Mkuu uchawi ni nini ?
Kwangu mimi kula rushwa, kuiba mali za watu, uongo uzandiki, kuchonganisha jamii kwamba bibi yako au shangazi yako ndio amekuroga, kutembea uchi kwenye nyumba za watu na kuchafua mazingira yao kufanya vitu visivyoeleweka (kwangu mimi huo ndio uchawi) na kuna sheria za kuweza kuwakabili hao watu sababu ni public nuisance na antisocial behavior
Sasa ukisema tuanze kuhukuma watu kwa definition yako ya uchawi sijui huyu ameingia kwangu ndio maana sipati mali au mtoto wangu kamuua au yule bibi mwenye macho mekundu ndio analeta mkosi mtaani tutaanza kuonea watu na ni hatari sana kwa wale watakaoonewa (persecution)