Katika dunia ya sasa, mheshimu sana yule anayefunga safari kuja kukutembelea "physically"

Katika dunia ya sasa, mheshimu sana yule anayefunga safari kuja kukutembelea "physically"

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
17,306
Reaction score
19,885
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wa humu JamiiForums.

Katika dunia ya sasa ambayo watu huweza kujuliana hali kwa njia ya simu/mitandao, muheshimu sana yule anayefunga safari kuja kukutembelea "physically"

Kuna mwalimu wangu mmoja alikuwa anaitwa Adonijah yeye alikuwa anatufundhisha somo la communications skills mwaka 2007 aliwahi kutuambia jambo la maana sana.

Mzee yule alitufundisha kwamba, muheshimu sana mtu anayeamua kukuandalia zawadi kwa mikono yake mwenyewe kuliko yule anayediriki kutoa pesa na kununua kisha akuletee.

Yaaani just imagine siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwako (Birtday) imefika na rafiki zako wanawiwa kukuandalia kitu cha kukupongeza nacho na mara nyingi huwa ni card pamoja na cake.

Kulingana na maelezo ya mwalimu wangu yule ni kwamba, siku zote mthamini sana rafiki ambaye atakuwa tayari kuchukua karatasi kisha akaandika salama za kukutakia heri ya siku yako ya kuzaliwa.

Mthamini sana mtu huyo kuliko yule anayetoa pesa yake mfukoni (let's say 5,000/=) kisha ananunua kadi na kukuletea au kumpa mtu alete. Aliyetayari kuandaa kadi kwa mikono yako anaweza kuwa anakuthamini zaidi kuliko yule aliyeinunua "ready-made" dukani.

Katika dunia hii ya sasa ya science na technology ambayo pesa/maisha yamekuwa magumu sana ni jambo la kawaida kukuta mtu na dada yake tumbo moja hawajaonana "physically" miezi 6 alafu wote wanakaa hapahapa Dar.

Unakuta mtu anafanya kazi katika taasisi binafsi (Bank) kuanzia jumatatu mpaka ijumaa, na kwa baadhi ya taasisi mfanyakazi anaenda mpaka siku ya jumamosi nusu siku, yaaani wanaingia saa mbili kisha wanatoka saa saba mchana.

Baba/ Mama anaondoka nyumbani saa 11 alfariji kuelekea kazini watoto wakiwa bado hawajaamka na kurejea usiku saa 4 watoto wakiwa tayari wamelala.

Jumapili ndio siku pekee ambayo mtu anapata muda wa kufanya shughuli ndogo ndogo za hapa na pale akiwa nyumbani kwake ikiwa ni pamoja na kwenda kanisani, kukagua madaftari ya watoto, siku hiyo hiyo afanye usafi, apumzike na mambo mengine mengi.

Ukiona mtu amefunga safari kuja kwako wewe ndugu, jamaa au rafiki ujue kuna mgonjwa, msiba au sherehe baaas, mbali na hapo fahamu kuwa huyo mtu amekuthamini na kukupenda sana. Mpe muda wako.

Give him your time, mpikie vizuri, piga naye story kwa maana huyo anakupenda. Kwanini ameamua kuja kwako? Kama suala ni kukusalimu tu si angeweza kukupigia simu kukujulia hali? Au unadhani yeye hana mambo ya kufanya mpaka akutafute physically? Ni kwa sababu anakupenda na kukuthamini.

Kwa bahati nzuri mimi ni moja kati ya watu waliobahatika kukaa na watanzania kutoka katika makabila mbalimbali. Mimi nimekaa sana na watu wanaitwa wazaramo. Hawa wazaramo mpaka sasa ndio kabila pekee ambalo bado ninaona wanao huu utamaduni wa kukutana ana kwa ana na wapendwa wao.

Kwa kusema hivi simaanishi kuwa makabila mengine hawana upendo wa namna hii, la hasha, bali ni kutokana na ukweli kwamba hawa ndugu zangu wazaramo wengi wao wapo katika ajira binafsi (wamejiajiri) kwa maana mtu wa namna hii anakuwa na namna ya kujipangia mambo yake kuliko yule aliyeajiriwa.

KUMBUKA: Mthamini sana mtu (ndugu/rafiki) anayetumia muda wake mwingi kukutana na wewe wakati angeweza kukujulia hali kwa njia ya simu tu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Ni ukweli mtupu, Mimi hapa nina ndugu wengi hatujaonana kitambo. Wengi pia humu watakuwa wamelengwa na uzi huu. Hata hivyo kautamaduni haka ka kisasa sio nzuri.
 
Hebu tuunganishe na hii hapa chini.

Wakati dunia ikiwa ndogo kulingana na teknolojia, kuna jambo linasahaulika katika jamii lipo hivi.

Mpo busy kama mtoa mada ulivyoandika hapo juu ila, wakati mnakuwa na utengano kutokana na ubize, kumbuka wewe na mkeo mna watoto wa jinsia zote mbili wanaokuwa.

Pia ndugu zako wanafamilia pia, wakati huohuo vijana kama wapo shule basi ni boarding ambako mnakutana kila baada ya miezi kadhaa.

Kwa kufupisha ubize unakuja kufanya hamuonani vijana wetu hawaonani, siku inakuja kutokea baba mdogo/mkubwa unakuja kutongoza mwanao au sababu kila mtu yupo bize, watoto ndugu huko huko shule wanatongozana kisa maisha magumu.

NB. Kuonana na kukutanisha ndg kuna umuhimu sana.
 
Kazi ya kutembelea watu makwao halafu kwangu hawaji siwezi mimi
Kama familia ili kuepuka hii kutupiana mpira na kuonana kama umeenda kuomba msaada kwa ndugu yako anzisheni utaratibu wa kukutana wote kila mwisho wa mwezi kwa mmoja wa wanafamilia. Mf, mwisho wa Jan mnaenda kwa yule,Feb kwa yule Mar wanakuja kwako na kuendelea unakuwa ni utaratibu wa miaka yote.

Hii ukoo wetu tunaifanya inasaidia sana unakuta mwenye uwezo anaenda kwa aliye hohehahe na aliye hohehahe anaenda kwa mwenye uwezo shida mkiwa hamna umoja mimi maskini nikienda kwa tajiri anaanza kueleza shida zake as if nimeenda kuomba msaada kumbe sivyo.
 
Mkuu uko sahii....Ila Kuna vitu lazima tuangalie pia kwa Yule unae mtembelea.kuna Yule ndugu mwenye Mali ukimtembelea anaona Kama umefata kitu.kuna Yule ndugu maisha duni ukimtembelea anaona mtihani maana hata hela ya kuku accommodate kwa lunch kwake Ni mtihani.pia maisha yame badilika tusikariri
 
Kuepuka kutongozeana wake na ku admire minyama nyama ya wake za watu. Kila mtu akae kwake. Tukutane neutral place Kama pub.
Mimi namaliza hata miaka mitatu sijaingia nyumba ya mtu. Misibani naishia kwenye hema, kwenye harusi tuonane kanisani au holini.
Sitaki umbea jumbani yangu na hata waif anajua. Akimualika rafiki yake namtizama huyo mgeni mwanzo mwisho mpaka atoke. Siku nyingine hamkaribishi.
 
Wengine sie hatuwezi kutembelea watu, aaaah tunawasiliana kwa simu imeisha hiyooooooh.
Mthamini sana mtu (ndugu/rafiki) anayetumia muda wake mwingi kwa ajili yako wakati angeweza kukujulia hali kwa njia ya simu tu.
 
Back
Top Bottom