Lisu huwa anapenda aonekane kuwa yeye ndio mwenye mawazo chanya chamani, na kwamba viongozi wengine wote hawana uwezo au ujanja wa kuona yale anayoyaona yeye.
Swala la katiba mpya na mengineyo yapo katika mchakato. Na tayari tumeshasikia kwamba raisi kaagiza viongozi wanaohusika na swala hilo la katiba waanza kufanyia kazi yale yanayohitajika. Hiyo ni hatua nzuri ambayo kwa muda wa miaka zaidi ya 7 hatukuishuhudia, wala kufikiria kuishuhudia.
Sasa sijui Lisu anataka raisi afanyaje?
Lakini pia kuna taratibu za kichama ambazo mtu unatakiwa kuzifuata ili kuufikisha ujumbe wako na kufanyiwa kazi na viongozi husika. Sasa yeye hizo taratibu hakupenda kuzifuata na badala yake kaanza kuandaa mikutano ili apate namna ya kuongelea mabaya ya viongozi wenzake kwamba wamefanya maamuzi ya kijinga na kwamba yeye ndio mjanja asiekubaliana na maamuzi yale.
Mwisho wa siku Mbowe, Mnyika au Lema uvumilivu utawashinda na wao waanze kumjibu majukwaani au mitandaoni. Chama kigawanyike kuhusu maridhiano hayo na maridhiano yafe na nchi irudi kule kule kwenye siasa za uhasama, mikutano ifungiwe tena na nchi irudi katika mfumo uliyokuwepo miaka iliyopita.