Kuendelea kumkamua maziwa ng'ombe bila kumhudumia kwa malisho na maji itafika wakati hata maziwa yake yatakata. Kusudio lako litakosa tija na kuchochea masuala hasi yasiyotegemewa. Kwa mfano, nchi yenye utitiri wa kodi au kodi kubwa haiwezi kuvutia wawekezaji wa maana. Watakaopatikana watakuwa wale wajanja na wakwepa kodi. Kwa upande mwingine, utozaji kodi inabidi uendane na kuchukuliwa hatua za makusudi za kuongeza uzalishaji/kipato cha mwananchi kwa ujumla.Huyu mama alianza kulazamisha ili swala muda mrefu utasikia vitu vitapanda bei nauli na kila kitu. Badala ya yeye kukemea upandishwaji hovyo wa bidhaa yeye ndio anabariki.
Serikali wanataka kutumia mwanya huu wa kupanda bei kwa mafuta kuongeza kodi na tozo kimya kimya ili wavune pesa