Katika Dunia yenye takribani watu Bilioni 8 leo, zaidi ya watu Bilioni 110 wamewahi kuishi na kufa

Katika Dunia yenye takribani watu Bilioni 8 leo, zaidi ya watu Bilioni 110 wamewahi kuishi na kufa

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Hii itukumbushe kuwa hii Dunia tunapita, na itusaidie kupunguza kama sio kuacha kabisa kiburi na kujipa umuhimu.

Waliowahi kuishi na kuondoka ni wengi zaidi ya waliopo leo, na kila mmoja kwa wakati wake alikuwa na umuhimu wake.

Hivyo nafasi ya wewe kuishi leo isikufanye ufikiri kuwa ni ya kipekee sana, utaondoka siku moja na watakuja wengine. Maisha yataendelea vizuri tu bila uwepo wako.

Hii nimekumbushwa na huyu kijana wangu mkubwa, nami nikaona niwakumbushe.

Ncha Kali.
 
Kujipa umuhimu?

Sometimes kila kitu ni tafsiri.

Mwingine anaweza sema msijiweke nyuma tokeni mbele mlete mawazo yenu nyinyi nyote ni muhimu msijidharau...

Halafu unatokea wewe tena. Usijipe umuhimu, usijione wa kipekee Sana...mtakufa Tu kama wengine.

Mradi kila mtu na mtazamo wake
 
Hii itukumbushe kuwa hii Dunia tunapita, na itusaidie kupunguza kama sio kuacha kabisa kiburi na kujipa umuhimu...

charlesdegaulle1.jpg
 
Kujipa umuhimu?
Sometimes kila kitu ni tafsiri...
Mwingine anaweza sema msijiweke nyuma ..tokeni mbele mlete mawazo yenu...nyinyi nyote ni muhimu..msijidharau....
Ukiambiwa 'ninyi nyote ni muhimu' maana yake umeitwa, umepewa hiyo hadhi hujajipa.... wala kinyume chake sio kujidharau.
 
Back
Top Bottom