Katika ulimwengu wa kutafuta pesa kudhulumiwa kawaida sana

Unaweza ukafanikiwa kufanya dhuluma lakini laana au adhabu itokanayo na dhuluma huwezi ikwepa hapahapa Duniani.

Utakuta familia inasamaratika au hata mkiishi ni kimkanda mkanda tu, watoto wanawasumbua kitabia hamuelewani, kuwa mtumwa wa madeni kwa mikopo isoisha, kuharibikiwa vitu mala Gari imegongwa mara vile n.k mara changamoto za magonjwa n.k

Tutubu tuache mabaya tutendeane mema kama alivyoagiza Mwenyezi Mungu.
 
Dah! Kweli hip kiboko. Lakini mnawakamataje mkuu?
 
Tumia unlockbase, kuna siku nililipia Tshs. 72429.84 ili wa-unlock simu, iliposhindikana waliirejesha na wakanitumia email kuhusu kurejesha pesa hiyo, kweli nilipocheck salio lilikuwa limeongezeka.

Sababu ya kushindwa ku-unlock ni kwa kuwa simu ilitengenezwa itumike Marekani pekee (region locked simu), so nje ya Marekani hakuna ujanja.
 
Mkuu mim nlipiga tukia nikatapeliwa 420,000 mpaka hiv sas sitaki kumuamin mtu yoyote kwenye maswala ya kifedha, ama kweli mjini shule yaani unatafuta fursa ya kuingiza fedha kumbe wenzako hiyo shida yako kwao ni fursa, hahahah
 
Mother angu alidead sababu ya kutapewa na best ake wa karibu sana waliekuwa wanafanya nae biashara

Alimpiga kama 4.5mls hiv

Mother alikuw anaumwa so akaona hawezi kwenda mkoani kununua mzigo na huku anaumwa friend akamuambia ampe 2ml then kila week awe anampa faida ya 200k mother akaona sio case nkachukua mzigo nkampelekea week ya kwanza akaleta pesa vizur,ya pili pia akaketa

Akamvaa mother amuongezee 2.5mls ili kila week awe anampa 500k kama faida huku mtaji wake uendelee kubaki pale pale 4.5mls,mother akakubali kiroho safi

Alileta leta pesa ndani ya week 3 after hapo kimya hapakan kwa simu wala nn,ikabidi tumtimbie mpaka kwake kumbe na nyumba yake alisha uza akatembea mother kupata habar akapoteza fahamu sababu ndio pesa alikuwa anazitegemea pia hata kutulipia ada mm na brother wangu
After time pressure ikazidi akapata paralysis upande wa kutosho,safari yake ndio ikaishia hapo niliumia sana

But sikuwa na cha kufanya

Mpaka Leo yule mother cjawah kumuona,juzi nkameet na mtoto wake fb nkamuuliza mother ako yupo,kumbe na yy alishakufa kitambo tu kwa kuuliw na bwana ake akatembea na pesa
 
Ha haa
 
Wangesema ngoja tukamuite wenyewe je?
 
Kasababisha kifo cha mtu na yy kasababishiwa kifo
 
Nimeshatapeliwa Sana Tu. Moja hiyo Kali alikuja Mzee mmoja anajifanya mcheshi nlikuwa nafanya kazi ofisi ya MTU mmoja, kama kabranch hivi. Kabla ya mwaka 2000 akanisalimia akaanza kuuliza watu ambao siwajui ghafla akatoa lundo la picha kwenye hizo picha Yupo yeye na BW Mkapa (RIP), nyingine Yupo yeye Mkapa na Kagame na picha kibao za viongozi wakubwa WA hapa na Nje. Akaniambia yeye Yuko Ikulu ndogo Dodoma na wiki end inayofuata wataenda Bahi kuchukua Mchele hivyo amenitunuku na Mie ataniletea Mchele, SASA itabidi nitoe hela za mifuko Ile mikubwa akapiga mahesabu yake nikampatia mpaka leo nasubiri Mchele WA BURE😁😁😁😁.
 
Kuna mdau amesema Hadi mama yake alifariki baada ya kutapeliwa 4.5mil. Mie yangu sisemi nimetapeliwa Sana kwenye biashara za mazao sina hamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…