shule za kata ni moja ya kitu muhimu zaidi alichoifanyia Tanzania, na hakitasahaulika...
Shule za kata ziliasisiwa wakati wa Mkapa.
Shule hizo zilianza ujenzi wake miaka ya kuanzia 2001.
Ilikuwa hivi, kipindi hicho shule zote za kata zilijengwa kwa nguvu za wananchi (kuanzia msingi mpaka kuezeka mpaka finishing).
Kata ambazo walilipokea wazo hilo positively, walichangishana haraka haraka na wakaweza kuanza masomo mapema. Ndiyo maana shule nyingi za kata ambazo kwa sasa ni kongwe kidogo zilianza 2002.
Waliochelewa kidogo walianza 2004, 2005.
Kisha kuna waliokuwa wazembe hao walianza mwaka 2006 miezi ya mwanzoni. Na hao ilibidi waziri mkuu wa enzi hizo Hayati Lowasa awe mkali (nakumbuka hotuba zake sehemu mbalimbali kwa wazembe alivyowawashia moto wakurugenzi kuhakikisha michango inachangwa kwa haraka). Yaani kwa waliochelewa chukulia kama ujenzi wa SGR, uanze wakati wa Magufuli ukamilike wakati wa Samia.
Wakati wa Jakaya, alihakikisha shule zinapata walimu, kwanza kwa kuanzisha ile kitu ilikuwa maarufu kwa jina la walimu wa vodafasta (mwaka 2007, 2008).
Kuanzia mwaka 2011, ndipo walimu walianza kuajiriwa kwa wingi (kila mwaka hadi 2015).
Najaribu kuweka kumbukumbu zangu katika jukwaa kwa kuwa niliona kwa macho yangu namna wazazi walivyokuwa wakijificha kukwepa michango ya kuasisi shule za kata. Na ili wananchi wasiwe na mamichango mengi, kodi ya kichwa (Tsh 4,000/=) ilifutwa rasmi. Katika kata nyingi (hasa za wilaya niliyozaliwa, michango ilikuwa ni Tsh 10,000/= kwa kila darasa. Na kurahisisha kazi, kama kata ilikuwa na vijiji 7, kila kijiji kilipaswa kujenga darasa moja moja kwa kuanzia na baada ya hapo kuendelea na ujenzi wa kuongezea madarasa.
Kama wilaya uliyotoka walichelewa kuanza masomo na wakaanza wakati wa Jakaya, jua kuwa walikuwa na wasimamizi wa wilaya wazembe. Naweza kukutajia shule zote za kata ndani ya wilaya yangu walioanza mwaka 2002, 2003, 2004, 2005 na waliochelewa na kuanza 2006 mwezi wa kwanza, pili au tatu.
Kabla sijamaliza, si unakumbuka MMEM na MMES? Sasa hiyo MMES ndiyo iliyochochea uongezaji wa mashule ya sekondari kwa kuasisi mashule ya kata nchini.
MMEM - mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi.
MMES - Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari.
Katika kuhakikisha shule zinapata walimu wa kutosha, ndipo mpango wa kujenga chuo cha UDOM ukaasisiwa (ndiyo maana wengine hukiita chuo cha kata). Ujenzi ulianza awamu ya Rais Kikwete.
Credit ya shule za sekondari inaangukia kwa awamu ya Kikwete (akiimbwa zaidi Loawasa) kwa kuwa katika wilaya nyingi, wazazi walikuwa wazembe kuchangia na hivyo hawakukamilishi majengo wakati wa awamu ya Mkapa, na ndipo Lowasa akasuma ajenda hiyo kwa nguvu sana kwa wilaya zote zembe zembe.
Shule za kata ujenzi wake ulikuja kupata sapoti ya serikali awamu ya Magufuli, ilikuwa wazazi wanachangishana kuanzia msingi hadi kumaliza boma lote, uezekaji na finishing ikawa inamalizia serikali.
Awamu ya Rais Samia, shule za kata ujenzi wake wa madarasa umekuwa chini ya serikali (kuanzia 2021 disemba chini ya program ya Covid 19).