Katuni za Masoud Kipanya (Special thread)

Katuni za Masoud Kipanya (Special thread)

Hii ni moja kati ya kazi bora za Kipanya, ametumia akili kubwa sana
 
Acha ajifariji. Chadema haitakaa ishinde Urais. Wakitaka kushinda basi wapinzani wote waungane watoe jina moja tu la mgombea.
Sio kujifariji hii kazi inaakisi hata mawazo yako uliyoyatoa hapa, fasihi ya kiwango cha juu sana
 
Upuuzi mtupu,ccm haiwezi toka madarakani kwa kanituni za kipuuzi kama hizi,nendeni kwa wananchi mkauze Sera wananchi wawapime,unadhani tabiri uchwara za kipanya zina nafasi yotote katika kuingoa ccm?
Hujaelewa hiyo fasihi, hata ulichosema kiko humo ndani
 
Kwa hiyo CCM hali ikiwa siyo shwari unadhani Mbowe atashinda Urais?
Hapa hakuna nilipo mtaja mh Mbowe bali ninaombea mgogoro huo uzidi hadi tukaizike rasmi ccm kama marafiki zake UPC na KANU
 
Mbona unashindwa kuelewa Kiswahili rahisi hivyo? Lowassa alivyopewa kupiga penalty 2015 kwa ajili ya UKAWA alifanyje?
Hapo sioni kama hata referee atakuwa yupo hivyo mpiga penalt anaweza kuubeba huo mpira akautumbukiza wavuni na kurudi uwanjani anashangilia na magongo yake
 
Umeeleweka sana mkuu na huu ni wakati wa wapinzani kuutumia vizuri ili hiyo penalt waweze kuitumia kufunga goli maana lango liko wazi
Hapo hakun penalty jmn ni faul hyo ambayo kipi hayupo na mabeki wanazozanaa pale hakuna penalt
 
Nilichokielewa kutokana na hii katuni ya Masoud ni kuwa:-
Pamoja goli lipo wazi lkn huyo mpigaji mwenyewe ni mlemavu hivyo hawezi kutumia nafasi hiyo kupiga na akashinda.

Hii maana yake ni kuwa

Kwa hali ya ccm ilivyo sasa kuna fursa ya wazi kabisa upinzani kushika nchi lkn upinzani wenyewe ni dhaifu kwa hiyo ni ngumu kuitumia fursa hiyo.

Huu ni kama ushauri Sawa na kusema, ikiwa upinzani utaweza kujiimarisha, haya njia nyeupe hiyo hapo ya kuchukua nchi
 
Nilichokielewa kutokana na hii katuni ya Masoud ni kuwa:-
Pamoja goli lipo wazi lkn huyo mpigaji mwenyewe ni mlemavu hivyo hawezi kutumia nafasi hiyo kupiga na akashinda.

Hii maana yake ni kuwa

Kwa hali ya ccm ilivyo sasa kuna fursa ya wazi kabisa upinzani kushika nchi lkn upinzani wenyewe ni dhaifu kwa hiyo ni ngumu kuitumia fursa hiyo.

Huu ni kama ushauri Sawa na kusema, ikiwa upinzani utaweza kujiimarisha, haya njia nyeupe hiyo hapo ya kuchukua nchi
Aisee pongezi nyingi sana zikufikie kwa ķuweza kuitafsiri bila unazi
 
Wapinzani wanashindwa kutumia vizuri Fursa ya mgogoro ndani ya CCM ambao kiukweli umekua mkubwa sana.
CCM walifanikiwa kuisambaratisha CUF kwa dhulma.
Mbinu zile zile za kujenga dhulma zinaendelea kutumika kusambaratishana wenyewe kwa wenyewe.

Hakika Bila CCM kufa kwa muda na kuibuka tena kikiwa Chama chini ya mfumo imara wa Katiba bora itakayoofanya nchi hii ipate viongozi kwa Hoja sio kwa vioja na migogoro.
Tanzania kwa muda mrefu tunanufaika kupata viongozi kupitia migogoro badala ya kupata migogoro kwa Hoja.

Nadhani 2020 iwe Mara ya kwanza kabisa kwa Tanzania kupata viongozi kupitia Hoja zenye agenda ya maendeleo na utaifa.

Hatutegemei kupata viongozi kwa kutumia Migogoro ,hasira, mabomu na kuhujumiana badala yake tutoe Fursa ya kupata viongozi bora kabisa kwa hoja,Historia safi ya kutetea Mali za umma kwa kujitoa sio kwa kushiriki kisha kugeukana.

Wapinzani waungane kwa kujenga itikadi moja kama ile ya Ukawa lakini awamu hii wasiwe na pupa ya Ikulu tu bila kiachiana majimbo na kutumia Rasilimali zao kidogo kuweza kujenga Mtandao.
Mbowe pia ni Tatizo kubwa Mana ana ubinafsi na uroho wa Mali kupindukia.
Hatuwezi kuwa na nchi itakayokuwa kiongozi mkubwa wa Chama mkwepa kodi.
Ikitokea Mbowe kwa uingwana akaachia Chama kwa Tundu Lisu au John Heche na kutoa ushirikiano mkubwa basi CCM ingesambaratika kabisa.

Watu wengi sana wanaipenda Chadema lakini wanamchukulia Mbowe kama MTU asiye na mikakati na mbinu za Kisomi zaidi ya kusubiri matukio ndipo aibuke.

CCM imepoteza dira kwa sasa ila wapinzani wakichelewa wataikuta CCM ikiendelea na safari yake kama kawaida.
Ni Chama kinachocheza na udhaifu wa wapinzani na ujinga wa watanzania.

Mbowe hata jimbo lake ameshindwa kufanya siasa na kuongeza wanachama badala yake wanatimkia CCM na kila kukicha wanazidi kuunga mkono juhudi.
Mbowe amefanya mengi lakini kwa sasa amwachie mwingine.
Akichelewa baada ya mgogoro wa CCM kuisha ataegemee mgogoro mkubwa sana kuobuka Chadema na utakisambaratisha kabisa
 
Mpigaji mwenyewe lisu amevunjwa migui yupo na magogo hata kupiga mpira hawezi

Angapicha vizuri
Mbona kama wameamua kulikimbia goli na hapo mwana cdm anajipanga kupiga penati wakati lango lipo tupu?
 
Nadhani hapo anasema goli lipo wazi Iakini mpigaji wa penalty yuko hoi bin taaban, hawezi kunyanyua hata mguu. Inawezekana wale kule wakamaliza mazungumzo yao kabla hajafanikiwa kusogeza mpira hata kwa Cm moja. Nimejaribu kutafsiri picha tu jamani
Hakuna hisia ngumu [emoji3][emoji3]
 
Goli liko wazi ila sio kwa wapinzani hawa wa TZ, hata hawajielewi.
 
Huyu Ki.nya.pa si ndo yule tuliambiwaga naye aliwananilihi wale wenye nanilihii hadi wakaamua kumnanilihi kwa siku km sio wiki kadhaa?

Nakumbuka wanazengo walinanilihii sana huko twita, mainsta na kwingineko hadi jamaa wakaona isiwe taabu acha wamnanilihii aweze kuungana na ndugu na jamaa au sio huyu yeye?

Au huyu sie ndo yule?
 
Kifupi hamna goli hapo..mabek wameachia goli, ila kibaya zaid mpiga penati ni majeruhi
 
Huna akili
Upuuzi mtupu,ccm haiwezi toka madarakani kwa kanituni za kipuuzi kama hizi,nendeni kwa wananchi mkauze Sera wananchi wawapime,unadhani tabiri uchwara za kipanya zina nafasi yotote katika kuingoa ccm?
 
Back
Top Bottom