Katika mazingira yasiyo ya kawaida Manara amuombea msamaha Ally Kamwe sakata la Sandaland

Wengi hawajawaza nje ya boksi kama ulivyofanya.

Naunga mkono hoja. Manaraanatia pilipili kwenye macho ya Kamwe
 
Mimi siyo Mwanasheria. Ila kupitia maelezo yako hapa juu, sioni kama kuna kesi kwa Ali Kamwe. kwa mfano Who is Bwana Sanda? Viongozi wa nini, na akina nani waliomshambulia huyo Bwana Sanda?

Kimsingi hakuna sehemu yoyote ile walipotajwa viongozi wa timu fulani kumshambulia huyo mwekezaji, na sidhani kama huyo mwekezaji jina lake ni Bwana Sanda!!

Kwa hiyo huyo Haji Manara pamoja na hao wanasheria wa Bwana Sanda; wote ni hamnazo.
 
Hamjamuelewa Manara,
Ally Kamwe kaongea,
Sandaland kasema maneno yale ni makosa,
Manara kaja kuomba msamaha kwa yale maneno (makosa),

Hapa ni kua Manara kaja kuthibitisha au kuunga mkono kua kweli Ally Kamwe kakosea. Yaani Manara kabla hata hajakaa na Ally Kamwe yeye katoka hadharani kuthibitisha kua Ally Kamwe alikosea.

Anachofanya hapa ni kum expose dogo tu, na sio kumsaidia. Na kafanya hivyo makusudi tu sababu dogo ndie aliekalia kibarua Cha Manara pale Yanga. Yeye Manara ana uhakika gani kama Ally Kamwe moyoni anajua amekosea??
 
Ila Sandaland naye aliharibu sana kuandika neno SANDA kwenye jezi.
 
ndio maana umeambiwa katika hali isiyo ya kawaida
 
Labda kama katumwa na Ali Kamwe
Kuomba msamaha maana yake ni kukiri kosa.
 
Tatizo hawa wasemaji badala kusemea timu zao wao kila kukicha wazungumzia timu zingine.
 
Ni sahihi. Jamaa kaongeza petrol kwenye moto unaofuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…