mwombe Mungu atakusaidia, sometimes inakatisha tamaa, sometimes unaweza kuwa na pesa lakini macho yako yameumba hadi Mungu akikufumbua au milango yako ya baraka ikifunguka au wakati wa Bwana unakuwa umeshaika, utajenga hata kama kipato chako kidogo. ila kipato kiwe kikubwa au kidogo, ujenzi una maumivu mno, ukiona mtu ana kwake mheshimu. hela inakutoka balaa unafika kipindi unakuwa kama umemsusia fundi jengo hahahaha.
unashusha nondo la milioni moja hapo hapo anakwambia hapa inatakiwa mifuko 50 ya cement, hapohapo anakwambia kokoto lori kubwa hapohapo mchanga wa kutosha, na hujampa ya ufundi, hapohapo vijana wa kumwagilia, hujamaliza hiki akifika kwenye lenter anakwambia hii inatakiwa iwekwe lenter haraka ili nyumba isitanuke, kwenye lenter hapo maumivu ya kutosha, ukimailza hapo kwenye mbao za kupaulia, roofiing, madirisha na nondo zake, milango, floor/tiles hujapiga lipu hujaweka fensi...., kwa kipato changu cha kawaida kabisa nimeshavumilia maumivu ya kutosha, ila ikiisha, ndio utaona utamu wake.