Katika jambo kubwa ninalojivunia, ni kutambua kuwa hakunaga UCHAWI

By the way mleta uzi ukiamini Mungu yupo basi directly unaamini Mchawi yupo unless turudi pia kwenye definition ya Mungu....

Ndio maana kila siku nasema waasisi wetu walikuwa na busara sana kusema Serikali / Nchi haina Dini bali wanaanchi wake ndio kila mtu kivyake na imani yake....

Sitakushangaa sana ukimuona mtu anaamini kwamba Ngw'anamalundi alikuwa anaweza kutembea kwenye maji na kumuona mjinga lakini nikigundua kwamba unaamini kwamba kuna aliyetembea kwenye maji na kubadilisha kinywaji kimoja na mkate mmoja kuwalisha maelfu na maelfu nitakushangaa sana na kuona huenda umekuwa indoctrinated...., Kama sio Hapa kwanini Kule ?

To each his / her Own....
 
Mkuu,
Umeuliza uchawi ni nini, umetoa perception yako kuhusu uchawi na last paragraph I cannot relate. It seems, it's you against youself
Naam nimekuuliza wewe definition yako ya uchawi ni ipi ? Nikatoa yangu kwamba neno uchawi ni chochote kile kinachoangamiza /umiza wengine na mwisho nikaonyesha tukiingiza mambo ya Imani / Spirituality ambayo ni ya kufikirika tukayatungia sheria tutaumiza wengi wasio na hatia kinachoweza kufanyika ni kuhukumu matokeo au deeds ambazo mtu amefan...

Kama mtu kachanganya jasho la simba ili mtu ampe bibi yake asifanikiwe tunaweza kuhukumu kuchonganisha na sio imani ya huyu Bwana kwamba jasho la simba linafanya mtu asifanikiwe
 
Sijawahi amini kabisa huo upumbavu, kijijini niliwaambia waniroge nikaishia kuitwa mimi ndo mchawi mwenyewe!
Imani za uchawi zipo direct proportional na ujinga!
Kuna watu ni mazuzu ukiwaambia wakuthibitishie wanakuambia wewe ndio mchawi hawana jipya.
 
Hataliii
 
Mkuu kwani kufanya hayo lazima uamini kwamba Mungu yupo au uamini katika Mungu / Dini ? Nadhani kama unafanya mazuri kwa hofu ya Mungu au usichomwe moto huo ni kama unafiki fulani..., mtu mwema katika jamii ni yule anayeamini katika wema na kutenda wema no matter maandiko yake au muumba wake anamwambia nini..., Muumba hachelewi kukutokea kama yule Abraham / Ibrahim na kukutest ukamtoe fulani kafara........

Point yangu kuu ni kwamba this is a can of worms ukishaanza kuleta mambo ya imani katika uongozi na sheria ambazo watu wana imani tofauti tutakuwa hatufiki cha maana yoyote atakaye-cause harm kwa mwenzake sheria ichukue mkondo wake hao ya imani yaishie kwenye mahekalu, makanisa, misikiti na sehemu za mazindiko.....
 
Mpaka hapo hesabu umeshatoboa Ndege.😁
 
Sawa, haya mambo yote yanahusiana nini na post niliyoituma?
 
Sawa, haya mambo yote yanahusiana nini na post niliyoituma?
Iwe club au elimu ila ni ya wachawi. LENGO langu sio kushabikia uchawi. Hayo mengine uko sahihi. Mambo hasi kwenye jamii ni mengi ni lazima tuyashinde ikiwemo na uchawi ili kuwe na jamii yenye maendeleo chanya.
Tuyashinde vipi ? Sababu kama hayapo tunayatungia vipi sheria ? Ndio maana nikasema outcomes zake kama ni mbaya kwa jamii basi sheria tayari zipo tutahukumu accordingly na lile baya lililofanyika..., ila tukisema tuanze kukemea kila tunayedhani ni mchawi kwa definition au mitizamo yetu tutafanya more harm than good..., Ndio maana nilianza kwa kukuuliza kwa wewe uchawi ni nini? Yaani ni kipi unachotaka tukishinde kama jamii ?
 
Hoja nzuri ila nchi yetu tayari miaka mingi ijayo sheria eneo hili. Tena nimeona humu JF Uzi mmoja walikuwa wamejadili.

Ndugu zangu, sisi tufanye kazi kwa bidii hakuna maendeleo bila kazi za haki. Watu waache kuumiza wengine watakuja wafungwe. Ingekuwa tuna kipindi cha kutembelea watu waliofungwa wakatoka tukawauliza ilikuwaje, tungejifunza mengi
 
Andaa mh. Kongamano hilo tuje kubadilishana utambuzi na maarifa
Sawa, katika mapambano dhidi ya ukatili kwenye jamii tunahitaji majadiliano ya visababishi vingi ikiwemo Imani hizi zimeumizaje wasio na hatia. Kukabiliana na ajenda ngumu kwa maendeleo na ustawi wa jamii liwe jukumu letu wote wanajamii kwa Nia njema tu ya kujenga.
 
SI kwa ubaya lakini naomba kukuulizatu, una ndugu zako kijijini au wote mmezaliwa mjini kwenye good life? Waulize watakupa jibu.

Then turudi kwenye tukio la juzi tu la mauaji ya albino kwanini point ya kwanza watu waseme kuwa watafutwe waganga wa tiba asili? Hao hizo tiba asili zinatokana na mambo gani?

Wengi tunapenda ku pretend kwenye majukwaa lakini uhalisia mnaujua na wengine wanafanya.
 
Nadhani hata shetani mwenywe akiiona hii thread atashtuka "kumbe kuna myanadamu mijinga hivi?"

Anyway Tumekuelewa SERIKALI
 
DR. Kongamano hilo liwahishe haraka sana tubadilishe fikra za watu wetu, wasomi wakubwa hawajengi vijijini kwao eti watarogwa ujinga uliopitiliza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…