Katika hili mimi nasimama na Mbowe, hakika jamaa kakomaa kisiasa na anaijua vizuri siasa

Katika hili mimi nasimama na Mbowe, hakika jamaa kakomaa kisiasa na anaijua vizuri siasa

Habari zenu wana JF wenzangu,

Kwanza kabla ya kuendelea na mada hii ningependa watu wengi wafahamu kwamba mimi nimeandika mada hii kwa utashi wangu mwenyewe. Sikushawishiwa, sikulazimishwa wala kushikiwa akili na mwanasiasa yoyote iwe wa upinzani, wa CCM au wa kujitegemea. Bali nimeandika hili kutokana na mapenzi ya kweli niliyonayo kwa nchi yangu ya asili ya Tanzania.

Ndugu wana JF wenzangu, mimi nimekuwa mfuatiliaji mkubwa wa siasa zetu za Tanzania toka enzi za uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi, hadi leo hii ninavyoandika mada hii, naweza kusema kwamba nina ujuzi na ufahamu wa kutosha kuhusu siasa zetu za Tanzania. Miaka yote hiyo nakiri kwamba niliwahi kuwa mwanachama wa vyama vikubwa tofauti.

Kwanza mimi na familia yetu mpaka bibi zetu na babu zetu tulianza kuwa upande wa NCCR - Mageuzi chini ya aliekuwa mwanasiasa machachari na hodari wa enzi hizo hayati Augustino L. Mrema. Baadae miaka ya 2000, binafsi nikaamua kuhamia chama cha Wananchi CUF baada ya kuona vyama vingine vya upinzani kama vile NCCR Mageuzi na TLP vinaendeleza migogoro mbali mbali. Kwa upande wa familia yetu wengine walihamia TLP, na wengine wakabaki NCCR Mageuzi.

Mwaka 2009 nikajiunga rasmi Chadema, japo sikuwa mwanachama, lakini nikawa shabiki na kuhakikisha natembeza elimu ya kutosha kwa vijana wenzangu ili na wao wajiunge na chama hicho au hata kama hawakujiunga kwa njia ya uanachama, basi wahakikishe wawe wanakipigia kura chama hicho katika chaguzi mbali mbali.

Kwa vile mimi binafsi niliamini kuwa chama hicho kina viongozi wa kweli na wenye malengo ya kweli ya kutuletea ukombozi haswa baada ya kuisomwa na kuelewa ile list ya mafisadi wa taifa letu kule mwembe yanga.

Pilika pilika za kukiombea kura Chadema nilikuwa nazifanya nikiwa tayari naishi nje ya nchi, kwa kuwahamasisha watanzania wenzangu waendelee kukiamini na kukitegemea Chadema katika maisha yao.

Mwaka 2015, niliamua kuachana na Chadema baada ya mwenyekiti wetu na genge lake kuharibu hali ya hewa chamani, na kupelekea matumaini yetu ya kukichinjia baharini chama tawala kuyayuka kama chumvi ndani ya maji. Kibaya au kizuri zaidi CCM wao wakasimamisha mtu ambae ilikuwa ngumu kwa mtu anaejielewa wakati ule kumnyima kura. Jamaa alipata kura kwa wana CCM na wasiokuwa wana CCM, kwa wanasiasa na wasiokuwa wana siasa. Huku kwa upande wa upinzani wakitumia muda mwingi kupangua kashfa za ufisadi walizomuanzishia wao wenyewe mgombea wao.

Hii ni sawa na mwanaume uwambie wazazi wako kwamba unataka kumpa talaka mkeo baada ya kumkuta na mwanaume ndani ya chumba chako wakigegedana. Afu baadae uje uwambie kwamba umeahirisha kumpa talaka baada ya kugundua kwamba mkeo na huyo kijana hawakuwa wakigegedana bali walikuwa wakitafuta panya chumbani kwako. Imagine kwa utetezi huo wazazi watakuelewaje??

Zile zilikuwa ni siasa uchwara ambazo wengi hatupendi zirudie.

Anyway pamoja na pilika pilika zilizotokea miaka 7 iliyopita kati ya CCM na Wapinzani. Sasa chama hicho tawala kimeamua kukaachini na wapinzani ili kumaliza tofauti zao zilizokuwepo huko nyuma, kwa kuanzisha maridhiano ambayo yatapunguza kelele kwa pande zote mbili. Yani upinzani na serikali ambayo ndio CCM yenyewe. Katika hili watu wengi tuliwasifu wapinzani na watawala kwa kukaa chini na kupanga namna ya kuitengeneza upya Tanzania yenye amani, upendo na mshikamano kupitia vyama vya siasa na asasi mbali mbali.

Tuliwapongeza pia wenyeviti wa vyama hivyo ambao ndio waliouwezesha mchakato huo wa maridhiano kama vile mwenyekiti wa CCM mh raisi Samia S. Hassani, mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe, mwenyekiti wa CUF mh Lipumba, kiongozi wa ACT Wazalendo mh Zito Kabwe, mzee wa ubwabwa nk.

Naweza kusema kwamba viongozi hao japo wana akili zao, madaraka yao na maamuzi yao, lkn inaonesha kuwa hawafanyi haya kwa mawazo yao, bali kwa kufuata miongozo thabiti ya vyama vyao.

Sasa anapokuja mtu kutoka ughaibuni ghafla na kuanza kupinga hadharani kile kinachofanywa na kiongozi wake au chama chake, huyo anakuwa ni mtovu wa nidhamu kwa chama chake na viongozi wake. Kwa sababu kama mtu haupendi au haukubaliani na kile kinachofanywa na chama chako au kiongozi wako, kwanini usipeleke madai yako katika chama yakajadiliwa na kutatuliwa kichama, badala ya kuja kuliongelea katika public kwa lengo la kumchafua na kumfanya yule kiongozi anaesimamia swala hilo (mwenyekiti) aonekane hana uelewa wowote juu ya swala hilo analolisimamia?

Inamaana mwenyekiti hufanya haya bila kuwashirikisha viongozi wa chama, na kama huwa anawashirikisha ni kwanini makamu huyo asimwambie kwamba hafurahishwi na maridhiano yao, ili wakae chini wayamalize kuliko kuja kulalamikia kwenye mikutano ya hadhara. Matokeo yake mwenyekiti atachoshwa na vijembe na yeye aamue kujibu na kupelekea mtifuano ambao utaharibu mchakato mzima wa hayo maridhiano yaliopo.

Mbona hatujasikia kelele hizi kutoka katika vyama vingine? Yani ni kilekile tu ambacho watu wengi ndio wanakiangalia!

Anyway katika hili mimi nasimama na Mbowe maana watanzania wengi tushachoshwa na siasa za majitaka, kuchafuana, kuingia barabarani kupambana na vyombo vya dola afu mwisho wa siku alieshawishi watu waingie barabarani akimbilie tena ulaya akaendelee ku claim ukimbizi kupitia mgongo wa fujo alizoziratibu mwenyewe nchini kwetu.

Haya yanafanywa sana na viongozi wa nchi za fujo na za vita kama Congo au Nigeria kwa kuendelea kuwadhamini waasi wapigane ili wao waendelee kupewa ukimbizi huko ughaibuni.

Mbowe asitishwe na kelele za chura, yeye aendelee kusimamia kile anachoona kina manufaa kwa taifa na chama chake. Afu huyo mleta kelele akiona hasikilizwi basi aanze chama chake mwenyewe, mbona Zito alipoona haeleweki akaanzisha cha kwake, Lisu anangoja nini?.

Sio kwa vile anaona uchaguzi wa chama unakaribia ndo ajaribu ku take advantage kupitia swala hili ili alitumie kama fimbo katika vikao vya chama kumuangusha mwenyekiti.

Lakini vile vile huenda jamaa amepewa mission na wabeberu ili aje ayumbishe maridhiano kwa lengo la kutengeneza migogoro itakayozaa vita, na vita ikiingia yanakuwa yale ya Congo. Wao wanaingia kujichotea tu bila mtu yoyote kuwa control. Maana wabeleji sio watu wazuri, wanachokifanya Congo na wajomba zao wamarekani kila mtu anakiona.

Hapa wenye upeo unaogusa mbingu ndo wataelewa.
Mbowe iko akili....
 
Kwann umeficha identity Yako ya CCM?

Ungedeclare interest ungeeleweka vizuri zaidi.
Ni wapi mimi niliwahi kusema kuwa mimi ni mwana CCM?
Naomba ushahidi wenye fact kupitia kadi yangu ya chama au kauli yangu mwenyewe nikisema kuwa mimi ni mwana CCM.
Karibu utoe ushahidi wa hayo maombi yangu mkuu. Nakuruhusu.
 
Labda Mbowe ndie anaemtuma kupitia mlango wa nyuma ili alete amsha amsha katika maridhiano yao.
Kwahiyo unataka kumaanisha kuwa Mbowe ni muoga, hana ujasiri wa kuongea mwenyewe hadi amtumie mtu mungine?
No i don't think so!
 
Naamini hao viongozi wengine uliowataja wana hekima, hawawezi kujitia uchizi alionao Lissu waanze kumjibu, wanajua wakifanya hivyo ndio watakuwa wanazidi kukivua nguo chama chao, muhimu Lissu aachwe aropoke tu akichoka atanyamaza.

Ajabu ni pale ambapo huu ujinga anaofanya, lipo kundi linampongeza, wanamuona jasiri muongoza njia, kumbe ni muhuni muongoza njia, wanataka Chadema iondoke kwenye kufuata sheria na taratibu walizojiwekea, sasa kiwe chama cha kila mwenye mdomo na aseme popote alipo!.

Hawa wajinga ni wakuhurumia tu, mahaba yao kwa Lissu yamewafunga upeo wao kifikra hawaoni wala athari za kile Lissu anachofanya kwa sasa, kwao Lissu ni kama malaika aliyeshuka kutoka mbinguni!.
Hao hao wajinga unaosema hapa ndio wanaomdanganya mpaka anaamini kuwa yeye sasa ni sikio lililozidi kichwa, kwamba anaamini kuwa yeye sasa yuko juu zaidi ya chama na viongozi wengine wa chama.
Ila ameshindwa kujifunza kupitia kwa kina zito na Dr Slaa ambao wajinga wengine walikuwa wanawaaminisha kuwa ni maraisi wa mioyo yao. Lkn mwisho wa siku wakajikuta wameondoka peke yao na familia zao.
 
Kama hivi ndivyo kwanini Lissu anahangaika kuwalaumu wenzake chamani? anawachorea ramani waonekane kama wepesi waliokubali kutongozeka mbele ya Samia..

Kama tatizo liko CCM, apeleke shutuma zake huko kwa 100% but not otherwise.
Jamaa anatafuta kujijenga kisiasa kupitia migongo ya wenzake. Hajui kwamba bila Mbowe wala Chadema yeye hawezi kufika popote.
 
Kuna mtu amekuuliza kuhusu maridhiano ya 2010 huko Zanzibar baada ya machafuko ya uchaguzi wa 2001 huko Zanzibar. Je ni kilifanyika kwenye uchaguzi wa 2015 kukiwa na serikali ya umoja wa kitaifa na katiba ya Zanzibar? Naona hutoi majibu bali unaleta porojo tu. Lisu hana haja ya kuamini kwenye maridhiano ya watu wasioaminika.
Labda sikuliona vizuri hilo swala unalozungumzia hapa. Hebu nikumbushe lipo katika comment ya namba ngapi?
 
Labda sikuliona vizuri hilo swala unalozungumzia hapa. Hebu nikumbushe lipo katika comment ya namba ngapi?
Achana na post namba, mimi nakuuliza ni kipi kinafanya maridhiano huko Zanzibar hayajeshimiwi, lakini huku Bara yataheshimiwa? Rejea uhuni katika uchaguzi wa 2015 huko Zanzibar.
 
Hata ikitokea maridhiano yamevunjika Leo, Bado wananchi wataendelea kuiamini CDM Kwa misimamo ya Lissu, Heche na Wenje.

Siasa zetu zinachukua episode ingine.

Tusubiri.
Bora Heche na Wenje wanaonekana wamekomaa kisiasa kwa kuyamaliza mambo yao kupitia vikao halali vya chama. Tofauti na jamaa ambae mwisho wa siku sikio litaponza kichwa.
 
Achana na post namba, mimi nakuuliza ni kipi kinafanya maridhiano huko Zanzibar hayajeshimiwi, lakini huku Bara yataheshimiwa? Rejea uhuni katika uchaguzi wa 2015 huko Zanzibar.
Uhuni upi wakati maalim Seifu alikimbilia kujitangaza mshindi wa uchaguzi kinyume na katiba yao ambayo inataka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ndio atangaze mshindi wa uchaguzi?
Je inamaana maalim yeye hakujua kama alichofanya kilienda kinyume na katiba yao?

Au ndio ile ya mshika makali kutaka kushindana na mshika mpini ili atapokatika vidole aonewe huruma kuwa kaonewa?
 
Uhuni upi wakati maalim Seifu alikimbilia kujitangaza mshindi wa uchaguzi kinyume na katiba yao ambayo inataka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ndio atangaze mshindi wa uchaguzi?
Je inamaana maalim yeye hakujua kama alichofanya kilienda kinyume na katiba yao?

Au ndio ile ya mshika makali kutaka kushindana na mshika mpini ili atapokatika vidole aonewe huruma kuwa kaonewa?

Mtu akikimbikia kujitangaza unafuta uchaguzi?
 
Bora Heche na Wenje wanaonekana wamekomaa kisiasa kwa kuyamaliza mambo yao kupitia vikao halali vya chama. Tofauti na jamaa ambae mwisho wa siku sikio litaponza kichwa.
Hata Lema akiwa nje ya nchi Naye amekuwa akihoji maridhiano na kusema huo ni msimamo wake binafsi.
Hata Msigwa pia ilikuwa hivyo ktk suala la Loriondo.

CDM IPO democracy, hivyo ni kawaida.
 
Makala ndefu hizi huchosha kusoma, lakini nimekusoma vya kutosha hadi ulipoanza kujitambulisha sababu zinazokufanya umshabikie Mbowe.

Kwanza nikusifu kwa uandishi mzuri, na umejieleza vyema toka mwanzo historia yako ilivyo kuhusu maswala ya siasa.

Kwa wakati huu ngoja nisiandike mengi sana, lakini inatosha kusema yafuatayo:
1. Umejiunga na vyama tele, lakini hujaeleza hasa sababu zako za kuyumbayumba kote huko. Hii ni dalili mbaya, na wengi watakuhukumu kwa msimamo wako huu wa sasa kutokana na yumbayumba yako hiyo

2. Umemsifu Mbowe kwa uhadari wake wa uongozi hadi hapo alipoingia yule jamaa 2015. Sasa swali kwako ni hilo hilo, unajuaje wakati huu na Samia Mbowe huyo huyo hakukengeuka kama alivyokwishaonekana kuwa huko nyuma, au kwa vile tu wakati huu ni Samia na siyo Ngoyayi?
Hapana, usinielewe vibaya, sina maana mbaya kwa Samia, lakini huyo huyo ndiye Mwenyekiti wa Chama ambacho katika uhai wa maisha yako yote hukueleza kuwa uliwahi kuwa mwanachama au mpenzi wa chama hicho. Hapa unahitaji kutoa maelezo juu yake. Huu ni upungufu mkubwa kwa upande wako
3. Hivi vyama vya siasa havianzishwi kwa sababu ya kutafuta maslahi ya viongozi wao. Katika maelezo yako mengi hujaeleza kwa nini wakati huu unaona Mbowe anacheza vizuri na uongozi wake wa chama kiasi cha kustahili sifa unazommiminia.
Hakuna mtu hata mmoja anayekata maridhiano, kama kuna maridhiano juu ya jambo lolote, lakini hiyo siyo sababu ya kubadili mwelekeo wa chama katika malengo yake.

Ngoja niishie hapa kwa sasa, isije ikawa gazeti jingine.
 
Sasa anapokuja mtu kutoka ughaibuni ghafla na kuanza kupinga hadharani kile kinachofanywa na kiongozi wake au chama chake, huyo anakuwa ni mtovu wa nidhamu kwa chama chake na viongozi wake. Kwa sababu kama mtu haupendi au haukubaliani na kile kinachofanywa na chama chako au kiongozi wako, kwanini usipeleke madai yako katika chama yakajadiliwa na kutatuliwa kichama, badala ya kuja kuliongelea katika public kwa lengo la kumchafua na kumfanya yule kiongozi anaesimamia swala hilo (mwenyekiti) aonekane hana uelewa wowote juu ya swala hilo analolisimamia
Makala yako imeanzia hapa kuwa mbovu, kwa sababu ulionyesha waziwazi rangi zako zilivyo. Umeshutumu na kutoa hukumu palepale.
 
Lakini vile vile huenda jamaa amepewa mission na wabeberu ili aje ayumbishe maridhiano kwa lengo la kutengeneza migogoro itakayozaa vita, na vita ikiingia yanakuwa yale ya Congo. Wao wanaingia kujichotea tu bila mtu yoyote kuwa control. Maana wabeleji sio watu wazuri, wanachokifanya Congo na wajomba zao wamarekani kila mtu anakiona.
Aiseee!
Nilikuwa sijakusoma hadi huku chini.

Ukianzia pale ulipoanza kumsema "mtu wa ugaibuni, hadi huku mwisho; mada yako umeinyonga kabisa. 'Objectivity'
ukaitupa jalalani moja kwa moja!

Pole yako.
 
..Lissu hapingi maridhiano.

..Lissu anatetea maridhiano yenye tija.

..Hoja za Lissu ndizo zitakazompa nguvu Mbowe anapojadiliana na CCM.
Very bright reply mkuu JokaKuu !
Hapa umemjibu mleta hoja na wengine wengi hasa wanaccm maana hii ndiyo hoja yao wanayochomeka baada ya kushindwa kumuelewa Lissu ambaye hajui Kuremba maneno bali fact.
Wasilojua ni kuwa viongozi wa Chadema wanaunga mkono kauli ya Lissu na ndio maana wanaunga mkono maandamano ya BAWACHA.
 
Lisu anatakiwa akae na viongozi wenzake wa chama awambie kile kinachohitajika kufanywa katika maridhiano hayo, badala ya kuanza kuzunguka nchi nzima kupinga wazi wazi kile kinachofanywa na chama katika maridhiano yao.
Utakuwa una kichwa kigumu kuelewa kama hoja zilizojibiwa na JokaKuu na wengine hujaelewa. Au waliokupa hii assignment hawajaridhika na juhudi zako! Analofanya Lissu ni mission ya chama
 
Very bright reply mkuu JokaKuu !
Hapa umemjibu mleta hoja na wengine wengi hasa wanaccm maana hii ndiyo hoja yao wanayochomeka baada ya kushindwa kumuelewa Lissu ambaye hajui Kuremba maneno bali fact.
Wasilojua ni kuwa viongozi wa Chadema wanaunga mkono kauli ya Lissu na ndio maana wanaunga mkono maandamano ya BAWACHA.
Sijui ni sababu zipi zinazowafanya baadhi ya watu kudhani kwamba maana ya maridhiano ni kuifungia CHADEMA sandukuni.
Maridhiano hayana maana ya kuifanya CHADEMA iwe CCM.

Maridhiano hayafuti mambo yanayosimamiwa na CHADEMA kama chama

Maridhiano hayawezi kuilazimisha CHADEMA kutosemea mambo ambayo haikubaliani nayo.

Na hayo maridhiano kama lengo lake ni kufifisha juhudi za CHADEMA kuiondoa madarakani CCM, hayo ni maridhiano yasiyokuwa na maana yoyote.
 
Back
Top Bottom