Katika jambo kubwa ninalojivunia, ni kutambua kuwa hakunaga UCHAWI

Katika jambo kubwa ninalojivunia, ni kutambua kuwa hakunaga UCHAWI

By the way mleta uzi ukiamini Mungu yupo basi directly unaamini Mchawi yupo unless turudi pia kwenye definition ya Mungu....

Ndio maana kila siku nasema waasisi wetu walikuwa na busara sana kusema Serikali / Nchi haina Dini bali wanaanchi wake ndio kila mtu kivyake na imani yake....

Sitakushangaa sana ukimuona mtu anaamini kwamba Ngw'anamalundi alikuwa anaweza kutembea kwenye maji na kumuona mjinga lakini nikigundua kwamba unaamini kwamba kuna aliyetembea kwenye maji na kubadilisha kinywaji kimoja na mkate mmoja kuwalisha maelfu na maelfu nitakushangaa sana na kuona huenda umekuwa indoctrinated...., Kama sio Hapa kwanini Kule ?

To each his / her Own....
 
Mkuu,
Umeuliza uchawi ni nini, umetoa perception yako kuhusu uchawi na last paragraph I cannot relate. It seems, it's you against youself
Naam nimekuuliza wewe definition yako ya uchawi ni ipi ? Nikatoa yangu kwamba neno uchawi ni chochote kile kinachoangamiza /umiza wengine na mwisho nikaonyesha tukiingiza mambo ya Imani / Spirituality ambayo ni ya kufikirika tukayatungia sheria tutaumiza wengi wasio na hatia kinachoweza kufanyika ni kuhukumu matokeo au deeds ambazo mtu amefan...

Kama mtu kachanganya jasho la simba ili mtu ampe bibi yake asifanikiwe tunaweza kuhukumu kuchonganisha na sio imani ya huyu Bwana kwamba jasho la simba linafanya mtu asifanikiwe
 
Nenda Kijiji Mahaha, Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza ukawaambie hivyo hadharani uone kitakachokupata.

Sitosahau miaka fulani ya nyuma aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu, tulipoamka asubuhi na kumkuta amelazwa kwenye uwanja wa Sabasaba, jirani na uwanja wa mpira wa Mwanankanda.
Hataliii
 
Swali zuri. Imani bila matendo ni bure. Sasa unaamini vipi mambo hujayaona? 😀

Mimi Dini naamini kama Silaha ya kunifanya niwe mtu mwema ambaye, nisiyopenda kutendewa mimi basi nisimfanyie mwingine. Naamini nilisikia njaa lazima niingie jikoni nipike nikitenge mezani jioe na siyo nikae namuomba Mungu akilete.... Kwa Imani yangu lakini. Na tangu nizaliwe mimi sijaona ile neema iliyoandikwa jangwani kuwa mikate ilishuka. Imeandikwa na maandiko naheshimu kuwa, ilikuwa neema ya Kizazi kile wakati ule kwa Sababu za wakati ule. Ila sasa hivi, bila kazi ya mikono yako na kuvipika viive.....😀 inakuwaje
Mkuu kwani kufanya hayo lazima uamini kwamba Mungu yupo au uamini katika Mungu / Dini ? Nadhani kama unafanya mazuri kwa hofu ya Mungu au usichomwe moto huo ni kama unafiki fulani..., mtu mwema katika jamii ni yule anayeamini katika wema na kutenda wema no matter maandiko yake au muumba wake anamwambia nini..., Muumba hachelewi kukutokea kama yule Abraham / Ibrahim na kukutest ukamtoe fulani kafara........

Point yangu kuu ni kwamba this is a can of worms ukishaanza kuleta mambo ya imani katika uongozi na sheria ambazo watu wana imani tofauti tutakuwa hatufiki cha maana yoyote atakaye-cause harm kwa mwenzake sheria ichukue mkondo wake hao ya imani yaishie kwenye mahekalu, makanisa, misikiti na sehemu za mazindiko.....
 
Nawasikitia sana watu ambao wamebaki kuamini kwamba hapa duniani kuna kitu kinachoitwa uchawi na kinafanya kazi. aisee hakuna kitu kama hicho binadamu ni mnyama tu ana limit zake yako miujiza hawezi tu kufanya mfano kupotea na kwenda kutokea sehemu nyingine au eti kujibadilisha umbo..

kuamini uchawi ni ujinga naini uoga uliopitiliza mimi nimeshapita mazingira mengi sana tu kuanzia makaburini, mabaharini, misituni usiku Kwa usiku na sijawahi kuona badiliko lolote nikalihusisha na eti ni mbinu za kishetani. Maisha yapo tu the way yapo magonjwa yapo ya Kuua so hata Ukifa ghafla hujalogwa tunakupima tunajua ulikuwa na ugonjwa gani..

Zamani kweli mambo mengi yalikuwa hayajagunduliwa maswali yasiyo na majibu yalikuwa mengi.. Pressure, kisukari, kifafa na magonjwa ya akili haya kujulikana hivyo watu akili zao ilibidi ziishie kwenye kuamini uchawi kwamba Ukifa na ugonjwa wasioujua basi umelogwa..

Uchawi upo Kwa dhana kwamba una fanywa (Wana upractice Kwa mazoea yao ila hautendi lolote yaani huwezi ukawa tabora eti umuue mtu yupo dar (hakuna outcome yoyote).

Ndo maana mimi daima napenda mtu ninayefanya naye mijadala awe haamini hakuna uchawi nitamkubali sana nitaona kichwa chake kinaweza ku solve mysterious mbalimbali.. mbona simple tu MUNGU YUPO, UKICHAA UPO, MAARIFA YAPO, NGUVU ZIPO ILA UCHAWI HAUPO LABDA UCHAWA.mwingine unakuta eti kisa tu ana kidonda kilichokataa kupona basi wanaelekeza fikra kwamba ni cha kulogwa cha kichawi mbona ishu kama hiyo ni nyepesi kwamba akili yako haitaki kuamini kama kidonda hakiwezi tu kupona Kwa sababu nyingine za afya au mazingira Mpaka utuhumu uchawi?
Mpaka hapo hesabu umeshatoboa Ndege.😁
 
Naam nimekuuliza wewe definition yako ya uchawi ni ipi ? Nikatoa yangu kwamba neno uchawi ni chochote kile kinachoangamiza /umiza wengine na mwisho nikaonyesha tukiingiza mambo ya Imani / Spirituality ambayo ni ya kufikirika tukayatungia sheria tutaumiza wengi wasio na hatia kinachoweza kufanyika ni kuhukumu matokeo au deeds ambazo mtu amefan...

Kama mtu kachanganya jasho la simba ili mtu ampe bibi yake asifanikiwe tunaweza kuhukumu kuchonganisha na sio imani ya huyu Bwana kwamba jasho la simba linafanya mtu asifanikiwe
Sawa, haya mambo yote yanahusiana nini na post niliyoituma?
 
Sawa, haya mambo yote yanahusiana nini na post niliyoituma?
Iwe club au elimu ila ni ya wachawi. LENGO langu sio kushabikia uchawi. Hayo mengine uko sahihi. Mambo hasi kwenye jamii ni mengi ni lazima tuyashinde ikiwemo na uchawi ili kuwe na jamii yenye maendeleo chanya.
Tuyashinde vipi ? Sababu kama hayapo tunayatungia vipi sheria ? Ndio maana nikasema outcomes zake kama ni mbaya kwa jamii basi sheria tayari zipo tutahukumu accordingly na lile baya lililofanyika..., ila tukisema tuanze kukemea kila tunayedhani ni mchawi kwa definition au mitizamo yetu tutafanya more harm than good..., Ndio maana nilianza kwa kukuuliza kwa wewe uchawi ni nini? Yaani ni kipi unachotaka tukishinde kama jamii ?
 
Mkuu kwani kufanya hayo lazima uamini kwamba Mungu yupo au uamini katika Mungu / Dini ? Nadhani kama unafanya mazuri kwa hofu ya Mungu au usichomwe moto huo ni kama unafiki fulani..., mtu mwema katika jamii ni yule anayeamini katika wema na kutenda wema no matter maandiko yake au muumba wake anamwambia nini..., Muumba hachelewi kukutokea kama yule Abraham / Ibrahim na kukutest ukamtoe fulani kafara........

Point yangu kuu ni kwamba this is a can of worms ukishaanza kuleta mambo ya imani katika uongozi na sheria ambazo watu wana imani tofauti tutakuwa hatufiki cha maana yoyote atakaye-cause harm kwa mwenzake sheria ichukue mkondo wake hao ya imani yaishie kwenye mahekalu, makanisa, misikiti na sehemu za mazindiko.....
Hoja nzuri ila nchi yetu tayari miaka mingi ijayo sheria eneo hili. Tena nimeona humu JF Uzi mmoja walikuwa wamejadili.

Ndugu zangu, sisi tufanye kazi kwa bidii hakuna maendeleo bila kazi za haki. Watu waache kuumiza wengine watakuja wafungwe. Ingekuwa tuna kipindi cha kutembelea watu waliofungwa wakatoka tukawauliza ilikuwaje, tungejifunza mengi
 
Andaa mh. Kongamano hilo tuje kubadilishana utambuzi na maarifa
Sawa, katika mapambano dhidi ya ukatili kwenye jamii tunahitaji majadiliano ya visababishi vingi ikiwemo Imani hizi zimeumizaje wasio na hatia. Kukabiliana na ajenda ngumu kwa maendeleo na ustawi wa jamii liwe jukumu letu wote wanajamii kwa Nia njema tu ya kujenga.
 
SI kwa ubaya lakini naomba kukuulizatu, una ndugu zako kijijini au wote mmezaliwa mjini kwenye good life? Waulize watakupa jibu.

Then turudi kwenye tukio la juzi tu la mauaji ya albino kwanini point ya kwanza watu waseme kuwa watafutwe waganga wa tiba asili? Hao hizo tiba asili zinatokana na mambo gani?

Wengi tunapenda ku pretend kwenye majukwaa lakini uhalisia mnaujua na wengine wanafanya.
Hongera sana. Wewe ni Shujaa wa fikra. Katika jambo linarudisha nyuma maendeleo na ustawi wa jamii ni hizi fikra za kubebeshana hii Imani na kuishi kuwa na hofu miaka yote na kusababisha majanga kwenye jamii.

Nakuunga mkono, tafadhali nipeni ushirikiano natafuta watu jasiri ambao hawakujengwa kwenye hii fikra tuandae mijadala ya wazo tukomboe fikra za wengi.

Mimi mwenyewe siyo muumini wa hizi fikra haya sms tafadhali kwenye 0765345777 turatibu wengine twendeni kwenye ukombozi jamani. Nilianza huu mjadala juzi Instagram pia, yaani kumbe watu wanaweza kukombolewa. Ahsante Sana.

Nasubiri sms yako na ya yeyote anayependa tushirikiane tafadhali anitumie ujumbe nawaomba Sana sana mashujaa🙏🏽
 
Nadhani hata shetani mwenywe akiiona hii thread atashtuka "kumbe kuna myanadamu mijinga hivi?"

Anyway Tumekuelewa SERIKALI
 
Ahsanteni sana jamani kwa kubadilishana mawazo. Haya ngoja wengine tuendelee na ratiba zingine, siku moja nitawaalika kwenye kongamano la mgongano wa fikra dhidi ya vikwazo vya maendeleo na ustawi wa jamii kwa jicho la ukatili utokanao na Imani potofu za kishirikina
DR. Kongamano hilo liwahishe haraka sana tubadilishe fikra za watu wetu, wasomi wakubwa hawajengi vijijini kwao eti watarogwa ujinga uliopitiliza sana
 
Back
Top Bottom