Katika ulimwengu wa kutafuta pesa kudhulumiwa kawaida sana

Nililizwa na hawa jamaa wanaojifanya sijui TISS 1.5m ili nipate chansi ya kwenda huko kwa wanaokumbuka mwaka 2011 mlandizi kuna Mzee alipiga zaidi ya vijana 40 nahisi kuna wenzangu tupo wote humu

Shikamoo Mzee ukubwa dawa
Bora ulilizwa tu maana Sasa hivi kazi yao ingekua Ni kutoa watu kucha tu.
 
Kuna jamaa yangu tupo chuo mwaka wa tatu semister ya kwanza,alikua anajidai anajuana sana na ma-officet wa kesho,Basi bana kuna officer alimchek ktk nafasi hizi za JKT ipo chance baada ya jamaa angu kumsumbua sana kupata nafasi KWA ajili ya mtoto wa dada ake.

Si wanaambiwa aaandae laki6 then dogo ajiandae na kila kitu kinachofanyika,Dogo akajiandaa na safari inaanza,kufika Kabuki(migambo) jamaa wanawasiliana,akamwambia kuna gari ya chakula inakuja mambieni TOKA stend kabuki,ausubirie hapo ila watumie hyo hela kabisa,Jamaa kweli wanawasiliana saaafi ikabidi atume.Haya dogo akaanza kusubiri gari mpaka saa4 usiku hola na jamaa hapokei simu kabisaaaaaaaa,piga na kupiga holaaaa.

Ikabidi akalale guest asubuhi akarudi zake tu DSM,na ndo ntoleee.Jamaa anamtisha officer eti atamloga maana hela yenyewe ilikua ya boom.

Officer kakausha na kuendelea na mambo take.Mjini challenge za kudhulumiwa kawaida sanaaa,Mi mwenyewe hapa nishadhulumiwa ki150000 kangu nimenyuti tu
 
Mkuu ukiona kazi inanza na mambo ya toa hela ujue umepigwa.
 
Kati ya watu waliopigwa, mimi ndiyo najiona boya kishenzi.

Utapeli wa kuuziwa mche wa sabuni baadala ya simu kila mtu anaujua siku hizi. Lakini mwaka jana nimeuziwa mche wa sabuni kwa sh. 10,000.

Wiki nzima moyo wangu ulikuwa na ganzi.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…