Funny boe
JF-Expert Member
- Mar 26, 2023
- 3,637
- 8,214
Habari za wakati huu wana-jukwaa wenzangu,
Maisha ya sasa yamekuwa na kasi sana. Kila mmoja wetu anapambana na majukumu, foleni, kazi, na changamoto mbalimbali za kimaisha. Katika mihangaiko hii yote, ni rahisi sana kujisahau na kupoteza ule utulivu wa ndani (inner peace).
Lengo la uzi huu si kulalamika, bali ni kupeana hamasa na ukumbusho wa upendo. Natamani tufanye uzi huu kuwa "kijiwe cha kupumzisha akili."
Hebu tushirikiane kwa upendo hapa: Ni kitu gani kidogo sana unachokifanya kwenye ratiba yako, au unachokiangalia, kinachokurudishia amani na utulivu wa moyo?
Kwangu mimi, ni ile nusu saa ya asubuhi kabla jua halijachomoza, nikipiga kimoja cha nguvu kwenye utulivu bila kushika simu. Inanipa nguvu ya kukabili siku.
Elewa neno "kimoja cha nguvu"
Karibu ushee chako, huenda ikawa tiba au hamasa kwa mtu mwingine mwenye siku ngumu leo. Upendo utawale! ❤️
Blue Monday
Leo mapovu hayaruhusiwi.