Katika Ukristo Mwanamke anaruhusiwa kuolewa baada ya muda gani toka kufiwa na mume wake?

Katika Ukristo Mwanamke anaruhusiwa kuolewa baada ya muda gani toka kufiwa na mume wake?

Inategemea yeye mwenyewe hata baada ya siku tatu ni sawa ndoa ya kikristo mmja akifa aliyebaki hai yupo huru kuolewa au kuoa tena wakati wowote ,haya Mengine inategemea na busara zake na tamaduni za eneo husika .Ili kuondoa baadhi ya dhana mbaya zinazoweza kujengeka Kwa ndugu wa mume ,Kwa binafsi yangu sio mbaya Kwa mtu kusubiri Kwa walau hata mwaka mmja Ili kuweka mambo sawa mfano mirath.Na vile vile wewe unayetaka kuolewa muda mfupi huyo mumeo mpya umefahamians nae lini?umezijua tabia zake?uchumba unahitaji angalau hata miezi 6 Ili upate fursa ya kumsoma mwenzako vizuri
 
Kwa utaratibu wa Dini ya kikristo, km walifunga ndoa ya kanisani baada ya kifo cha m1, yule anae baki muda huo huo anakua huru kuolewa tena.

Ila kwa taratibu za kwetu, mke ndo ana amua aolewe tena au abaki kuwa mjane, km ana amua kuolewa bas anatakiwa kukaa mwaka m1, ndo aolewe tena.
Hiyo shelia mnaitoa wapi?kwenye biblia au maneno ya kiongozi?
 
Inategemea yeye mwenyewe hata baada ya siku tatu ni sawa ndoa ya kikristo mmja akifa aliyebaki hai yupo huru kuolewa au kuoa tena wakati wowote ,haya Mengine inategemea na busara zake na tamaduni za eneo husika .Ili kuondoa baadhi ya dhana mbaya zinazoweza kujengeka Kwa ndugu wa mume ,Kwa binafsi yangu sio mbaya Kwa mtu kusubiri Kwa walau hata mwaka mmja Ili kuweka mambo sawa mfano mirath.Na vile vile wewe unayetaka kuolewa muda mfupi huyo mumeo mpya umefahamians nae lini?umezijua tabia zake?uchumba unahitaji angalau hata miezi 6 Ili upate fursa ya kumsoma mwenzako vizuri
Hiyo sheria mmeitoa wapi?
 
Inaama wajuzi wa dini leo wa kuja na vifungu vya biblia leo wamechemka? Maana katika Uisilamu hili ni jambo dogo sana, hata kwa mwanamke aliyeolewa halafu akafa bila kuingiliwa na mumewe Mwenyezi Mungu amelielezea vizuri kabisa,

Hata kwa mwanaume aliyefiwa na mke limeelezewa vizuri kabisa.Sasa kitu kidogo hiki watu wanashindwa kujibu na wameowa, wataweza kijibu vikubwa?
 
Naomba kuuliza kwa wakristo,

Mwanamke anaruhusiwa kuolewa baada ya muda gani toka kufiwa na mume wake au baada ya kuachwa? Maana kwa waisilamu pindi mume akifa mwanamke hukaa miezi 4 na siku 10, na taraka hukaa mpaka aingie mwezini mara tatu.
Akivunja ungo
 
Hata kesho yake.
Simu mume anakufa saa hiyohiyo yuko qualified kuolewa.
Mengine ni utamaduni tu
 
Kwa mila hizo za kizungu na kiarabu kwa kweli mie sifahamu,

Ila kwa Mila zangu za kiafrika anatakiwa akae kwao mume hamna tena kuolewa labda arithiwe na ndugu wa mume wako.
Hizo siyo mila za kiafrika sema mila za kabila lenu, ama ukoo wenu.
 
Naomba kuuliza kwa wakristo,

Mwanamke anaruhusiwa kuolewa baada ya muda gani toka kufiwa na mume wake au baada ya kuachwa? Maana kwa waisilamu pindi mume akifa mwanamke hukaa miezi 4 na siku 10, na taraka hukaa mpaka aingie mwezini mara tatu.
1 Wakorintho 7:8-9
[8]Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.
I say therefore to the unmarried and widows, It is good for them if they abide even as I.
[9]Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.
But if they cannot contain, let them marry: for it is better to marry than to burn.

Akijiona pale ambapo hawezi jizuia basi aolewe au aoe.
 
Back
Top Bottom