Dodoma.
Mchuchu aliniona natumia simu ya batani ya TECNO T484 akaipenda, nikamwambia tulia nitakununulia.
Siku za mbele katika mizunguko yangu Town nikasimamishwa na msela yuko smart tu, akaniambia ana shida kuna matatizo yametokea, anauza simu yake ya TECNO T528 (jamii ya T484), nikaona yes!, ntaenda kumspraizi mchumba, nikainunua, akanifungia kwenye mfuko.
Niko njiani narudi nikaamua kuikagua kwa furaha, hamadi!!, mche wa sabuni!!, nguvu zikaniishia, ikabidi nikae barabarani pembeni ya lami nusu saa nzima akili ikae sawa. Nilijiona bonge la mjinga. Mchumba sijamwambia hiyo ishu mpaka leo, nimemnunulia mpya dukani.
Nikikumbuka nilivyotapeliwa kiboya wakati mimi mwenyewe mtoto wa mjini roho inaniuma sana.