Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hujaona ile video inayotrend insta?Kivip
inasemekana mtu mwenye makandokando mengi ndo anapataga shida na kuona vitu vya ajabu wakati wa kufaNimeuguza mtu mpaka kanifia mikononi.
Alikuwa anatapatapa huku anasema anaogopa sana, anasema eti kuna watu wako kwa mbali anawaona wanamsubiri.
Ujumbe kuntu kabisa.Hii itukumbushe kuwa hii Dunia tunapita, na itusaidie kupunguza kama sio kuacha kabisa kiburi na kujipa umuhimu.
Waliowahi kuishi na kuondoka ni wengi zaidi ya waliopo leo, na kila mmoja kwa wakati wake alikuwa na umuhimu wake.
Hivyo nafasi ya wewe kuishi leo isikufanye ufikiri kuwa ni ya kipekee sana, utaondoka siku moja na watakuja wengine. Maisha yataendelea vizuri tu bila uwepo wako.
Hii nimekumbushwa na huyu kijana wangu mkubwa, nami nikaona niwakumbushe.
Ncha Kali.
Hujaona ile video inayotrend insta?Huyo alikuwa anawaona Malaika wakimlaki, hakupaswa kuogopa.
Clip za insta ni vichekesho tu au maudhui kwa lengo fulani, katika hali halisi huwezi kupata camera.Hujaona ile video inayotrend insta?
Mtu aliyehai anapigana na kufukuza kiumbe kisichoonekana ila mwisho wa siku roho inanyofolewa kimaajabu!
Kuogopa lazima.
Huyo alikuwa na hallucinations.Nimeuguza mtu mpaka kanifia mikononi.
Alikuwa anatapatapa huku anasema anaogopa sana, anasema eti kuna watu wako kwa mbali anawaona wanamsubiri.
Simple kwa nn ufukuzane viumbe vya ajabu wakati bodaboda ni chapu haraka 2 upo kwa GodHujaona ile video inayotrend insta?
Mtu aliyehai anapigana na kufukuza kiumbe kisichoonekana ila mwisho wa siku roho inanyofolewa kimaajabu!
Huwa najiuliza nitakufaje😕😕😕
Inatia sana huzuni.inasemekana mtu mwenye makandokando mengi ndo anapataga shida na kuona vitu vya ajabu wakati wa kufa
ila wale mambo machache wanakufa kimyakimya , tena wengine wanaaga
bibi yangu alimwambia mzee wangu amgeuze, baada ya kumgeza kakimya kakapita, kumsemesha alishakata moto
Ni video halisi.Clip za insta ni vichekesho tu au maudhui kwa lengo fulani, katika hali halisi huwezi kupata camera.
Huenda kila mtu na taswira ya kifo chake kinavyomjiaHuyo alikuwa na hallucinations.
Mbona hata ndotoni unaona watu.
Sodoma na gomora,mafuriko wakati wa Nuhuhilo halina shaka,
tunapita tena kwa kasi
ila hiyo Bn110 sijui umeitoa wapi mkuu
Inasemekana huenda wanapigana na zirail mtoa roho.Simple kwa nn ufukuzane viumbe vya ajabu wakati bodaboda ni chapu haraka 2 upo kwa God
Umeweza kuacha pombe mpwa?Inatia sana huzuni.
Umenikumbusha kisa cha marehemu bibi yangu aliyefariki 2015.
Alifariki Jumatatu saa 2 asubuhi.
Jana yake Jumapili nilikesha Coco beach, piga sana pombe.
Inafika asubuhi saa 1, napigiwa simu bibi ananiita.
Kufika pale, kila mtu ananiambia bibi yako yuko hoi, anakuita.
Nafika chumbani na pombe pombe zangu bibi akaniambia nimpakate, nikampakata.
Akasema unanuka pombe na kwanini jana hujaenda kanisani.
Aliniambia maneno 3 tu.
Moja, acha pombe,
Pili, usiache kwenda kanisani na jambo la 3 ni siri yangu.
Baada ya pale akanipa funguo kisha akaniambia nakukabidhi huu funguo, tafuta mlango unaoingia funguo hii.
Baada ya pale nikaita watu huku nimempakata.
Akatabasamu, akafumba macho mwenyewe kisha akakata roho.
Aloooo.....sitasahau.
Bibi yangu alikuwa kipenzi changu sana sana sana.
Kwani ni lini ulishawahi kuwaza namna hiyo kwamba wewe ni 'so special' katika hii dunia?Hii itukumbushe kuwa hii Dunia tunapita, na itusaidie kupunguza kama sio kuacha kabisa kiburi na kujipa umuhimu.
Waliowahi kuishi na kuondoka ni wengi zaidi ya waliopo leo, na kila mmoja kwa wakati wake alikuwa na umuhimu wake.
Hivyo nafasi ya wewe kuishi leo isikufanye ufikiri kuwa ni ya kipekee sana, utaondoka siku moja na watakuja wengine. Maisha yataendelea vizuri tu bila uwepo wako.
Hii nimekumbushwa na huyu kijana wangu mkubwa, nami nikaona niwakumbushe.
Ncha Kali.