Mimi nazipongeza sana hizo nchi ambazo hazikupiga kura kuunga mkono au kupinga hiyo motion ya suala la vita vya Urusi vs Ukraine, pamoja na zilizopinga. Nazipongeza kwa sababu zimeonyesha ukakamavu mkubwa wa kuwaambia hao wababe wa dunia kwamba sisi siyo vikaragosi wao wa kuunga mkono kila uchafu wao.
Ingekuwa ni kuonyesha unafiki mkubwa wa kujali haki za binadamu kama Tanzania, na hizo nchi, zingepiga kura kuunga mkono hoja ya marekani na rafiki zake kuhusu Ukraine, wakati hao hao wamarekani wanaikalia Syria kinyume na matakwa yake. Hao wanaodai haki itendeke kwa Ukraine, walivamia Libya na kumuua Gaddafi bila kujali uhuru wa nchi na wananchi wake kujiamulia mambo yao.
Hao hao walivamia Iraq kwa kutumia sababu za UONGO wa wazi, bila kujari uhuru wa hiyo nchi!
Kama wanatambua uhuru wa nchi kuwepo na territorial integrity, basi walete motion za kukiri kuwa walikosea kwa waliyotenda huko Iraq, Libya, na wanayofanya sasa huko Syria. Watubu kuwa walikosea na walipe fidia kwa madhira waliyowatendea wananchi wa nchi hizo.
Haya mambo ya kunya anye kuku akinya bata kaharisha hayana nafasi ktk dunia ya leo. Enzi zile za ukoloni na ukoloni mamboleo yaliwezekana, lakini sasa hivi ktk dunia ya utandawazi hayana nafasi.
Hongera sana Tanzania kwa kusimia misingi halisi ya haki za binadamu, bila kujali kuwa wenye motion wanatupa misaada kiasi gani. Huo msimamo imara uliasisiwa na Baba wa taifa mwl Nyerere uendelee 💪🏽