Katika Marais wote waliopita Tanzania namkubali Kikwete zaidi

Katika Marais wote waliopita Tanzania namkubali Kikwete zaidi

Usisahau ufisadi wa kiwango cha juu, madawa ya kulevya, magenge ya uhalifu kama kibiti, kuuza gesi yote ya mtwara kwa wachina, IPTL, nk! Please be serious
Acha kuongopa magenge ya kibiti sio wakati wa Kikwete
 
View attachment 3217066

sijui ni kwanini Legacy yake haizumgumziwi kabisa,

shule za kata ni moja ya kitu muhimu zaidi alichoifanyia Tanzania, na hakitasahaulika...

Mwana demokrasia na mwana diplomasia ambae hakuna aliyewahi kumfikia Tanzania hii...

Hata chuo kikuu cha UDOM na miradi mingine ameitekeleza yeye mwenyewe akiwa madarakani.

lakini hakuna anaeongelea na kupongeza jitihada
zake.

ni kwasababu ya hulka yake na demokrasia yake ya kuruhusu kila kitu kusemwa hadharani ? l


Legend JK
Mimi namkubali
JK
Samia
Mkapa

Ila naheshimu mchango wa baba wa Taifa.
 
View attachment 3217066

sijui ni kwanini Legacy yake haizumgumziwi kabisa,

shule za kata ni moja ya kitu muhimu zaidi alichoifanyia Tanzania, na hakitasahaulika...

Mwana demokrasia na mwana diplomasia ambae hakuna aliyewahi kumfikia Tanzania hii...

Hata chuo kikuu cha UDOM na miradi mingine ameitekeleza yeye mwenyewe akiwa madarakani.

lakini hakuna anaeongelea na kupongeza jitihada
zake.

ni kwasababu ya hulka yake na demokrasia yake ya kuruhusu kila kitu kusemwa hadharani ? l


Legend JK
Na ndo aliye asisi mpango wa kusambaza umeme vijijini REA ambao mpaka sasa umesaidia watanzania wengi kupata nishati ya umeme.
 
Walikufa?
Unawaongezea mshahara wezi majambazi tena wenye vyeti feki?

Ww umesikia wapi watu wanaongezewa mshahara kama peremende.?

Kuna nchi yeyote ile unayoijua inawaongezea mishahara watu wake kiholelaholela?
PAMOJA NA UWEPO WA WATUMISHI HEWA LAKINI BADO ALIFANIKIWA
1)kuajiri watumishi kila mwaka
2)alipandisha madaraja watumishi kwa wakati kila baada ya miaka 3
3)Aliongeza mishahara ya watumishi wa umma.
4)HUDUMA ZA AFYA MATIBABU YA KIBINGWA kama hospitali ya JKCI huduma za afya hii ilipunguza watu kwenda kutibiwa INDIA magonjwa ya moyo...KWA WATUMISHI WA UMMA WATAMKUMBUKA KWA HILO LA KUAJIRI KILA MWAKA,KUPANDISHA MADARAJA,ANNUAL INCREMENT,NA KUWAONGEZEA MSHAHARA KWA KIWANGO KIKUBWA AMBACHO HAKIKUWAHI KUTOKEA KABLA.
 
Hii nchi ina wapumbavuh wengi mpaka naona aibu hata kurudi Kuja Ishi Tanzania. Ngoja niendelee kubaki ishi huku ughaibuni. Wewe utakuwa ni Division 5 kilaza wa vyeti fake.
hahhhah nyie ndo mnapenda drama watu kutumbuliwa jukwaani na propagana ya kuitwa wanyonge
 
JK Kuna malafa flani km huyu ambao wanamchukia na hawataki kusema ukweli lkn Kuna mengi amefanya (sijasema Hana madhaifu.......hayo Kila mtu anayo). Kuna kitu flani wakati wa JPM walilishwa wanyonge na ghafla wakaibuka na chuki kubwa dhidi yake. Matokeo yakawa Kila alichokifanya basi anapewa JPM. Nitatoa mifano michache;
-Wanyonge wanaamini mwendo Kasi ni JPM (ukweli ni jk ndiye aliyeasisi na kuanza kushughulikia)
-Flyovers wanyonge wanaamini ni JPM (ukweli ni uasiso wa jk)
-wanyonge wanaamini jk hajajenga barabara Bali ni JPM. Ukweli hakuna aliyejenga mtandao mrefu wa barabara kumzidi jk.
Na mengine meeeengi, hayo ni kwa uchache tu.

Jk analipwa chuki, wengi tukiwa hata hatujui kwanini tunamchukia Bali tunafuata tu tulichoambiwa.

Ila jamaa ni mwamba kweli kweli, Hana hoyana na mtu. Anawaonyesha tu tabasamu na Mungu anamjaalia mambo yake yanaenda vizuri sana.....no stress. Wanamchukia na kujaribu kumharibia wanachemka wao Huku wakimuacha vilevile. Kina Bashe na Makonda wamejaribu sana kumfuatafuata lakini kawakaushia na wanajikuta wanahangaika wao peke yao.
Michepuko mkipenda huwa akili hamtumii kabisa. Mnasifia hata takataka. Ngoja mkewe akusome.
 
Subiri kupigwa pingu, Trump hawataki, Waingereza hawawataki, yaani hakuna mzungu anayekuhitaji huko na labda unarudi na singlendi😂😂😂😂😂😜
Division 5. Singlendi ni nini? Mimi nipo sana USA. sina mpango wa kurudi huko mnakoongozwa na vilaza....nanyi mnashabikia hao vilaza mkiwa mmebemendwa kiakili. Nmeoa na nina mtoto wa mwanamke wa kizungu. Kifupi siyo illegal.
 
Aisifuye mvua imemnyeshea !
Watu wengi ni maSelfish kwa Asili yao !
Ilimradi kama yeye alinufaika katika kipindi fulani au ananufaika kwa sasa utawajua tu wanavyofagilia !

Ni wachache sana humu wanaosema kweli, kweli tupu !

Wengi humu ni wale akina Muamba Ngoma huvutia upande wake !
Kazi kweli kweli !
 
Ukitumia kigezo cha aliyefanya Makubwa ni Mkapa,
Ukisema Rais bora ni Nyerere,ni basi tu kidunia nguvu za ubepari zilizidi zile za kijama,kunafanya umuhimu wake odhoofike-ila ukweli ni kuwa Nyerere is the best na sidhani kama tutakuja kumpata Nyerere mwingine.

Laiti kama kusingekuwa na propaganda za kuangusha Serikali za kijamaa zilizofanywa na western countries,vile viwanda alivyoanzisha Nyerere karibu kila Mkoa sa hivi tungekuwa mbali sana kiuchumi.
 
Ukitumia kigezo cha aliyefanya Makubwa ni Mkapa,
Ukisema Rais bora ni Nyerere,ni basi tu kidunia nguvu za ubepari zilizidi zile za kijama,kunafanya umuhimu wake odhoofike-ila ukweli ni kuwa Nyerere is the best na sidhani kama tutakuja kumpata Nyerere mwingine.

Laiti kama kusingekuwa na propaganda za kuangusha Serikali za kijamaa zilizofanywa na western countries,vile viwanda alivyoanzisha Nyerere karibu kila Mkoa sa hivi tungekuwa mbali sana kiuchumi.
Mkapa Mr Ubinafsishaji akaandika kwenye kitabu chake kwamba amejuta sana kuvibinafsisha vile viwanda !

Kujuta peke yake ilikuwa haitoshi !
Ingekuwa ni China 🇨🇳 ingekuwa habari nyingine 😳😳😱 !
 
Viongozi wengi walitakiwa wapate Darasa la huyu Mwamba!! Aanzishe hata chuo Cha kufundisha siasa Africa
 
Shule za kata ziliasisiwa wakati wa Mkapa.

Shule hizo zilianza ujenzi wake miaka ya kuanzia 2001.

Ilikuwa hivi, kipindi hicho shule zote za kata zilijengwa kwa nguvu za wananchi (kuanzia msingi mpaka kuezeka mpaka finishing).

Kata ambazo walilipokea wazo hilo positively, walichangishana haraka haraka na wakaweza kuanza masomo mapema. Ndiyo maana shule nyingi za kata ambazo kwa sasa ni kongwe kidogo zilianza 2002.

Waliochelewa kidogo walianza 2004, 2005.

Kisha kuna waliokuwa wazembe hao walianza mwaka 2006 miezi ya mwanzoni. Na hao ilibidi waziri mkuu wa enzi hizo Hayati Lowasa awe mkali (nakumbuka hotuba zake sehemu mbalimbali kwa wazembe alivyowawashia moto wakurugenzi kuhakikisha michango inachangwa kwa haraka). Yaani kwa waliochelewa chukulia kama ujenzi wa SGR, uanze wakati wa Magufuli ukamilike wakati wa Samia.

Wakati wa Jakaya, alihakikisha shule zinapata walimu, kwanza kwa kuanzisha ile kitu ilikuwa maarufu kwa jina la walimu wa vodafasta (mwaka 2007, 2008).

Kuanzia mwaka 2011, ndipo walimu walianza kuajiriwa kwa wingi (kila mwaka hadi 2015).

Najaribu kuweka kumbukumbu zangu katika jukwaa kwa kuwa niliona kwa macho yangu namna wazazi walivyokuwa wakijificha kukwepa michango ya kuasisi shule za kata. Na ili wananchi wasiwe na mamichango mengi, kodi ya kichwa (Tsh 4,000/=) ilifutwa rasmi. Katika kata nyingi (hasa za wilaya niliyozaliwa, michango ilikuwa ni Tsh 10,000/= kwa kila darasa. Na kurahisisha kazi, kama kata ilikuwa na vijiji 7, kila kijiji kilipaswa kujenga darasa moja moja kwa kuanzia na baada ya hapo kuendelea na ujenzi wa kuongezea madarasa.

Kama wilaya uliyotoka walichelewa kuanza masomo na wakaanza wakati wa Jakaya, jua kuwa walikuwa na wasimamizi wa wilaya wazembe. Naweza kukutajia shule zote za kata ndani ya wilaya yangu walioanza mwaka 2002, 2003, 2004, 2005 na waliochelewa na kuanza 2006 mwezi wa kwanza, pili au tatu.

Kabla sijamaliza, si unakumbuka MMEM na MMES? Sasa hiyo MMES ndiyo iliyochochea uongezaji wa mashule ya sekondari kwa kuasisi mashule ya kata nchini.
MMEM - mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi.
MMES - Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari.

Katika kuhakikisha shule zinapata walimu wa kutosha, ndipo mpango wa kujenga chuo cha UDOM ukaasisiwa (ndiyo maana wengine hukiita chuo cha kata). Ujenzi ulianza awamu ya Rais Kikwete.

Credit ya shule za sekondari inaangukia kwa awamu ya Kikwete (akiimbwa zaidi Loawasa) kwa kuwa katika wilaya nyingi, wazazi walikuwa wazembe kuchangia na hivyo hawakukamilishi majengo wakati wa awamu ya Mkapa, na ndipo Lowasa akasuma ajenda hiyo kwa nguvu sana kwa wilaya zote zembe zembe.

Shule za kata ujenzi wake ulikuja kupata sapoti ya serikali awamu ya Magufuli, ilikuwa wazazi wanachangishana kuanzia msingi hadi kumaliza boma lote, uezekaji na finishing ikawa inamalizia serikali.

Awamu ya Rais Samia, shule za kata ujenzi wake wa madarasa umekuwa chini ya serikali (kuanzia 2021 disemba chini ya program ya Covid 19).
Shule za kata ni wakati wa JK na Lowasa akiwa waziri mkuu, so sifa ya shule za kata inamuhusu Kikwete kupitia kwa Waziri Mkuu Lowasa ambaye alihamasisha sana na sio vinginevyo!!
 
View attachment 3217066

sijui ni kwanini Legacy yake haizumgumziwi kabisa,

shule za kata ni moja ya kitu muhimu zaidi alichoifanyia Tanzania, na hakitasahaulika...

Mwana demokrasia na mwana diplomasia ambae hakuna aliyewahi kumfikia Tanzania hii...

Hata chuo kikuu cha UDOM na miradi mingine ameitekeleza yeye mwenyewe akiwa madarakani.

lakini hakuna anaeongelea na kupongeza jitihada
zake.

ni kwasababu ya hulka yake na demokrasia yake ya kuruhusu kila kitu kusemwa hadharani ? l


Legend JK
Mkapa,kikwete,na Samia, ni viongozi wa mfano kabisa,yule dikteta sijui alitokea wapi!?
 
Shule za kata ni wakati wa JK na Lowasa akiwa waziri mkuu, so sifa ya shule za kata inamuhusu Kikwete kupitia kwa Waziri Mkuu Lowasa ambaye alihamasisha sana na sio vinginevyo!
Nimeshaeleza na sirudii.

Kama shule za kata zilikuwa kwa nguvu ya wananchi, ilikuwaje shule zilizochelewa zilianzishwa 2006 mwanzoni?

Shule za kata ziliasisiwa wakati wa Mkapa, sema kwa kuwa zilikuwa zinajengwa kwa nguvu za wananchi, kata zilizosimamia kivivu ndiyo walichelewa na ndipo Lowasa alipoingia aka-push agenda fasta kwa ukali, ndipo viongozi legelege nao wakawawashia moto wananchi na wakaharakisha ujenzi.

Kama wilaya unayotoka hakuna shule ya kata iliyoanza ama mwaka 2004, 2005 au 2006 mwanzoni, jua umezaliwa wilaya ya majitu mavivu. Fullstop.
 
M23 wako wapi sasa?
Retreating and reorganize ni moja ya mbinu za kivita, inawezekana ilikuwa ni strategic retreat sisi tukaona wameshindwa maana bado wapo wanasumbua na wameweza kuiteka mpaka Goma.
Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom