Katika biashara mbaya zaidi duniani ni ya madawa ya kulevya. Haitaki utani kabisa

Aisee lugha inatufelisha sana
 
Aisee bora nifungwe tu ila kuacha kilimo cha bangi kiukweli siwezi
 
Na kujiamini lugha sio tatizo mtu anaweza kujifunza taratibu watu wakishikwa mkono Singapore ni Singapore tu hata kama hiyo bidhaa anaweza kupata sehemu ingine kwa gharama ndogo.
Natamani mno nipakwepe kariakoo nijaribu machimbo mengine....Kuna brother mmoja kafanikiwa kweli yupo dar ila tunatoka sehemu moja yeye ishu zake ni matunda anayatoa south huko uliko..ila kama unavyojua sisi wamakonde kila nikimuhoji kuhusu hilo huwa hanipi ushirikiano kabisa
 
Aisee bora nifungwe tu ila kuacha kilimo cha bangi kiukweli siwezi
Mkuu Mnachihanguuu kifungo cha maisha kisikie kwa wengine tu. Ukienda kuwatembelea wale jamaa unakuta kwenye nguo yake kifuani imeandikwa tarehe ya kuingia jela hakuna tarehe ya kutokea

Lakini kabda ya hapo ndani ya siku wanazokua pale kwenye selo za DCEA mateso wanayopitia sio ya dunia hii. Ukisikia wametajana na mtandao wao unaweza kudhani kua labda ni kwa hiyari

Mwnasiasa mmoja aliwahi kuingia kwenye anga za hawa jamaa, na yeye alikua mdau wa biashara hiyo tata. Basi mateso yake hadi akakata moto katika interrogation ila watu hawajui ni kitu gani kilimtokea wakidhani ni issue za kisiasa
 
Kaka anaetisha ni Mungu peke yake kwasababu hapokei rushwa....mimi nina ndugu yangu alidakwa na bangi gunia 5 akakaa ndani miezi miwili akachomoka....juzi kati Kuna mzee kijiji jirani kadakwa na kete 220 za bangi kakaa ndani wiki moja kachomoka....na hao wote hakuna hata mmoja alieacha nikweli hizo biashara zinatisha ila zinatisha zaidi ukiwa unaangalia kwenye tv...
 
Nina hakika huyo alikamatwa na polisi na sio DCEA. Polisi mbona mnaongea biashara fresh tu?

Na pia ulipomtaja Mungu mimi nimekubaliana nawe. Lolote kukufika binadamu liwe zuri au baya basi ni kwa ruksa yake
 
Nina hakika huyo alikamatwa na polisi na sio DCEA. Polisi mbona mnaongea biashara fresh tu?

Na pia ulipomtaja Mungu mimi nimekubaliana nawe. Lolote kukufika binadamu liwe zuri au baya basi ni kwa ruksa yake
Polisi wakiwekewa mpunga mezani wanakuachia
Ila wakija dcea kikazi hutoki
Na sahv mwamba anataka akukute na kidhibiti kabisa

Ova
 
Iko siku atanasa tu

Ova
 
Kuna jamaa mmj sema nmepotezana naye,alikuwa analeta tiles toka Vietnam
Aise zilikuwa quality ya hali juu sana

Ova
Vietnam wana bidhaa bora sana vitu vyao vingi mimi nilikua nanunua Hong Kong ndio wamejaza pale na si vya kutoka China ndio nikasanuka ngoja nifate mwenyewe huko huko nilikutana na vitu vingi sana kwa wakati ule wale jamaa wanakupa sample box hata 20 mpaka 30 uje kuangalia biashara kama umechukua mzigo wa kutosha wanaojua kuwa ni chimbo ni watu wachache sana na wengi wamefunikia majani hata wakienda huko wanatorokana unajua kashuka China kumbe yupo Cambodia anapanga kazi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…