafisa ya DCEA kabda ya kupelekwa mahakamani . Mateso hayo pamoja na vipigo vikali lakini pia wanafanyiwa udhalilishaji wa kingono.

Uzuri ni kwamba hao jamaa hawaonei watu kusema kwamba mtu alikua hajihusishi kwa namna yoyoye na hizo issue waje wamkamate! Hapana. Wote wanaokamatwa wanakua wamechunguzwa vizuuri kabisa na kwa muda wa kutosha

Inatokea saa zingine wakati wa interrogation wakatajiwa majina ya wahusika wengine. Hapo huchunguzwa then wanaweka mtego na wanawadaka kama ilivyokua kwa yule aliyekua kocha wa magolikipa wa Simba anaitwa Mwarami.

Yeye hakua anajulikana maana walikua wanamtafuta Cambiaso. Sasa kwenye interrogation ndio akatajwa. Kimykimya wakamuwekea mtego wakamnasa. Kesi yao mwaka wa tano sasa huu wapo mahabusu Keko hata robo haijafika na sasa inatakiwa ianze tena upyaa kabisa

Majina yote makubwa ya wafanyabiashara hiyo wameshafungwa vifungo virefu au kifungo cha maisha. Chonji wa Magomeni na wenzake wamefungwa maisha, yule Yanga Omar wa Tanga kafia gerezani akitumikia kifungo cha miaka 30, kuna jamaa anaitwa Horohoro kapigwa maisha, Abdul Nsembo na mkewe Shamim Mwasha(nao hawa enzi zao walikua kama jamaa wa Katoro) wanatumikia kifungo cha maisha na hata rufaa yao pia imeshindwa Mahakama ya Rufaa. Wameambiwa waendelee na kifungo cha maisha. Sasa iliyobaki waombe labda wapate msamaha wa Rais. Wapo wengi wa namna hiyo magerezani. Biashara unayoona hata Mchaga anaogopa kuifanya achana nayo na kimbia mbali kabisa.

Saivi Wanigeria ndio wanawadanganya sana dada zetu. Wanawapangia nyumba za thamani kisha pale wanafanya kama stoo ya dawa za kulevya huku wao wenyewe wakiwa hawakai hapo. Kinaponuka mwanamke ndio anashikwa na kidhibiti na Mpopo anasave. Sasa hivi mamlaka kama zimeshtuka. Wameshawawekea mkakati. Ushahidi mdoogo tu na Mpopo anachukua nyundo maisha.

Kwa ujumla Aretas Lyimo amesafisha kabisa mambo hizo na ndio maana hata mateja wamepungua sana ukilinganisha na miaka ile tisini na ya mwanzoni wa 2000 hadi 2017
Aisee bora nifungwe tu ila kuacha kilimo cha bangi kiukweli siwezi
 
Na kujiamini lugha sio tatizo mtu anaweza kujifunza taratibu watu wakishikwa mkono Singapore ni Singapore tu hata kama hiyo bidhaa anaweza kupata sehemu ingine kwa gharama ndogo.
Natamani mno nipakwepe kariakoo nijaribu machimbo mengine....Kuna brother mmoja kafanikiwa kweli yupo dar ila tunatoka sehemu moja yeye ishu zake ni matunda anayatoa south huko uliko..ila kama unavyojua sisi wamakonde kila nikimuhoji kuhusu hilo huwa hanipi ushirikiano kabisa
 
Aisee bora nifungwe tu ila kuacha kilimo cha bangi kiukweli siwezi
Mkuu Mnachihanguuu kifungo cha maisha kisikie kwa wengine tu. Ukienda kuwatembelea wale jamaa unakuta kwenye nguo yake kifuani imeandikwa tarehe ya kuingia jela hakuna tarehe ya kutokea

Lakini kabda ya hapo ndani ya siku wanazokua pale kwenye selo za DCEA mateso wanayopitia sio ya dunia hii. Ukisikia wametajana na mtandao wao unaweza kudhani kua labda ni kwa hiyari

Mwnasiasa mmoja aliwahi kuingia kwenye anga za hawa jamaa, na yeye alikua mdau wa biashara hiyo tata. Basi mateso yake hadi akakata moto katika interrogation ila watu hawajui ni kitu gani kilimtokea wakidhani ni issue za kisiasa
 
Kaka anaetisha ni Mungu peke yake kwasababu hapokei rushwa....mimi nina ndugu yangu alidakwa na bangi gunia 5 akakaa ndani miezi miwili akachomoka....juzi kati Kuna mzee kijiji jirani kadakwa na kete 220 za bangi kakaa ndani wiki moja kachomoka....na hao wote hakuna hata mmoja alieacha nikweli hizo biashara zinatisha ila zinatisha zaidi ukiwa unaangalia kwenye tv...
 
Nina hakika huyo alikamatwa na polisi na sio DCEA. Polisi mbona mnaongea biashara fresh tu?

Na pia ulipomtaja Mungu mimi nimekubaliana nawe. Lolote kukufika binadamu liwe zuri au baya basi ni kwa ruksa yake
 
Polisi wakiwekewa mpunga mezani wanakuachia
Ila wakija dcea kikazi hutoki
Na sahv mwamba anataka akukute na kidhibiti kabisa

Ova
 
Kaka anaetisha ni Mungu peke yake kwasababu hapokei rushwa....mimi nina ndugu yangu alidakwa na bangi gunia 5 akakaa ndani miezi miwili akachomoka....juzi kati Kuna mzee kijiji jirani kadakwa na kete 220 za bangi kakaa ndani wiki moja kachomoka....na hao wote hakuna hata mmoja alieacha nikweli hizo biashara zinatisha ila zinatisha zaidi ukiwa unaangalia kwenye tv...
Iko siku atanasa tu

Ova
 
Kuna jamaa mmj sema nmepotezana naye,alikuwa analeta tiles toka Vietnam
Aise zilikuwa quality ya hali juu sana

Ova
Vietnam wana bidhaa bora sana vitu vyao vingi mimi nilikua nanunua Hong Kong ndio wamejaza pale na si vya kutoka China ndio nikasanuka ngoja nifate mwenyewe huko huko nilikutana na vitu vingi sana kwa wakati ule wale jamaa wanakupa sample box hata 20 mpaka 30 uje kuangalia biashara kama umechukua mzigo wa kutosha wanaojua kuwa ni chimbo ni watu wachache sana na wengi wamefunikia majani hata wakienda huko wanatorokana unajua kashuka China kumbe yupo Cambodia anapanga kazi..
 
Back
Top Bottom