Katika nchi 35 zilizokataa kupiga kura suala la Urusi kuvamia Ukraine 50% ni za Afrika, ikiwemo Tanzania

Katika nchi 35 zilizokataa kupiga kura suala la Urusi kuvamia Ukraine 50% ni za Afrika, ikiwemo Tanzania

Najua, ila wasiwasi hapa ni kama wewe Mkuu unajua ninachosema? Alichosema Nyerere na kushangiliwa na kila nchi kwa nguvu sana? Unaelewa?
Mi naelewa vizuri tu, na nakuelewa, ila sjui kama unaelewa. Mbona sasa maamuzi ya Tanzania kwenye mambo ya Urusi na Ukraine yanasmamia kanuni kama aliyoitoa Baba wa Taifa?
 
Teh kisa humsapoti marekani na wenzie
Enyi watu msio na maarifa, hii kura haikuwa kumsupport USA na wenzake, ilihusu kupinga Urusi kuvamia nchi huru kwa lengo la kuchukua sehemu ya nchi hiyo. Mtakosa maarifa hadi lini?
 
Hivi America huwa havamii nchi za watu,,??

Uzi wa kijinga Sana ..
Huwa wanavamia. Kwa hiyo tusipinge Urusi kuvamia kwa sababu USA nao huwa wanavamia? Wewe ndio mjinga shobosho kweli kama hiyo ndio reasoning yako.

Kwa taarifa yako, hata USA wakivamia tunapaswa kupinga.
 
Mwingereza alivyo mpiga Argentina ni sawa ?[emoji3062]
 
Kwanini nchi za kiafrika ziwe na umuhimu kama jambo linawafaidi tu wazungu na siyo vinginevyo?

UN haina nia njema na Afrika and it remains a tool for America and its allies to control other countries.

Of all the organisations, UN is the most bogus institution which must be either restructured or disbanded like yesterday.
Kama sio na UN haina nia njema na Afrika, mnatafuta nini kwenye uanachama wa UN? Jitoeni basi, hamlazimishwi kuwa members.
 
Hamjui Siasa za kimataifa..nendeni mkaangalie Yanga na Simba yenu.

Gadafi alivyouwawa ni sawa?

USA mwenye interest zake Mashariki ni sawa??

Zelensky akivyoonywa asiingie NATO akielezwa Soviet Ina allergy na NATO hamkusikia?? Unadhani ukrane haina raia wenye asili ya Russia? Wanachukizwa na tabia za America?? Kwanini alazimishe kujoin
 
Mi naelewa vizuri tu, na nakuelewa, ila sjui kama unaelewa. Mbona sasa maamuzi ya Tanzania kwenye mambo ya Urusi na Ukraine yanasmamia kanuni kama aliyoitoa Baba wa Taifa?
Si kweli. Kwa sababu Nyerere alisema hatutakaa kimya pale tunapoona ukosefu wa haki. Sasa hapa suala la msingi ni kwamba Urusi kuvamia nchi nyingine na kusema wataimega ni uonevu, hakuna sababu yeyote itakayokubalika nchi nyingine kumega nyinchi huru. Pia, Urusi kuamua kupiga mabomu maeneo ya raia ni uonevu, kwa sababi hata kama vita ina sababu za msingi huwezi kupiga makombora eneo la makazi ya watu eti unawafundisha adabu kwa kubomoa daraja.

Hivi umejiuliza kwa nini Ukraine hapigi makombora maeneo ya raia Urusi japo ana silaha za kuweza kufanya hivyo? NI kwa sababu akifanya hivyo nae atakuwa anakiuka misingi ya haki, na itabidi nchi zote zinazomsaidia kwa silaha ziache kumpa silaha, kulingana na kanuni za haki.

Sasa hayo ndio Nyerere alisimamia. Angewapinga Urusi, na kama Ukraine angepiga makombora nmaeneo ya raia nchini Urusi angewapinga pia

Sasa watu hawaelewi kabisa kanuni za kutofungamana na upoande wowote lakini wanakuwa wa kwanza kubisha. Eti ooh, mbona USA nao walivamia Libya
 
Fair enough....japo pia kutokusmamia upande wowote kwenye hili swala ni njia ya kutokuingilia migogoro tusiyoijua.
Ila nimekuelewa pia kwamba kutokusimamia upande wowote kwenye maswala ya haki ni sawa na kutokutetea haki. Na hilo ni kosa kubwa sana.
 
Mimi nazipongeza sana hizo nchi ambazo hazikupiga kura kuunga mkono au kupinga hiyo motion ya suala la vita vya Urusi vs Ukraine, pamoja na zilizopinga. Nazipongeza kwa sababu zimeonyesha ukakamavu mkubwa wa kuwaambia hao wababe wa dunia kwamba sisi siyo vikaragosi wao wa kuunga mkono kila uchafu wao.
Ingekuwa ni kuonyesha unafiki mkubwa wa kujali haki za binadamu kama Tanzania, na hizo nchi, zingepiga kura kuunga mkono hoja ya marekani na rafiki zake kuhusu Ukraine, wakati hao hao wamarekani wanaikalia Syria kinyume na matakwa yake. Hao wanaodai haki itendeke kwa Ukraine, walivamia Libya na kumuua Gaddafi bila kujali uhuru wa nchi na wananchi wake kujiamulia mambo yao.
Hao hao walivamia Iraq kwa kutumia sababu za UONGO wa wazi, bila kujari uhuru wa hiyo nchi!
Kama wanatambua uhuru wa nchi kuwepo na territorial integrity, basi walete motion za kukiri kuwa walikosea kwa waliyotenda huko Iraq, Libya, na wanayofanya sasa huko Syria. Watubu kuwa walikosea na walipe fidia kwa madhira waliyowatendea wananchi wa nchi hizo.
Haya mambo ya kunya anye kuku akinya bata kaharisha hayana nafasi ktk dunia ya leo. Enzi zile za ukoloni na ukoloni mamboleo yaliwezekana, lakini sasa hivi ktk dunia ya utandawazi hayana nafasi.
Hongera sana Tanzania kwa kusimia misingi halisi ya haki za binadamu, bila kujali kuwa wenye motion wanatupa misaada kiasi gani. Huo msimamo imara uliasisiwa na Baba wa taifa mwl Nyerere uendelee 💪🏽
Asante sana mdau. Nahisi wengi wetu wanadhan hatujui marekan na west kwa ujumla ni waovu kiasi gani. Hadi leo urusi imeingizwa kwenye vita na marekan kwa chokochoko zake. Marekan haitaki kuheshimiana. Sera yake ya unilateralism msiichukulie ya kawaida na salama kwa dunia. Pia tukubari russia ni superpower sio kama nchi zetu za mfano(quasi states). Inahitaji usalama wa nje na ndan.
Russia akishindwa leo na marekan akawa kilanja mkuu wa dunia bila checks and balance tumekwisha. Tatizo kubwa la marekan ni tabia za kijambazi.
I HATE AMERICA,
I HATE HER EVILS SPIRIT!
 
Hamjui Siasa za kimataifa..nendeni mkaangalie Yanga na Simba yenu.

Gadafi alivyouwawa ni sawa?

USA mwenye interest zake Mashariki ni sawa??

Zelensky akivyoonywa asiingie NATO akielezwa Soviet Ina allergy na NATO hamkusikia?? Unadhani ukrane haina raia wenye asili ya Russia? Wanachukizwa na tabia za America?? Kwanini alazimishe kujoin
Heee, hizo ni point za kutoa mbele ya wanaume?

Eti unakasirika na kufura kwa kuwa jirani yako anataka kujiunga Wailamu na wewe hupendi, kwa hiyo unavamia nchi yake na kuchukua watoto wake kwa sababu mke wake na wewe ni kabila moja!

Hlafu unasema watu hawajui siasa za kimataifa?
 
Huna kitu unajiliwaza wewe.

Wewe ni wanaume wanaokubali kuishi na wanaume wanawaochapia wake zao? Jibu.

Je ni mwanaume gani anakubaki kutishiwa? Kama hakuna wewe sio ndio walewale.

Nipe kosa la sadam Hussein

Rais wa Libya amekosea nini Hadi kuuwawa??

Huna jibu la maana ....haiwezekani ukae upande wa Marekani kisa ana nguvu na kujinasibu urusi ana makosa na Marekani) Ukraine Hana kosa. Nonsense
 
Back
Top Bottom