Katika hili mimi nasimama na Mbowe, hakika jamaa kakomaa kisiasa na anaijua vizuri siasa

..CCM wanataka nini kwenye maridhiano?

..Why are they in maridhiano? What are they trying to achieve?

..Lingine, CCM wana maoni gani kuhusu Katiba Mpya?

..Mwenyekiti wao ameruhusu mchakato wa Katiba Mpya lakini sijasikia makada wa CCM wakiweka hoja zao mezani kuhusu Katiba Mpya.
 
Uzi mreeeefu,nikadhani Kuna point.Kumbe ni Uvccm tu.
Huna upeo wa kudadavua siasa ndugu,Bora ukae kimya bosi.

Ila wenye kuijua CCM ni hao wanasiasa na Hali kadharika Vyama vya upinzani.

Swala la Vita ya wenyewe kwa wenyewe hapa Tanzania,sahau.

Democrasia Ina upana wake,so usimsoti mtu kana kwamba unamjua Sana.
 
Ameshasahau juzi tu aliwaambia waandamane akiibiwa kura, lakini alivyogeuka nyuma hakuona mtu, Lissu mwenyewe akawaita waoga, ajabu bado analazimisha njia ile ile iliyofeli kwa wafuasi wake wale wale akitegemea outcome tofauti!.
 
Kumbe umekuwa ukiizimia Chadema na kuionea wivu,ila sio kwa kutangatanga kwenye vyama vyote hivyo🏃🏃
 
Si Mbowe tu, sema CDM nzima imeshiba viongozi wanaojitambua, Chama makini, viongozi makini, wanachama makini.
 
Huo mkutano ndio ambao pia Lissu amezungumzia habari za nusu mkate na mengine...

Hoja hapa, hayo anayozungumza ameshawaambia wenzake chamani wakagoma kumsikiliza mpaka aende kuropoka barabarani?

Au tunakubaliana Chadema hakuna taratibu zozote, kila mwenye jambo lake anaruhusiwa kusema popote atapoamua?

Hii tabia ya kila kiongozi kujiamulia kuongea anachotaka popote ikiota mizizi itasababisha wale wanaosema Chadema ni kama kambale baba ndevu..watoto ndevu.. wapate hoja, lazima ikemewe mapema.
 

..Ccm wana utaratibu wa kukabidhi akili zao kwa Mwenyekiti.

..Chadema kila mwanachama ni "kambale" na ana ruhusa ya kutoa mawazo na msimamo wake.
 
..Ccm wana utaratibu wa kukabidhi akili zao kwa Mwenyekiti.

..Chadema kila mwanachama ni "kambale" na ana ruhusa ya kutoa mawazo na msimamo wake.
Aisee..

Kumbe Chadema hakuna kufuata taratibu, ni kuropoka tu!.

Hapa lazima ujue kutofautisha kati ya kiongozi, na mwanachama wa kawaida, hawa usiwachanganye utaharibu kila kitu.

Mwanachama wa kawaida anaweza kusema au kuandika chochote, na popote, kama tufanyavyo huku JF...

Lakini kwa kiongozi, hatakiwi hata mara moja kuwa "kambale", wale wana vikao vyao chamani wakayazungumzie huko, watoke na msimamo mmoja ili kuepuka kuwachanganya wanachama wao.
 

..wewe unaona anaropoka.

..wengine wanaona anatoa mawazo yake kwa uhuru.
 
Hata Lema akiwa nje ya nchi Naye amekuwa akihoji maridhiano na kusema huo ni msimamo wake binafsi.
Hata Msigwa pia ilikuwa hivyo ktk suala la Loriondo.

CDM IPO democracy, hivyo ni kawaida.
Kuhoji sio tatizo lkn sasa jamaa ni kama vile anabeza wenzake kukubali maridhiano.
Ukifuatilia vizuri maelezo yake utaelewa.
 
1. Swali la kwanza nilieleza huko juu kwamba niliyumba yumba au kuhama hama sababu ya migogoro (ya kimasilahi) iliyokuwepo katika vyama hivyo kati ya viongozi kwa viongozi.

2. Swali la pili nakubali kwamba mwaka 2015 Mbowe pamoja na viongozi wengine akiwepo huyo huyo Lisu walikengeuka. Akaingia raisi mungine kwa upande wa CCM ambae alibadili kabisa muelekeo wa siasa za Tanzania, ikaonekana kuwa raisi amebana demokrasia na haki za vyama vya upinzani kufanya mikutano yao kwa mujibu wa sheria.

Sasa ameingia raisi mungine ambae ameamua kurudisha uelekeo wa kisiasa uliokuwepo miaka yote kwa kuruhusu mikutano ya kisiasa, uhuru wa kutoa maoni na kufanya maridhiano yatakayosaidia kupatikana suluhu ya matatizo ya kisiasa yaliokuwepo na yaliopo nchini.

Hii ni hatua nzuri ambayo inahitajika kupongezwa na watu wanaopenda amani na siasa zenye muelekeo wa kujenga taifa bila kujali ilikadi za vyama vyao. Anapokuja mtu na kuanza vijembe mikutanoni ili mwisho wa siku alete mgawanyiko ndani ya chama wa wanaosapoti maridhiano na wasiosapoti hadi kupelekeo mchakato mzima wa maridhiano kuvunjika inakuwa haileti picha nzuri.

Lisu ni makamu mwenyekiti wa chama na ni mwanasheria anaezijua sheria za chama. Sijui kwanini hakufuata sheria kwa kulipeleka swala lake au malalamiko yake katika vikao vya chama wakalifanyia kazi huko huko chamani.

3. Swali la tatu lishajibiwa hapo namba 2. Kwamba kama kuna tatizo basi Lisu alitakiwa akae na kiongozi wake au viongozi wenzake walimalize kichama.

Lisu aliwahi kumlaumu Zito kipindi kile kwamba alipoona kuna tatizo kati yake na chama, basi angeitisha kikao cha chama na kulimaliza swala lake kupitia vikao vya chama, kuliko kuchukua uamuzi wa kulimaliza swala hilo nje ya vikao vya chama kwa kwenda mahakamani nk.

Sasa cha kushangaza na yeye karudia yale yale ya kuongelea hadharani bila kufuata taratibu za kichama.
 
Aiseee!
Nilikuwa sijakusoma hadi huku chini.

Ukianzia pale ulipoanza kumsema "mtu wa ugaibuni, hadi huku mwisho; mada yako umeinyonga kabisa. 'Objectivity'
ukaitupa jalalani moja kwa moja!

Pole yako.
Dunia ina mengi hii, kama haujui inavyokwenda hauwezi kuelewa.
 
..Lissu hapingi maridhiano.

..Lissu anatetea maridhiano yenye tija.

..Hoja za Lissu ndizo zitakazompa nguvu Mbowe anapojadiliana na CCM.
Uko sahihi.

Tofauti za mawazo na fikra ni afya sio udhaifu - kwenye mfumo wa demokrasia halisi.

Budi sasa tujenge na kuukubali utamaduni huo maana una faida nyingi kuliko ule wa "zidumu fikra za....Rais au Mwenyekiti"
 
Utakuwa una kichwa kigumu kuelewa kama hoja zilizojibiwa na JokaKuu na wengine hujaelewa. Au waliokupa hii assignment hawajaridhika na juhudi zako! Analofanya Lissu ni mission ya chama
Kama mission ya chama ni hii ya kuwalaumu watu hadharani sawa.
 
CCM ndio serikali. Kwahiyo wanataka amani na mshikamano kupitia hayo maridhiano, maana kuna mda ilifikia watu wa familia moja wanagombania maiti kisa upande wa baba ni CCM na upande wa mama ni Chadema au ACT Wazalendo. Kwahiyo hali inapofikia hapo wa kulaumiwa ni serikali ambayo ipo chini ya chama cha mapinduzi (CCM)

Kuhusu mwenyekiti wao kuruhusu mchakato au makada wa chama hicho kutokuzungumzia mambo ya katiba. Huu nahisi ni utaratibu wao wa kichama. Huenda huwa wanamaliza mambo yao huko na kuwaachia viongozi wayasimamie na kuyafanyia kazi.
 
Ameshasahau juzi tu aliwaambia waandamane akiibiwa kura, lakini alivyogeuka nyuma hakuona mtu, Lissu mwenyewe akawaita waoga, ajabu bado analazimisha njia ile ile iliyofeli kwa wafuasi wake wale wale akitegemea outcome tofauti!.
Tofauti ya Mbowe na Lisu ni kwamba Mbowe anatumia akili zaidi kuliko nguvu na mdomo, Lisu anatumia nguvu na mdomo zaidi kuliko akili na maarifa.
Laiti kama Lisu ndo angekabidhiwa chama kipindi kile alichokabidhiwa Mbowe, basi leo hii naamini chama kingekuwa kimeshakufa zamani.
 
Ila wewe, kwa sababu unazozijua mwenyewe, huwezi kamwe kufikiri kwamba Rais huyo huyo unayemsifu hapa anatumia mbinu tofauti tu na yule wa mwanzo kuendeleza jitihada za kuwamaliza CHADEMA!

Hayo mazuri unayoyaona na kudhani ni fadhira anazozifanya Rais huyu, hujui kwamba ni wajibu wake?
CHADEMA kufanya mambo yake ndani ya taratibu zinazoruhusiwa na sheria wakitofautiana na hivyo vyama vingine ni makosa?
Lissu kutahadharisha juu ya mtego waliowekewa iwe ni nongwa?
Sijui haya ya "amani" yanatoka wapi?
CHADEMA iliwahi kufanya vitendo vya kuvunja amani popote bila ya sababu?
Ni nani hasa aliyekuwa akihatarisha amani ya nchi, CHADEMA au CCM?

Ni wapi Lissu alipozungumzia vurugu katika shughuli za kisiasa zinazofanywa na CHADEMA, hata bila ya uwepo wa maridhiano?
Haya maridhiano mbona ndio umekuwa mtego uliotegeshewa kuwanasa CHADEMA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…