EDWARD JOHN
Member
- Mar 9, 2012
- 83
- 183
Habari Wana Jf niende moja kwa moja kwenye point, ni kwamba Mimi na mke wangu tulifunga ndoa miaka sita iliyopita na wakati huo tulikutana mkoani Ruvuma yeye akiwa mwajiriwa wa kampuni flani na Mimi wakati huo nilikuwa nafanya kazi na shirika flani.
Baada ya mahusiano kama ya Mwaka mmoja tuliweza kufunga ndoa, na baada ya miaka mitatu ya ndoa tukaweza kuhamia Jijini Dar es salaam.
Sasa siku moja ilikua ni weekend tupo nyumbani mke wangu aliniambia hivi, mtu ukiwa umepelekwa kuishi mkoani hasa kijijini kama Kule mbinga huwa na akili nazo zinalala uwezo wa kufikiri zaidi unapungua, na ndiyo maana uliweza kunipata na kunioa Ila ingekuwa tumekutana hapa Dar es salaam, wala hilo lisingewezekana.
Sasa tangu hapo nimekuwa nikiwaza sana sipati jibu, nawaza nifanyeje,? Najiuliza je yupo anayempenda kwa dhati? Na je anapanga Nini? Je kubaki nami mpaka Sasa ni kwasababu ya kiapo Cha ndoa tu? yani sielewi, mawazo yenu ndugu zangu.