SoC04 Katika kurahisisha huduma za jamii na maendeleo, serikali ichukue jukumu la kujenga minara ya mawasiliano maeneo yaliyoko mbali na miji (vijijini)

SoC04 Katika kurahisisha huduma za jamii na maendeleo, serikali ichukue jukumu la kujenga minara ya mawasiliano maeneo yaliyoko mbali na miji (vijijini)

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jan 3, 2024
Posts
26
Reaction score
25
Kutokana na umuhimu wa mawasiliano ya simu ya mkononi pamoja na internet iko haja kwa serikali kujenga miundombinu ya mawasiliano ya simu za mkononi na internet kwenye maeneo yote ambayo yako mbali na mijini ili kuyapunguzia mzigo wa gharama makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano ambayo kwa namna moja ama nyingine yanakwepa gharama za kujenga miundombinu kwa kigezo kuwa maeneo hayo hayana watumiaji wengi ambao wanaweza kufidia gharama hizo punde miradi yao inapoanza kufanya kazi. Kukosekana kwa huduma za mawasiliano kwenye maeneo ya mbali na miji kunaleta changamoto nyingi zikiwemo za kiafya, elimu, kiuchumi na kiusalama.

Mfano eneo la Iyovi liliko kati Mikumi na Ruaha mbuyuni lenye urefu usiopungua KM 80 halina mawasiliano ya simu jambo ambalo ni hatari kwa wasafiri pundi wanapoweza kupata shida ya kiusalama katika eneo hilo kwani hakuna njia mbadala ya kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama zaidi ya barabara. Mawasiliano ya simu na internet hurahisisha sana utoaji wa huduma, mfano; daktari aliyeko kijijini anaweza kujiongezea maarifa kupitia internet au kupiga simu kwa mtaalamu kutoka kituo kingine cha afya na akaweza kutatua shida ya mgonjwa wake kwa wakati bila kumpa rufaa.

Kiusalama wote tunajua taarifa za dharura husambaa kwa haraka zaidi kwa njia ya mtandao yaani internet na simu iwe ni kukatika kwa mawasiliano ya barabara, uvamizi pamoja na ajali ni miongoni mwa mifano. Bila kusahau kielimu internet imekuwa chanzo bora cha maarifa kwa wanaotaka kujifunza au kuongeza maarifa katika shughuli zao ikiwemo kwa walimu, madaktari,wanafunzi, wafanyabiashara na kadhalika. Fursa kama hizo watu walioko mbali na miji mikubwa wanazikosa kutokana na kukosa miundombinu ya mawasiliano na internet.

Hivyo basi naishauri serikali iweze kuchukua jukumu la kujenga minara katika maeneo yote ya mbali na miji mikubwa ili makampuni ya simu za mkononi yaweze kukodi minara hiyo na kufunga antena zao za mawasiliano na internet ili yaweze kutoa huduma bora kwenye maeneo hayo kwa gharama nafuu bila kuathiri (athari hasi)uchumi wa kampuni husika na kuwaacha wananchi wa maeneo husika kufurahia huduma za mawasiliano na internet, kwasababu mnara ukiwa unamilikiwa na serikali unatoa fursa kwa kampuni zaidi ya moja kupanga kwenye mnara husika huku kila kampuni ikiwa na antena zake za mawasiliano na internet.
 
Upvote 2
Hivyo basi naishauri serikali iweze kuchukua jukumu la kujenga minara katika maeneo yote ya mbali na miji mikubwa ili makampuni ya simu za mkononi yaweze kukodi minara hiyo na kufunga antena zao za mawasiliano na internet ili yaweze kutoa huduma bora kwenye maeneo hayo
Huu ni ushauri mzuri, ukizingatia umezungumzia matumizi ya intaneti ya kujifunzia zaidi na vitu kama hivyo.

Kwa kweli kuwa na uwezo wa kuipata intaneti huwa ni 'priveledge' moja nzuri sana tu.
 
Back
Top Bottom