Katika kipindi hiki cha Pasaka jamaa mmoja ameenda na kondoo Hekaluni huko Israel

Echolima1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
9,662
Reaction score
8,023
Katika kipindi hiki cha Pasaka huko Jerusalem Israel jamaa mmoja jana alienda Hekaluni akiwa na kondoo kwa nia ya kwenda kutoa sadaka ya kuteketezwa baadaye Alikamatwa na polisi walieko kwenye eneo hilo ambalo ni Takatifu kwa Wayahudi, Wakristo na waislamu.

Eneo hilo lilikabidhiwa waislam ndiyo wanaweza kuingia ndani na wayahudi hawaruhusiwi kusali ndani ya Hekalu hilo.
 
Attachments

  • telegram-cloud-document-4-6046464030279734287.mp4
    6 MB
Shida amevaa kisasa halafu na mkamera!, angevaa ile kizamani kama akina petro halafu na upanga pembeni huku kashikilia fimbo!, hapo wangekuwa wanajiuliza huyu ndo yeye ama!..🤣
 
Katika kipindi hiki cha Pasaka huko Jerusalem Israel jamaa mmoja jana alienda Hekaluni akiwa na kondoo kwa nia ya kwenda kutoa sadaka ya kuteketezwa baadaye Alikamatwa na polisi walieko kwenye eneo hilo ambalo ni Takatifu kwa Wayahudi,Wakristo na waislamu. Eneo hilo lilikabidhiwa waislam ndiyo wanaweza kuingia ndani na wayahudi hawaruhusiwi kusali ndani ya Hekalu hilo.
Sawa. Asante kwa taarifa.
Ukinawa uso pia usikose kutuhabarisha
 
Katika kipindi hiki cha Pasaka huko Jerusalem Israel jamaa mmoja jana alienda Hekaluni akiwa na kondoo kwa nia ya kwenda kutoa sadaka ya kuteketezwa baadaye Alikamatwa na polisi walieko kwenye eneo hilo ambalo ni Takatifu kwa Wayahudi, Wakristo na waislamu.

Eneo hilo lilikabidhiwa waislam ndiyo wanaweza kuingia ndani na wayahudi hawaruhusiwi kusali ndani ya Hekalu hilo.

Unajua ni kwa nini Wayahudi hawaruhusiwi kuingia ndani?
Ni kwa sababu mafunzo yao yanasema ni mpaka Masihi wao aje. Kwenye hili Wayahudi wa Orthodox wamelishikilia kwa nguvu mpaka Mazionists wanagwaya!

Kitu pekee kilichowashinda Wayahudi wafuata dini ni Ishu ya Kurudi Israel, Walijitahidi sana kuwazuia Mazionists wasijichukulie mamuzi mikononi kurudi Israel kabla ya Masihi, lakini Mazionists waliamua lolote na liwe. Wakarudi kibabe kinyume cha mafundisho ya dini yao. Mbinu waliyoitumia Mazionists kuwaconvince Wayahudi wafuata dini ni pamoja na ugaidi, walikuwa wanakwenda wanabomb masinagogi ya Wayahudi ktk nchi za kiarabu halafu wanansema mnaona hamko salama hapa twendeni Israel.

Mbinu nyingine waliyotumia ni incentives kwa shule za dini ya Kiyahudi, Wayahudi wafuata dini wakawa wanapokea ruzuku, wakawa wanakuwa exempted katika military service etc.

Lakini bado kuna kundi kubwa la orthodox Jews ambao wanaona kuwa uwepo wa Taifa la Israel la leo ni uasi mwingine mbele ya Mungu aliyewaexile
 
Endelea kuwadanganya wajinga!!
 
Hayo uliyoyaongea hapo ni uongo ukweli ni huu hapa:

Wayahudi hawaingi ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa kwa sababu za kidini, kihistoria, na kisiasa. Msikiti wa Al-Aqsa uko kwenye eneo linalojulikana kama Haram al-Sharif kwa Waislamu na Mlima wa Hekalu (Har HaBayit) kwa Wayahudi, ambalo ni patakatifu kwa dini zote mbili. Hapa kuna sababu za msingi:

1. Marufuku ya Kidini: Kulingana na baadhi ya tafsiri za sheria za Kiyahudi (Halakha), Rabbi Mkuu wa Israel amepiga marufuku Wayahudi kuingia kwenye eneo la Mlima wa Hekalu, ambalo linajumuisha Msikiti wa Al-Aqsa, kwa kuwa mahali hapo inaaminika ni Patakatifu pa patakatifu. Wanafikiri kuwa kuingia hapo kunaweza kupanajisi, hasa kwa sababu eneo la Patakatifu pa Patakatifu (ambalo Wayahudi wengi wanaamini liko hapo) linahitaji utakaso wa Ki-Ibada ambazo haziwezekani kufanyika sasa kwa sababu ya ukosefu wa hekalu.

2. Mvutano wa Kisiasa: Eneo la Msikiti wa Al-Aqsa limekuwa kitovu cha mzozo kati ya Waislamu na Wayahudi kwa muda mrefu. Waislamu wanaona msikiti huu kama wa tatu kwa utakatifu katika Uislamu, na udhibiti wake unasimamiwa na Wakfu wa Kiislamu chini ya Jordan. Kuanzia mwaka 2003, Israel ilianza kuruhusu Wayahudi kutembelea eneo hilo kama watalii chini ya ulinzi wa polisi, lakini hawaruhusiwi kusali hapo ili kuepuka migogoro. Hata hivyo, baadhi ya Wayahudi waliovaa kama Waislamu wamejaribu kuingia na kusali, jambo ambalo limezusha mvutano zaidi.

3. Hali Iliyopo (Status Quo): Kuna makubaliano ya kihistoria yanayoitwa “hali iliyopo,” ambayo yanadhibiti upatikanaji wa eneo hili. Waislamu wana ruhusa ya kusali ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa, lakini Wayahudi wanaweza kutembelea eneo la nje (kama Ukuta wa Magharibi) au sehemu za Mlima wa Hekalu kama watalii tu, bila kusali. Hii ni kujaribu kudumisha amani katika eneo linalochukuliwa kuwa la kumudu sana.

4. Migogoro ya Kiitikadi: Baadhi ya vikundi vya Wayahudi wenye msimamo mkali, kama vile wale wanaotaka kujenga Hekalu la Tatu, wanashinikiza kuruhusu Wayahudi kuingia na kusali katika eneo hilo, lakini hii inapingwa vikali na Waislamu na jamii ya kimataifa, kwani inaweza kuongeza mzozo. Kwa sababu hiyo, serikali ya Israel mara nyingi hudumisha marufuku ya Wayahudi kuingia ndani ya msikiti yenyewe ili kuzuia ghasia.

Kwa muhtasari, marufuku hii inatokana na mchanganyiko wa imani za kidini zinazozuia Wayahudi kuingia katika maeneo yanayochukuliwa kuwa patakatifu sana, pamoja na jitihada za kisiasa za kudumisha utulivu katika eneo lenye mvutano wa kihistoria. Hata hivyo, hali hii inabaki kuwa tete, na matukio ya mvutano bado yanatokea mara kwa mara.
 
Katika kipindi hiki cha Pasaka huko Jerusalem Israel jamaa mmoja jana alienda Hekaluni akiwa na kondoo kwa nia ya kwenda kutoa sadaka ya kuteketezwa baadaye Alikamatwa na polisi walieko kwenye eneo hilo ambalo ni Takatifu kwa Wayahudi, Wakristo na waislamu.

Eneo hilo lilikabidhiwa waislam ndiyo wanaweza kuingia ndani na wayahudi hawaruhusiwi kusali ndani ya Hekalu hilo.
Mpoland
 
Sasa ibada yao wayahudi huwa na kuchinja, kondoo, au njiwa au ng'ombe kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi na makosa mbali mbali.
Je hawafanyi kama isemavyo Torati?
Vipi kuhani mkuu kwa sasa Israel wanaye?
 
Kesho tena tunaenda kwenye hilo hekalu tutapata mengi sana lakini kutokana na maswali yako sasa hivi hawatoi sadaka za kuteketezwa au kuchinja sababu kubwa ni kwa sababu hakuna Hekalu mpaka wajenge Hekalu la Tatu ambalo linatakiwa liwe pale ulipo msikiti wa Al-Aqsa wenye dini yao huwa wanataka kuuvunja msikiti huo ili wajenge Hekalu lao hapo na wakishajenga ndipo Kuhani Mkuu wanaweza kumweka kwa sasa hivi yupo Chief-Rabbi Kalman Ber na Rabbi David Yousef. walichaguliwa mwaka jana 2024 watatumikia wadhifa huo kwa miaka kumi. Kwa ujumla Ibada nyingi hawafanyi kwa sababu ya hakuna Hekalu mara zote IBADA hufanyikia western wailing wall Ukuta wa Magharibi hapo ndipo askari wote wa Israel wanaapishwa hapo.
 
Shida amevaa kisasa halafu na mkamera!, angevaa ile kizamani kama akina petro halafu na upanga pembeni huku kashikilia fimbo!, hapo wangekuwa wanajiuliza huyu ndo yeye ama!..🤣
Kwenda na wakati. Yesu angekuja leo ungekuta ana jinsi ya kuchanika.
 
Kesho tena tunaenda kwenye hilo hekalu tutapata mengi sana lakini kutokana na maswali yako sasa hivi hawatoi sadaka za kuteketezwa au kuchinja sababu kubwa ni kwa sababu hakuna Hekalu mpaka wajenge Hekalu la Tatu ambalo linatakiwa liwe pale ulipo msikiti wa Al-Aqsa wenye dini yao huwa wanataka kuuvunja msikiti huo ili wajenge Hekalu lao hapo na wakishajenga ndipo Kuhani Mkuu wanaweza kumweka kwa sasa hivi yupo Chief-Rabbi Kalman Ber na Rabbi David Yousef. walichaguliwa mwaka jana 2024 watatumikia wadhifa huo kwa miaka kumi. Kwa ujumla Ibada nyingi hawafanyi kwa sababu ya hakuna Hekalu mara zote IBADA hufanyikia western wailing wall Ukuta wa Magharibi hapo ndipo askari wote wa Israel wanaapishwa hapo.
Sawa mkuu, ila sasa dini yao kwa sasa itakuwa hawako sawa, kwa sababu lazima kuwe na utoaji wa sadaka za upatanisho ambazo huwa kwa mtu mmoja au ile ya kila mwaka ya upatanisho kwa taifa zima,
Au hawa waliopo nikubaliane na watu mbalimbali wenye kusema si Waisraeli halisi?
 
Ili ibada ikamilike lazima kuna mambo lazima yawepo kwao hayo yote hayawezi kukamilika mpaka Hekalu lijengwe sadaka kama hizo ni lazima zifanyike kwenye Hekalu na sasa hilo halipo!! Maana lilivunjwa na sehemu hiyo pakajengwa Msikiti wa Al-Aqsa. Kingine kuna Ibada zingine haziwezi kufanyika kwa sababu hakuna Kuhani Mkuu. Ndiyo maana wenye hiyo dini wanafanya kila njia ili Hekalu la tatu lijengwe maana kila kitu walishaandaa watumishi, Vyombo vya Hekaluni na wale Ng’ombe wa kutolea sadaka( Heifer ). Na ni Propaganda tu kusema kuna wayahudi fake!! Huku hakuna ubaguzi tuliokuwa tunaaminishwa na wafuga Midevu na Majini huku wakristo wako wengi sana na kuna watanzania wako huku wanaishi kwa Amani bila shida yoyote!!
 
Ok shukurani, si lazima kufanya taratibu za ibada yao hadi iwe hekaluni, Kipindi cha Mussa walifanyia kwenye hema, haikuwa hekalu, walipoingia Nchi ya ahadi kabla ya ujenzi wa hekalu walikuwa wanaenda mahali pa Juu Gibeoni,
Any way wao na dini yao
 
Back
Top Bottom