Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
CCM ndiyo inayoongoza Serikali. Lolote baya au zuri linalofanywa na Serikali, CCM inabeba uhusika mkuu.
Jukumu la kwanza la msingi kabla ya mengine yote kwa Serikali yoyote halali Duniani, ni usalama wa wananchi wake.
Katika kipindi hiki cha awamu ya 6, tumeshuhudia uovu wa ajabu kabisa wa utekaji na mauaji ya watu, na utekaji na upotezwaji wa watu; na wote wanaofanyiwa uharamia huo ni wale ambao ama wanamkosoa Rais au wanaikosoa Serikali yake. Na katika yote, Serikali na CCM ndio wamekuwa wakinyoshewa kama watuhumiwa wakuu, huku baadhi ya viongozi wa CCM (kama yule wa UVCCM Kagera), akisema wazi kuwa kama watu wanaoikosoa Serikali na Rais, wakipotea, polisi wasiwatafute. Lakini pia kuna matukio ya wazi kama yale ya uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2024, ambapo vyama vya upinzani na wananchi kwa ujumla walihujumiwa kwa kiwango cha ajabu, hadi kwa mara ya kwanza, wagombea wa vyama vya upinzani kuuawa na polisi (mfano ni yule mgombea wa CHADEMA kule Singida).
Fikiria katikati ya uovu huu mkuu dhidi ya ubinadamu, CCM inakuja na kauli ya UTU NA KAZI!! Ni utu gani ambao CCM inausimamia? Ni huo wa 'kama wapinzani wakimkosoa Rais, wakipotezwa, Polisi wasiwatafute"? Ni huu wa wanaoikosoa Serikali na Rais kutekwa na kuuawa au kutekwa na kupotezwa; bila ya watuhumiwa kukamatwa? Ni huu wa kuengua wagombea wa upinzani na kupora haki ya wananchi kuwa ya kuwa na machaguo katika uchaguzi? Ni huu wa kuua wagombea wa upinzani? Ni ule wa kukataa maoni ya wananchi na taasisi mbalimbali juu ya muundo wwa Tume Huru ya Uchaguzi? Ni ule wa kuouuza maoni ya wananchi juu ya rasilimali zao asilia wanazogawiwa wageni??
Kauli mbiu ya CCM uchaguzi 2025 inatengeneza maswali mia dhidi yake kuliko kumvutia mwananchi yeyote mzalendo anayelipenda taifa lake bila unafiki wala uchawa.