Kauli hii ya mke wangu ina maana gani?

Kauli hii ya mke wangu ina maana gani?

Ndugu huyo mkeo anawezekana teyari ameanzisha mahusiano nje au ndio anaanza kusaliti ndoa rasmi. Kwa kusema hivyo anatafuta faraja ya moyo wake kuwa ameshakuambia kuwa wewe alikubali umuoe kimakosa kwani wewe sio aina ya mwanaume ampendaye. Pole lakini kubwa zaidi kuanzia sasa kuwa makini sana sana na huyo mkeo.
 
Brother, mna mahusiano kwa zaidi ya miaka 7 na ndoa yenu ina zaidi ya miaka 6, kauli kama hiyo tena ambayo ameitoa siku moja tu ya hiyo weekend kama ulivyosema; Hilo sio tatizo.

Ninakushauri umueleze kuhusiana na kauli yake hiyo aliyowahi kukutolea, kisha mlizungumzie hilo jambo na maisha na ndoa yenu iendelee.

Kuna walio tamkiana maneno mabaya zaidi ya hayo lakini haimaanishi hawapendani, la hasha!
 
Dah Yani mkuu Sasa nawaza sana watoto 3, na bibi yao ambaye ni mama yangu ambaye naona angeweza Kaa nao wakati Mimi napambana kuwatafutia ridhki ya kila siku Alisha tangulia mbele za haki, nawaonea huruma kuja kulelewa na mama mwingine, na ukimwachia aende nao hujui huko kwingine Nini kitawasibu
 
Mkuu, maana yake ni kuu umeshuka thamani mbele yake. Yaani kipindi mna oana ulikua wa thamani kubwa ilio mvutia na kumfanya kua nawe.

Sasa cha kufanya hapo ni kua pambana kujiongezea thamani. Fanya kazi na mishemishe za kukuingizia kipato ×3 ya sasa, weka mwili wako katika umbo la kuvutia ( fanya mazoezi ) , tafuta marafiki na washauri wenye busara. Na mwisho kabisa punguza matamanio ya sex kwake.

Kila la heri mkuu, Ndoa ina changamoto zake na ndoa ni vita unayotakiwa kushinda.
 
Dah nakupata mkuu,
 
Ni kweli kakosea kusema haya maneno lakini aliyasema kwenye mazingira gani? Kama kumekuwa na ugomvi baina yenu na hakuna amani kabisa ni sahihi wewe kuiona kama red flag. Lakini kama kumekuwa na amani baina yenu..na ni mke mwema kwako dont overthink hiyo maneno alosema....itakuondolea raha.

Ukiwa mtu wa kuanalyze kila neno, tendo, decision, choice za your partner..mke ama mume, utakuwa mtu wa hasira sana moyoni, uchungu utapata kao katika maisha yako. Jifunze kupuuzia mambo..ili uwe na amani. Ukiwa na amani, utaweza kufanya kazi zako vizuri..as long as anafanya majukumu yake kwako na watoto na familia kwa ujumla, potezea hiyo statement.

Wanawake kuna muda kuna kama kakichaa huwa tunacho. Na kila mwanamke hakosi haka kakichaa..sema tu inategemea kitatokaje, mwingine kwa kuongea maneno yasiyo na idadi, mwingine kwa kuropokwa kwa nguvu, mwingine kwa kwenda kupeleka poonani nje anyooshwe ili akili imkae sawa, mwingine alewe mpaka apelekwe nyumbani, mwingine kwa kutukana matusi makubwa, mwingine kwa kulia sana kwa uchungu.na mwingine kwa kuondoka nyumbani kwake, kibaya kuna mwingine mpaka aone damu au mme wake kazimia au kaumia ndo na yeye atatulia.

Sasa kwenye uchumba si rahisi sana kuyaona haya..hata kama mmedate miaka mitano sijui mkaishi pamoja..kuna kale katabia ama kakichaa katajificha, sasa isitokee mkaoana maana si utaona "ooh huyu nimemjua vizuri nishajua madhaifu yake yote na anafit kuwa mke wangu unaoa"...hahaahahaha...mambo ndo yanakuwa yananoga..wapare wanasema yanora. Utaanza sasa kuona zile rangi. Kwaiyo aso hili ana lile. Pima mwenyewe!!
 
[emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]daahh...anakudharau Sana huyoo [emoji16][emoji4][emoji4][emoji16][emoji16][emoji16]!!!pole
 
Habari Wana Jf niende moja kwa moja kwenye point, ni kwamba Mimi na mke wangu tulifunga ndoa miaka sita iliyopita na wakati huo tulikutana mkoani Ruvuma yeye akiwa mwajiriwa wa kampuni flani na Mimi wakati huo nilikuwa nafanya kazi na shirika flani.

Baada ya mahusiano kama ya Mwaka mmoja tuliweza kufunga ndoa, na baada ya miaka mitatu ya ndoa tukaweza kuhamia Jijini Dar es salaam.

Sasa siku moja ilikua ni weekend tupo nyumbani mke wangu aliniambia hivi, mtu ukiwa umepelekwa kuishi mkoani hasa kijijini kama Kule mbinga huwa na akili nazo zinalala uwezo wa kufikiri zaidi unapungua, na ndiyo maana uliweza kunipata na kunioa Ila ingekuwa tumekutana hapa Dar es salaam, wala hilo lisingewezekana.

Sasa tangu hapo nimekuwa nikiwaza sana sipati jibu, nawaza nifanyeje,? Najiuliza je yupo anayempenda kwa dhati? Na je anapanga Nini? Je kubaki nami mpaka Sasa ni kwasababu ya kiapo Cha ndoa tu? yani sielewi, mawazo yenu ndugu zangu.
Ukiona manyoya jua keshaliwa huyo. Na dalili ya mvua ni mawingu. Juhadhari kabla ya ajali.
 
😀😀😀😀😀

Yaaani hakuwaza kama angetoka kule kijijini ko alikukubaliantu asije kuzeeka single bure

Ila kwa sasa yuko daslama anaona type alizokua anazitaka pengine yuko in rooooooveee na LOML wake au pengine aliropoka tu

Ila wanawake sisi 😀😀😀
 
Tuliangalie kwenye muktadha mwingine.Naona kama ni utani ambao sio wa kuutilia manani.
Endelea kumpenda tuu aelewe kwamba ulimanisha ulivyoamua kumuoa.kauli zingine huwa shetani anaziingiza kwa wenza ili kuharibu utulivu.

Kama amekuchoka,vitendo ndiyo vingeongea
Kwenye ndoa huwa hakuna utani wa kijinga na maudhi km huo. Huyo anamaanisha
 
Pole sana mkuu unakaribia kuwa mpweke muombe sana MUNGU
JamiiForums-382154248.jpg
 
Habari Wana Jf niende moja kwa moja kwenye point, ni kwamba Mimi na mke wangu tulifunga ndoa miaka sita iliyopita na wakati huo tulikutana mkoani Ruvuma yeye akiwa mwajiriwa wa kampuni flani na Mimi wakati huo nilikuwa nafanya kazi na shirika flani.

Baada ya mahusiano kama ya Mwaka mmoja tuliweza kufunga ndoa, na baada ya miaka mitatu ya ndoa tukaweza kuhamia Jijini Dar es salaam.

Sasa siku moja ilikua ni weekend tupo nyumbani mke wangu aliniambia hivi, mtu ukiwa umepelekwa kuishi mkoani hasa kijijini kama Kule mbinga huwa na akili nazo zinalala uwezo wa kufikiri zaidi unapungua, na ndiyo maana uliweza kunipata na kunioa Ila ingekuwa tumekutana hapa Dar es salaam, wala hilo lisingewezekana.

Sasa tangu hapo nimekuwa nikiwaza sana sipati jibu, nawaza nifanyeje,? Najiuliza je yupo anayempenda kwa dhati? Na je anapanga Nini? Je kubaki nami mpaka Sasa ni kwasababu ya kiapo Cha ndoa tu? yani sielewi, mawazo yenu ndugu zangu.
Mjini kuna watanashati wa kufa mtu. Pamba kali mitoko kama yoote. Yeye anaiona anadhani ndio maisha hayo🤣🤣
 
Kiufupi inaonekana ameshapata exposure ya kutosha na akikuweka kwenye mizani kulinganisha na vijana wenzio wa rika lako wanaomtongoz tongoza hapa mjini unaonekana uko nyuma sana kwa kila kitu, kifedha, kiusafiri, spending pattern yako.

Ila kwa kipindi kile kule Mbinga wewe ndio ulikuwa top of the class ya wanaume aliowahi kutoka nao coz wengi walikuwa wachimba chumvi tu.

Stay alert sababu inaonekana ame loose attraction na wewe. Kuna mtu anakaribia kumla mkeo na akishamla huenda mke akachange vibaya mno akakupiga marufuku hata ya kummbato na kuanza migogoro. Mwisho ni kuachana tu sababu mwanamke anajuta kuolewa na wewe huna maisha.
 
Back
Top Bottom