Katuni ya Masoud Kipanya inamaanisha nini?

Katuni ya Masoud Kipanya inamaanisha nini?

Nimeona katuni ya Kipanya ikionesha Nyoka mkubwa wa Kijani akicheza na Mbwa rangi ya Gwanda na kisha Mbwa yule alimezwa

Wengi wameihusisha katuni hii na siasa za CCM na Chadema

Sisi Wahenga tunakumbuka zamani Vikundi vya Sanaa mfano DDC Kibisa, Muungano nk walikuwa na onesho la Mbwa/Mbuzi kumezwa live na Chatu ukumbini

Ilikuwa inahuzunisha sana hatimaye Serikali ikapiga marufuku onesho lile

Masoud Kipanya kwa katuni ile umenikumbusha nyakati zile tukiishi Mwananyamala Komakoma, kitambo sana!

Jumaa kareem!
 
Wahafidhina mpo wengi sana hata mama alisema
Kabisa.
FqsVdVaWIAAapSB.jpg
 
Naona muendelezo wa katuni za KP kuhusu Chatu na Mbwa series haijaisha ni episode ya 3, nimewaletea episodes zote3 ina one pic
Wakuu njooni na majibu.

FB_IMG_1678426117976.jpg
 
Naona mmemuita Sukuma gang kaamua kubalance ili wote mfurahi .Hope kile chama ambacho hakina makali tena wamefurahi .
 
Kwa hiyo Jo,umeamua kuvuka mipaka kwa kiwango cha kuwa tusi watu,mbali na kuwa unajifichia kwenye katuni uisemayo🤔
 
Mbwa yule alipomezwa alifanikiwa kutoboa tumbo la chatu yule wa KIJANI Kwa mguu,

Hiyo inaitwa "km vp tukose wote".
Kutoboa tumbo umetafsri vibaya,Yaani mbwa kesha mezwa na katoboa tulmbo a chatu ila haoni pa kwenda,Kashamezwa huyo anamalizia tu Pumzi ya mwisho.
 
Ukweli haupigwi teke bwashee
Kama haupigwi teke sawa. kwann wewe hukubaliani na ukweli kwamba magufuli aliiba uchaguzi?

kwamba alinunua ndege bila kufuata kanuni na sheria ya manunuzi?

kwamba alipora korosho za wana wa kusini?

kwamba aliwabambikizia watu kesi na kuwapora mali zao?

ukweli upi unaousema wewe?
 
Kama haupigwi teke sawa. kwann wewe hukubaliani na ukweli kwamba magufuli aliiba uchaguzi...
Hayo ya uchaguzi yashapita ndio maana chadema wameweza kukubali kuchukua ruzuku zenye kutokana na huo uchaguzi, hayo ni matunda ya maridhiano.
 
Kutoboa tumbo umetafsri vibaya,Yaani mbwa kesha mezwa na katoboa tulmbo a chatu ila haoni pa kwenda,Kashamezwa huyo anamalizia tu Pumzi ya mwisho.
Baada ya KIFO Cha mbwa ndani ya tumbo, kinafuatia kifo Cha NYOKA,

Hakuna maisha tumbo likiwa limetobolewa.

Mbona vitu Rahisi hivi huelewi?

Tunahitaji chama mbadala wa CCMM na CDM.
 
Mbwa yule alipomezwa alifanikiwa kutoboa tumbo la chatu yule wa KIJANI Kwa mguu,

Hiyo inaitwa "km vp tukose wote".
Point muhimu ilikuwa pale kwenye kutoboa tumbo.
Na kuna uwezekano mbwa alimuua chatu kwa huo mkono na akatoka salama au walikufa wote
 
Point muhimu ilikuwa pale kwenye kutoboa tumbo.
Na kuna uwezekano mbwa alimuua chatu kwa huo mkono na akatoka salama au walikufa wote
Probability za kupona mbwa na chatu ni:

1. Chatu Ili apone ni kumtapika mbwa na kuzibwa tumbo Kwa treatment za msaada wa Kutoka nje.

2. Kupona Kwa mbwa ni aokolewe na Walio nje Kwa kumuua chatu na kupasua tumbo, jambo ambalo ni nadra. Maana mbwa haezi jiokoa mwenyewe kupitia nafasi wazi tumboni mwa chatu.

In other words, kifo Cha mbwa na chatu Kwa pamoja kitawasaidia wengine.

Chama kipya kinahitajika Kwa maoni yangu,kiandaliwe just in case....

CCM na CDM vikifa, Tanzania itaendelea kuwepo.

Let it be. Amen
 
Tatizo haya maigizo yanatumia gharama kubwa sana za sisi walipa Kodi...,
 
Baada ya KIFO Cha mbwa ndani ya tumbo, kinafuatia kifo Cha NYOKA,

Hakuna maisha tumbo likiwa limetobolewa.

Mbona vitu Rahisi hivi huelewi?

Tunahitaji chama mbadala wa CCMM na CDM.
Waza tena mzee
 
Nimeona katuni ya Kipanya ikionesha Nyoka mkubwa wa Kijani akicheza na Mbwa rangi ya Gwanda na kisha Mbwa yule alimezwa....
Kwa hiyo unataka kusema nini hasa?! Hii huruma against CDM imekujia lini ghafla wewe mfia legacy?!
 
Back
Top Bottom