Katika nchi 35 zilizokataa kupiga kura suala la Urusi kuvamia Ukraine 50% ni za Afrika, ikiwemo Tanzania

Cha kuchekesha utakuta hao hao tunarud na kuwaomba misaada Kama unataka uwe huku na huku kuwa tajir Kama China nazan bora wasingeenda kwenye hilo azimio
Wanatoa misaada maana wao wanachukua vingi sana kutoka kwetu !! There’s no free lunch !! Makampuni yao yanabeba madini kila kukicha !!
 
Na kuwa na msimamo haina maana watakunyima misaada. Nyerere alikuwa akiwatukana sana Marekani kwa matendo yao dhidi ya Kina Patrice Lumumba, Kwame Nkuruma nk, lakini haina maana Tanzania tulikuwa adui wa USA. Infact Nyerere na Kennedy walikuwa marafiki sana, japo walipingana katika mambo mengi, pamoja na suala la Afrika Kusini ya Makaburu.

Kwa hiyo kumwambia Putin unakosea kuivamia Ukraine hata kama hupendi wanachofanya sioni kwa nini liwe tatizo. Hivi kwa nini watu wanaona huwezi kumshauri rafiki yako anapompiga mkewe kila siku, au kuitelekeza familia yake? Watu wajue huo sio urafiki, ni unafiki, labda kwa kuwa kuna ofa za bia kila jioni.
 
Mkuu umesema kitu ambacho watu wengi hawajui. Warusi ni wabaguzi wabaya wa watu weusi hata kaburu hafai? Hebu google racist killings of blacks in Russia utaona wasivyo watu hawa!
Sasa mkuu, unapigania "rangi" au humanity? Mbona unayumba sasa!!! Hao blacks wanaouwawa Russia ni msimamo wa serikali ya huko au ni mauaji kama yale ya Marekani?
 
Hujanielewa Mkuu. Nilisema hivi kwa watu wanaodhani Tanzania isipinge Urusi kuvamia Ukraine kwa kuwa Warusi ni rafiki zetu wakati Marekani ni wabaguzi wanaua weusi. Ndio nikasema kama hiyo ndio sababu wanayotumia then wajue Warusi ni wabaguzi dhidi ya weusi kuliko hata Marekani. Kuna mtu alisema humu ukiwa mweusi na uraia wa Urusi, hata kama unacheza soka zaidi ya Pele hawatakuweka timu ya Taifa. Hawataki ngozi nyeusi timu zao za taifa
 
Niliweka thread humu JF kwamba suala la Urusi na Ukraine ni dogo sana kwa mtu asie na ukahaba wa kisiasa wa kufuata bwana atakaekupa maslahi bila kujali utu wa mtu huyo.

Nilisema wazi, leo hii wakati tunamkumbuka Nyerere tutafakari angesimamia wapi katika suala la Urusi na Ukraine. Nyerere alisema siku zote mipaka ya nchi zetu inayotambulika kimataifa tunaweza tusiipende, lakini sio sababu za kuvamia nchi nyingine.

Hilo moja, pili ni kwamba, hatupaswi kuwa watumwa wa nchi fulani kwa sababu ya misaada yake, kwamba kwa kuwa tunasaidiwa au tulisaidiwa na nchi fulani, basi hiyo nchi inapofanya mambo kinyume cha maumbile tutakuwa upande wake. Huo ni umalaya wa kisiasa. Dhambi ni dhambi, ifanywe na rafiki au adui.

Angalia kura zilivyopigwa Umoja wa Mataifa juu ya suala la Urusi na Ukraine, na angalia Tanzania ilisimamia wapi. Aibu tupu kwa nchi iliyojiita nchi ya mstari wa mbele kwenye ukombozi wa nchi nyingine. Nasema wazi, tulichofanya hapa ni umalaya wa siasa za kimataifa

Katika hotuba ya mwisho ya Nyerere Umoja wa Mataifa, alisema hiki anachofanya Samia leo hatutafanya hata siku moja! Lakini ndio hivyo tena. Tunafanya. Samia ame-surrender our freedom and dignity. Angalia video hapo chini.

Nchi kama Zambia, Kenya, Rwanda nk wanajitambua sana

View attachment 2387354

Msimamo wa nchi za Afrika juu ya suala la Urusi na Ukraine ni jambo dogo sana linalopaswa kuongozwa na kanuni, sio maslahi ya nchi zetu

Hatuna ubaya wowote na Russia ,kifupi hatutaki kuuziwa Adui,Adui wa wazungu hatakiwi kuwa Adui wa Kila Mtu,
After all Russia ni boss wetu wa zamani kabla Soviet union haijaharibika ,
Pia Russia hata historia yoyote ya kulitawala bara la Africa ,hatuna Sababu yoyote yenye mashiko

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Na kuwa na msimamo haina maana watakunyima misaada. Nyerere alikuwa akiwatukana sana Marekani kwa matendo yao dhidi ya Kina Patrice Lumumba, Kwame Nkuruma nk, lakini haina maana Tanzania tulikuwa adui wa USA. Infact Nyerere na Kennedy walikuwa marafiki sana, japo walipingana katika mambo mengi, pamoja na suala la Afrika Kusini ya Makaburu.

Kwa hiyo kumwambia Putin unakosea kuivamia Ukraine hata kama hupendi wanachofanya sioni kwa nini liwe tatizo. Hivi kwa nini watu wanaona huwezi kumshauri rafiki yako anapompiga mkewe kila siku, au kuitelekeza familia yake? Watu wajue huo sio urafiki, ni unafiki, labda kwa kuwa kuna ofa za bia kila jioni.
Nyerere alikuwa hamuogopi mtu yeyote kumwambia ukweli!!
 
Hatuna ubaya wowote na Russia ,kifupi hatutaki kuuziwa Adui,Adui wa wazungu hatakiwi kuwa Adui wa Kila Mtu,
After all Russia ni boss wetu wa zamani kabla Soviet union haijaharibika ,
Pia Russia hata historia yoyote ya kulitawala bara la Africa ,hatuna Sababu yoyote yenye mashiko

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Nibora tukibaki non aligned!!
 
Watanzania wengi ni vilaza wa kutupwa panapo Geopolitics
Waafrika hawajielewi, hawajui umuhimu wa kuwa na sheria za kimataifa zinazoheshimiwa.

Ndiyo maana hata nchi zetu zenyewe zimejaa madikteta yanayoingia madarakani kwa mapinduzi au wizi wa kura

Halafu kitu kingine tunachokiamini ni kuwa Urusi na China zinawapenda Waafrika, hakuna nchi ya kibaguzi kama Urusi, hata timu ya taifa hawaruhusiwi kuchukua wachezaji weusi
 
Hujanielewa Mkuu. Nilisema hivi kwa watu wanaodhani Tanzania isipinge Urusi kuvamia Ukraine kwa kuwa Warusi ni rafiki zetu wakati Marekani ni wabaguzi wanaua weusi. Ndio nikasema kama hiyo ndio sababu wanayotumia then wajue Warusi ni wabaguzi dhidi ya weusi kuliko hata Marekani. Kuna mtu alisema humu ukiwa mweusi na uraia wa Urusi, hata kama unacheza soka zaidi ya Pele hawatakuweka timu ya Taifa. Hawataki ngozi nyeusi timu zao za taifa
Kama hii statement ni kweli basi mhhh hatari sana
 
Hatuna ubaya wowote na Russia ,kifupi hatutaki kuuziwa Adui,Adui wa wazungu hatakiwi kuwa Adui wa Kila Mtu,
After all Russia ni boss wetu wa zamani kabla Soviet union haijaharibika ,
Pia Russia hata historia yoyote ya kulitawala bara la Africa ,hatuna Sababu yoyote yenye mashiko

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Unaona unavyojichanganya? hatupigi kura kwa sababu hatutaki kuuziwa adui. Kura haikuwa juu ya kuwa adui au rafiki wa Urusi. Kura ilikuwa ni kwa ajili ya "border integrity", kwamba, kitendo cha Urusi kuvamia ndani ya mipaka ya Ukraine na kumega sehemu ya Ukraine ni sahihi au sio sahihi kufanywa na Urusi?

Sasa ukikaa kimya ni kwamba huna akili ya kuamua jambo ndogo kama hilo, au unaogopa kumuudhi bwana wako. Ndio maana nikaita umalaya wa kisiasa
 
Na unadhani hilo ndio lingetufanya tuwapinge Urusi? Bado tungekuwa wapumbavu kama tungetumia hilo kuwa sababu
 
Watanzania wengi ni vilaza wa kutupwa panapo Geopolitics
Yaani hawajui politics kiujumla, hata local politics tu, 80% ni mbumbumbu kwenye hayo masuala

Ukisoma facebook huko watu walivyoamini zile propaganda za jiwe ndio utajua
Labda mpira wa miguu ndio utawakuta wamekariri hadi pasi alizopiga Messi PSG
 
Unaona unavyojichanganya? hatupigi kura kwa sababu hatutaki kuuziwa adui. Kura haikuwa juu ya kuwa adui au rafiki wa Urusi. Kura ilikuwa ni kwa ajili ya "border integrity", kwamba, kitendo cha Urusi kuvamia ndani ya mipaka ya Ukraine na kumega sehemu ya Ukraine ni sahihi au sio sahihi kufanywa na Urusi?

Sasa ukikaa kimya ni kwamba huna akili ya kuamua jambo ndogo kama hilo, au unaogopa kumuudhi bwana wako. Ndio maana nikaita umalaya wa kisiasa
Shida si akili ,ni kura ambayo Haina manufaa yoyote ,upige usipige Attitude ya mzungu kuhusu wewe haibadiliki,

Yaani Kwa kifupi si jambo la manufaa kuonekana una akili Kwa mzungu , Kuna mambo ya msingi ya kushughulika nayo siyo hizo petition za kipuuzi

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Niliweka thread humu JF kwamba suala la Urusi na Ukraine ni dogo sana kwa mtu asie na ukahaba wa kisiasa wa kufuata bwana atakaekupa maslahi bila kujali utu wa mtu huyo.

Nilisema wazi, leo hii wakati tunamkumbuka Nyerere tutafakari angesimamia wapi katika suala la Urusi na Ukraine. Nyerere alisema siku zote mipaka ya nchi zetu inayotambulika kimataifa tunaweza tusiipende, lakini sio sababu za kuvamia nchi nyingine.

Hilo moja, pili ni kwamba, hatupaswi kuwa watumwa wa nchi fulani kwa sababu ya misaada yake, kwamba kwa kuwa tunasaidiwa au tulisaidiwa na nchi fulani, basi hiyo nchi inapofanya mambo kinyume cha maumbile tutakuwa upande wake. Huo ni umalaya wa kisiasa. Dhambi ni dhambi, ifanywe na rafiki au adui.

Angalia kura zilivyopigwa Umoja wa Mataifa juu ya suala la Urusi na Ukraine, na angalia Tanzania ilisimamia wapi. Aibu tupu kwa nchi iliyojiita nchi ya mstari wa mbele kwenye ukombozi wa nchi nyingine. Nasema wazi, tulichofanya hapa ni umalaya wa siasa za kimataifa

Katika hotuba ya mwisho ya Nyerere Umoja wa Mataifa, alisema hiki anachofanya Samia leo hatutafanya hata siku moja! Lakini ndio hivyo tena. Tunafanya. Samia ame-surrender our freedom and dignity. Angalia video hapo chini.

Nchi kama Zambia, Kenya, Rwanda nk wanajitambua sana

View attachment 2387354

Msimamo wa nchi za Afrika juu ya suala la Urusi na Ukraine ni jambo dogo sana linalopaswa kuongozwa na kanuni, sio maslahi ya nchi zetu

Nasimama na nchi yangu katika hili. Ukraine anajizima data! Kazi ya mjinga ni kuumia.
 
Mimi nazipongeza sana hizo nchi ambazo hazikupiga kura kuunga mkono au kupinga hiyo motion ya suala la vita vya Urusi vs Ukraine, pamoja na zilizopinga. Nazipongeza kwa sababu zimeonyesha ukakamavu mkubwa wa kuwaambia hao wababe wa dunia kwamba sisi siyo vikaragosi wao wa kuunga mkono kila uchafu wao.
Ingekuwa ni kuonyesha unafiki mkubwa wa kujali haki za binadamu kama Tanzania, na hizo nchi, zingepiga kura kuunga mkono hoja ya marekani na rafiki zake kuhusu Ukraine, wakati hao hao wamarekani wanaikalia Syria kinyume na matakwa yake. Hao wanaodai haki itendeke kwa Ukraine, walivamia Libya na kumuua Gaddafi bila kujali uhuru wa nchi na wananchi wake kujiamulia mambo yao.
Hao hao walivamia Iraq kwa kutumia sababu za UONGO wa wazi, bila kujari uhuru wa hiyo nchi!
Kama wanatambua uhuru wa nchi kuwepo na territorial integrity, basi walete motion za kukiri kuwa walikosea kwa waliyotenda huko Iraq, Libya, na wanayofanya sasa huko Syria. Watubu kuwa walikosea na walipe fidia kwa madhira waliyowatendea wananchi wa nchi hizo.
Haya mambo ya kunya anye kuku akinya bata kaharisha hayana nafasi ktk dunia ya leo. Enzi zile za ukoloni na ukoloni mamboleo yaliwezekana, lakini sasa hivi ktk dunia ya utandawazi hayana nafasi.
Hongera sana Tanzania kwa kusimia misingi halisi ya haki za binadamu, bila kujali kuwa wenye motion wanatupa misaada kiasi gani. Huo msimamo imara uliasisiwa na Baba wa taifa mwl Nyerere uendelee [emoji1434]
Angalau wewe ndiye niliyekuelewa.
 
Nimeuliza hapo juu, wewe unaweza kuwa na alignment kati ya dada zako wawili?

Sasa ukikuta mmoja wao anampiga mwenzie na kumuumiza akidai kamkosea kwa kufanya urafiki na adui yake, utakaa kimya kwa kuwa huna alignment?
Lazima useme ukweli kwamba wewe fulani umekosea sana kufanya uliyoyafanya !!
 
Back
Top Bottom