Katika hili mimi nasimama na Mbowe, hakika jamaa kakomaa kisiasa na anaijua vizuri siasa

Katika hili mimi nasimama na Mbowe, hakika jamaa kakomaa kisiasa na anaijua vizuri siasa

..Lissu hapingi maridhiano.

..Lissu anatetea maridhiano yenye tija.

..Hoja za Lissu ndizo zitakazompa nguvu Mbowe anapojadiliana na CCM.
Sasa kwanini hakukaa na viongozi wenzake wakajadiliana kuhusu mambo hayo, badala ya kuanza kuzunguka nchi nzima kuyananga maridhiano hayo.

Inamaana huwa hawasiliani na Mbowe na kuongea juu ya maswala hayo hadi aje ayaongelea yeye mwenyewe tu kwenye public?
 
Kwani Mbowe mwenyewe anasemaje?
Mbowe kakomaa kiakili na kisiasa. Sio mtu wa kukurupuka na kuanza kujibiza na watu aina ya kina Lisu mikutanoni.
Anachofanya Lisu ni sawa sawa na kelele za mpangaji kwa mwenye nyumba tu.
 
Lisu anatakiwa akae na viongozi wenzake wa chama awambie kile kinachohitajika kufanywa katika maridhiano hayo, badala ya kuanza kuzunguka nchi nzima kupinga wazi wazi kile kinachofanywa na chama katika maridhiano yao.
Majukwaani ndio pazuri ili na Wananchi wasikie HATUTAKI SERIKALI YA NUSU MKATE.

TUNATAKA KATIBA MPYA HALAFU TUINGIE KWENYE UCHAGUZI.
 
Sasa kwanini hakukaa na viongozi wenzake wakajadiliana kuhusu mambo hayo, badala ya kuanza kuzunguka nchi nzima kuyananga maridhiano hayo.

Inamaana huwa hawasiliani na Mbowe na kuongea juu ya maswala hayo hadi aje ayaongelea yeye mwenyewe tu kwenye public?

..uwezekano mkubwa Mbowe na Lissu wameongea.

..Na Mbowe sio Mwenyekiti anayeamini ktk kuwanyamazisha au kuwashikia akili viongozi wenzake au wanachama.

..All in all, maridhiano sio mabaya, tatizo yanakwenda kwa kasi ya konokono.
 
Tuna imani na Lisu na sio hayo maridhiano ya kitapeli ya Mbowe.
Mbowe anafanya siasa kisayansi zaidi. Tofauti na Lisu ambae anachukulia siasa kiharakati matokeo yake atakosa vyote.
 
..Nadhani kinachoendelea ni over-reaction ya ziara alizoanza Tundu Lissu.

..Lissu angejikalia nyumbani kwake usingesikia makelele haya dhidi yake.

..Majuzi tu kulianzishwa mada hapa ikihoji alipo Tundu Lissu kwa namna ya kumbeza.

..Leo Lissu yuko barabarani yameibuka makundi ya kila aina kumshambulia.
Akifanya ziara zake kwa kuelezea sera za chama chake, akielezea namna atakavyoleta ahueni ya maisha pindi atakapochaguliwa, hapo hakuna atakaetofautiana nae.

Ila kuanza kulaumu maridhiano ambayo bado yapo kwenye hatua ya kufanyiwa kazi ni sawa sawa na kuturudisha kulekule kwenye siasa za chuki ambazo huwafaidisha wao wanasiasa na kutuacha sisi wananchi wa kawaida tukichukiana wenyewe kwa wenyewe.
 
Lisu anatakiwa akae na viongozi wenzake wa chama awambie kile kinachohitajika kufanywa katika maridhiano hayo, badala ya kuanza kuzunguka nchi nzima kupinga wazi wazi kile kinachofanywa na chama katika maridhiano yao.

Hakuna haja ya kuendekeza maridhiano ya kupotezeana muda. Lisu anaweka msisitizo kuwa hayo maridhiano yana walakini, hilo sio jambo la kufichaficha. Na kwa taarifa yako tunamuelewa Lisu zaidi kuliko hao viongozi wa chama chake.
 
Lissu yupo kwa vile Mbowe yupo and not the other way round
Tatizo Lisu anafikiri kwamba sikio linaweza kuzidi kichwa, kumbe anajidanganya.
Ajifunze kupitia kwa Dr Slaa na Zito Kabwe.
 
Hakuna haja ya kuendekeza maridhiano ya kupotezeana muda. Lisu anaweka msisitizo kuwa hayo maridhiano yana walakini, hilo sio jambo la kufichaficha. Na kwa taarifa yako tunamuelewa Lisu zaidi kuliko hao viongozi wa chama chake.
Sipingani na wewe katika hili, lkn kwanini Lisu hakutumia njia nyingine za kichama kuelezea madai yake, na badala yake kaamua kuyazungumzia zungumzia hovyo kwenye public?

Je wakitokea wanachama wengine na kuanza kupingana na maamuzi ya chama hadharani kama anavyofanya yeye hali uko mbele itakuaje?
 
Umejuaje kuwa hayo maridhiano ni makubaliano ya chama? Hakuna anayewazuia hao wanachama wengine wakijitokeza kutetea wanachoamini, sisi wafuasi wengine tutasimama na anayesimamia tunachotaka sio porojo za maridhiano yasiyo na mpango.
 
Akifanya ziara zake kwa kuelezea sera za chama chake, akielezea namna atakavyoleta ahueni ya maisha pindi atakapochaguliwa, hapo hakuna atakaetofautiana nae.

Ila kuanza kulaumu maridhiano ambayo bado yapo kwenye hatua ya kufanyiwa kazi ni sawa sawa na kuturudisha kulekule kwenye siasa za chuki ambazo huwafaidisha wao wanasiasa na kutuacha sisi wananchi wa kawaida tukichukiana wenyewe kwa wenyewe.

..anatoa elimu ya uraia kuhusu umuhimu wa katiba mpya na bora.
 
Hakuna sayansi kwenye siasa, kwenye siasa ni kufanya lile wanataka wafuasi wako. Hiyo kusema siasa ni sayansi ni maneno ya kitapeli ya CCM.
Raisi wa sasa ni mtu anaependa siasa za maelewano, kwahiyo nina imani kila lililopangwa katika maridhiano yao litafanyika, japo kila moja litafanywa kwa muda wake.

Inashangaza hata mwaka haujaisha watu washaanza kulalamika na wakati zaidi ya miaka 7 huko nyuma watu hao walikuwa kimyaa.
 
Sasa kwanini hakukaa na viongozi wenzake wakajadiliana kuhusu mambo hayo, badala ya kuanza kuzunguka nchi nzima kuyananga maridhiano hayo.

Inamaana huwa hawasiliani na Mbowe na kuongea juu ya maswala hayo hadi aje ayaongelea yeye mwenyewe tu kwenye public?
Anayozungumza Lissu yana baraka zote za chama.
 
Slaa na Zito ajifunze nini kupitia kwao?
Walijiona kwamba wao wako juu ya chama kwa kuongea, na kufanya maamuzi kinyume na yale yalioamuliwa na chama.

Walijua kwamba hata wakifukuzwa wataondoka na umati wao na kukiacha chama kitupu. Lkn sasa kilichotokea ilikuwa ni tofauti na matarajio yao maana mwisho wa siku wakajikuta wanaondoka wao tu, wale waliowashika masikio mitandaoni wakabaki katika chama chao.
 
Back
Top Bottom